La Ultima Letra - (Tahadhari: Picha zilizomo zinaogofya)

La Ultima Letra - (Tahadhari: Picha zilizomo zinaogofya)

Dah ona sasa post ya jana naiona saa hizi. Kitu safi nasubiri muendelezo mkuu.
Mkuu hii post aliipost tokea jana ila mods waliiweka pending.
239498075896f70eeaa8b2e49e4bbedb.jpg

Hivyo hujachelewa...
Enjoy
 
Muhimu: Makala hii ndani yake ina maelezo na picha zenye kuogofya na ukatili. Soma kwa tahadhari binafsi. (reader’s discretion is strongly advised)



LA ULTIMA LETRA.


View attachment 464318

C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg



Katika wiki ambayo Taifa zima la Mexico likiwa limeingia katika hofu kuu kutokana na wafungwa 130 ambao wanatambuliwa na serikali kama "watu hatari kupindukia" (extremely dangerous) wakiwa wametoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Matamoros katika mji wa Tamaulipas, ndipo papo hapo ambapo pia Mwendesha mashitaka wa serikali Bw.Ricardo Castillo anapokea simu kutoka kwa askari waliopo eneo la Nuevo Laredo wakimtaarifu juu ya tukio lingine la kuogofya ambalo kwa hakika lazima nalo litalitumbukiza zaidi nchi ya Mexico katika hofu kuu.

Polisi walimtaarifu Bw. Castillo kuwa asubuhi hiyo wananchi wamekuta miili ya watu 9 ambayo kati yao wanne wakiwa wanawake ikiwa imening'inizwa darajani pasipo uhai.

Kitu cha kuogofya zaidi miili hii ilining'inizwa bila vichwa kuwepo katika viwili wili vyake. Pia miili ilikuwa imetobolewa tumboni pamoja na kukatwa katwa mabegani kiasi cha mifupa kutokeza nje.
Pia miili ya maiti hizo za wanaume ilikuwa imenyofolewa sehemu za siri.

Castillo akawauliza polisi kama kulikuwa na kitu chochote eneo la tukio kinachowawezesha kung'amua watekelezaji wa tukio hilo na polisi wakamjibu kuwa kuna ujumbe wa maandishi yameandikwa kwa damu katika kuta za daraja.

Kabla polisi hawajamueleza Kikichoandikwa kwenye kuta za daraja, Castillo anapigiwa simu nyingine na kamanda wa polisi kutoka eneo la Monterrey kumuarifu kuwa usiku wa kuamkia siku ya leo katika klabu maarufu ya usiku ya mjini hapo imevamiwa na watu 52 wameuawa kikatili.

Kamanda huyo wa polisi akaendelea kumueleza zaidi kwamba mauaji hayo ni ya kutisha na kuogofya kwani miili yote hiyo 52 imekutwa ikiwa imefungwa kamba mikononi na yote haina vichwa.

Castillo akakumbwa na mshituko na kuishiwa nguvu na akamuuliza kamanda wa polisi kama kulikuwa na chochote zaidi eneo la tukio, na kamanda wa polisi akamjibu kuwa kulikuwa na maandishi ukutani ndani ya klabu yameandikwa na damu. Lakini pamoja na hilo miili yote ilikuwa imechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'.
Castillo akapigwa na bumbuwazi zaidi akakata simu akimuahidi kamanda wa polisi kuwa anampigia baada ya dakika chache.

Baada tu kukata simu Castillo akapiga simu kwa afisa wa kwanza wa polisi aliyeko Nuevo Laredo ambaye alimpigia simu ya kwanza.

Baada ya afisa huyo wa polisi kupokea simu akamuuliza haraka kwamba ukiachikia mbali maandishi yaliyoandikwa kwa damu kwenye kuta za daraja je kulikuwa na kitu kingine chochote kwenye miili ya maiti hizo. Afisa wa polisi akamjibu "ndio maiti zote zimechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'"

Castillo akashikwa na hofu kubwa na mshangao na akamjibu kwa kifupi tu afisa huyo wa polisi "Niko njiani nakuja, nadhani nimeshafahamu waliotekeleza tukio", afisa wa polisi akamuuliza "ni nani?" castillo akamjibu kwa ufupi.. "Los Zetas

C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image003.jpg




View attachment 464323
Moja ya maeneo ya tukio ambapo wapinzani wa Gulf Cartel waliuwawa kwa ukatili wa kutisha na kukatwa katwa kila kiuongo mahali pake.



1999: Tamaulipas, Mexico

Bw. Cardenas Guillen, miezi michache baada ya kukabidhiwa uongozi wa genge la mihadarati la Gulf Cartel lengo la kwanza alilo jiwekea ilikuwa ni kutwaa tena upya maeneo yao ya kibiashara katika miji yote ambayo hapo zamani yakikuwa chini ya himaya yao lakini wakapokonywa na genge la Sinaloa Cartel.

Ili kufanikisha azma hii Cardenas aling'amua wazi kuwa inahitaji kikosi maalumu cha Ulinzi kwa ajili ya kulinda viongozi wa genge lake, kulinda 'biashara' yao pamoja kusambaratisha mawakala wote wa Sinaloa Cartel katika miji ambayo atailenga.

Ni hapo ambapo aliwasiliana na Ruben Salinas Luteni mstaafu wa kitengo maalumu cha Operation za weledi wa hali ya juu cha Jeshi la Mexico kilichoitwa GAFE (Grupo Aeromovil de Feurzas Especiales).

Baada ya kuwasiliana naye na kufanikiwa kufanya naye kikao maalumu akamueleza juu ya azma yake na kumuomba kumsaidia kutengeneza kutengo maalumu cha kijeshi ndani ya genge lake la Gulf Cartel, kwa ajili ya ulinzi na kusambaratisha wapinzani wake kibiashara.

Luteni Salinas akakubaliana na ombi la Boss Cardenas wa Gulf Cartel na akamuahidi kuunda kikosi cha kijeshi chenye weledi na ufanisi kuliko kikosi chochote cha uhalifu dunia ilichowahi kukiona.

Luteni Salinas akatumia uzoefu wake wa kijeshi kushawishi wanajeshi wengine 30 kutoka vitengo vya kijeshi vya weledi na oparesheni maalumu katika jeshi la Mexico, wakajiunga naye kuunda kikosi maalumu cha kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa viongozi wa Gulf Cartel na kusambaratisha washindani wote wa Gulf Cartel.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kikundi ambacho kilikuja kuwa tishio kwa ukanda mzima wa Amerika ya kusini, kutawala biashara nzima ya mihadarati nchini Mexico na kuingiza hofu isiyomithirika katika jamii Mexico kiasi kwamba hata muandishi wa habari au mtu mtaani aliogopa kutamka jina lao.

Wenyewe walijiita "Los Zetas"



View attachment 464325
C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image005.jpg

Masalia ya viungo vya Wanachama wa Sinaloa Cartel walio katwa katwa viande kama wanyama.



La Ultima Letra

Ndani ya miezi miwili luteni Salinas alikuwa amefanikiwa kuwasiliana na wanajesh 30 ambao walikubali kujiunga naye na kutengeneza kitengo cha kijeshi ndani ya genge la Gulf Cartel.
Wanajeshi hawa ambao luteni Salinas aliwachagua walikuwa ni wale pekee ambao walikuwa wamepatiwa mafunzo ya weledi wa hali ya juu katika jeshi la Mexico.

Kwa mfano, kulikuwa na wanajeshi ambao walikuwa wamepata mafunzo yao kutoka katika kikosi maalumu cha kijeshi cha nchi ya Israel (Israel Special Forces Units) na wengine mafunzo yao waliyapata kutoka katika vikosi maalumu vya jeshi la Marekani (American Special Forces).

Baada ya kukutana na kujadiliana kuhusu namna watakavyo endesha shughuli zao ndani ya genge la Gulf Cartel, moja ya washiriki aliyeitwa Arturo Decena akapendekeza kwa wenzake kwamba, kwa kuwa watakuwa wanaendesha shughuli zao katika mtindo wa kijeshi basi ni vyema hata kikosi chao wajiite jina la kijeshi na akapendekeza waitwe 'Los Zetas' (The Z's).

Ni kwamba, Katika mfumo wa mawimbi ya simu ya kijeshi (military radio airwaves) nchini mexico, kamanda mwenye ngazi ya juu kabisa kwenye eneo husika huwa anatambuliwa kama 'Z' katika mawasiliano ya simu za jeshi.
Ndio kusema kwa mfano kamanda wa ngazi ya juu kabisa ataitwa 'Z 1' anayemfuatia kwa cheo atakuwa 'Z 2' anayefuatia 'Z 3' vivyo hivyo na kuendelea.

Hii ndio ilikuwa maana halisi ya wao kujiita 'Los Zetas' (The Z's) wakimaanisha kuwa kikosi chao wanakifananisha na mkusanyiko wa wanajeshi makamanda wa ngazi za juu kabisa wenye weledi wa kutosha.
Pia wao wenyewe ndani kwa ndani walipenda kuitana jina la utani 'la ultima letra' (herufi ya mwisho).




Angelitos (Malaika Wadogo)

Baada ya kikosi cha Los Zetas kuwa kimezinduliwa rasmi baada ya kikao hicho, Arturo Decena ambaye alipewa jina la fumbo (code name) Z 1, alipewa wadhifa wa kuwa kamanda Mkuu wa Los Zetas.
Kisha kila mwanachama kati ya wanachama wote 31 akaamuriwa kutafuta vijana wasiopungua 8 wenye uzoefu au waliowahi kupitia jeshi au polisi.

Kila mmoja kati ya wanachama hao 31 akaleta vijana hao wasiopungua 8 hivyo wakapata vijana waliokaribia 300.
Gulf Cartel ikatengeneza kituo kijeshi maeneo ya mpakani na Guatamala kinachofanana kabisa na kituo cha kijeshi cha serikali. Kituo kilikuwa na kila kitu kinachohitajika kukidhi matakwa ya kuwa kituo cha kijeshi.
Kisha vijana hawa wapatao 300 wakapelekwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.

Kumbuka vijana hawa karibia wote walikuwa na uzoefu wa polisi au jeshi lakini katika kituo hiki walipatiwa mafunzo maalumu ili kuwapatia weledi ju kazi watayoenda kufanya kwa "mwajiri" wao mpya, Gulf Cartel.

Mafunzo hayo yalihusisha ushushu (intelligence gathering),utekaji (kidnaping), ulinzi maalumu, utesaji (torturing) na namna ya kudhibiti serikali za mitaa (local authorities).

Baada ya vijana kuwiva katika mafunzo waligawanywa tena kwa makamanda wakuu 31 ambao waliwatafuta na kuwaingiza Gulf Cartel. Kila kamanda alipatiwa vijana wasiopungua 8 na yeye kamanda pamoja na vijana wake wakapangiwa sehemu ndani ya mexico ambayo wataenda "kufanya kazi".

Makamanda hawa 31 waliwaita vijana wao waliopewa 'Angelitos' (little angels (malaika wadogo)).

Baada ya Makamanda na 'malaika' wao kugawanywa kwenye maeneo waliyopangiwa kwenye miji tofauti tofauti ndani ya mexico, kazi ikaanza.



View attachment 464326 .
Mmoja wa Angelitos. Kijana mdogo mpiganaji chini ya makamanda wa Los Zetas.


Agizo kuu ambalo walikuwa wamepewa ilikuwa ni kusambaratisha mawakala wote wa Sinaloa Cartel ambayo ilikuwa chini ya El Chapo.
Makamanda wa Los Zetas walipoingia katika miji waliyopangiwa walifanya kazi kama Kikosi maalumu cha kijeshi cha wanamaji wa marekani (Navy SEALs) kutokana na mbinu walizotumia na ufanisi wa hali ya juu katika kutekeleza matukio yao.

Kwanza kabisa walikusanya taarifa za muhusika (wakala wa Sinoloa Cartel na wenzanke katika mji husika) kwa mbinu za 'kishushushu'. Walikusanya taarifa na kujua kila nukta ya maisha ya mtu wanayemlenga. Walijua mahali anapoishi, familia yake, sehemu anazopenda kutembelea, mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine zaidi ya mke wake kama ameoa, n.k.

Baada ya kujipatia taarifa za kutosha, Kamanda wa Los Zetas na 'malaika wake' walimteka muhusika na kutokomea nae mahali kusikojulikana. Wakiwa huko, wanamtesa muhusika kwa siku kadhaa ili atoe siri za viongozi wa Sinaloa Cartel pamoja na washirika wao.

Baada ya mateso ya siku kadhaa kinafuata kitendo cha kinyama ambacho ndicho hasa kinaifanya nchi nzima ya Mexico kuwaogopa Los Zetes na kuifanya nchi kuwa kama Jehanum duniani.

Muhusika aliyetekwa pamoja na wenzake wanaingizwa kwenye chumba maalumu wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi usoni. Wanaongozwa mpaka kwenye ukuta mmoja wapo wa chumba hicho ambapo kwente ukuta kunakuwa na kitambaa kikubwa cheupe kimening'ninizwa kwenye kuta kikiwa na maandishi ya kuisifu Los Zetas.
Baada ya hapo mtu huyu na wenzake waliotekwa wanapigishwa magoti mbele ya kitambaa hicho na Camera ya kurekodi video inawashwa.

Baada ya Camera kuwashwa Makamnda wa Los Zetas wakiwa wameficha sura zao kwa kuvaa 'kininja' wanatoa maelezo ya kuwaonya wanachama wengine wa Sinaloa Cartel kuwa kitakachotokea muda huo ndicho hicho hicho pia kitawakuta wanachama wengine wote wa Sinaloa Cartel kwenye kila pembe ya Mexico.

Kisha Makamanda na 'malaika' wao wanachukua sime na kuwakata vichwa mateka wao mmoja baada ya mwingine kama wanachinja Kuku na tukio hili linarekodiwa kwa ufasaha kwenye video na baadae video hiyo inawekwa kwenye mtandao kufikisha Ujumbe kwa ulimwengu mzima na Mara nyingi miili ya waliochinjwa ulitupwa katika barabara kuu au kuning'inizwa kwenye madaraja.

Matukio haya yaliyotekelezwa na Los Zetas yalileta taharuki ndani ya Mexico kwani matukio yalitekelezwa katika tarikbani miji 15 ya Mexico ambapo makamanda hawa na 'malaika' zao walitawanywa.

Ndani ta miezi michache taharuki ilikuwa kubwa kiasi kwamba washirika na mawakala wa magenge mengine ya mihadarati walidiriki kuyakana magenge yao na kujiung na Gulf Cartel kwa kuogopa kuchinjwa hadharani Los Zetas na kikundi cha ulinzi cha Gulf Cartel.

Pamoja na mamilioni ya madola waliyokuwa wanalipwa Los Zetas kutoka kwa Gulf Cartel, wakaamua watumie mbinu na uwezo wao wa kijeshi kujiongezea mamilioni zaidi.

Los Zetas wakaanzisha mfumo ulioitwa "Pisos".
Mfumo ambao ulikuja kuigwa na magenge mengine karibia yote hapo baadae.

Je, unafahamu mfumo huu ulihusu nini na ulifanyaje kazi??

Nitarudi kumalizia.. stay tuned.!!




The Bold
Hukuni tag kwa hasira nime quote uzi wote but big up dude so genius indeed The bold
 
Daaaahh.! Drugs dealin huwa ni kama aptocalpto ukikaa vibaya watu wanakutoa uhai kama kuku vile.
 
Mkuu The bold umetuacha na Arosto wengine, aka ka mfumo kakutomaliza kametokea wapi tena?
But all in all Hongera & Asante kwa Kuukaribisha mwaka, let's keep on waiting segment inayofuata...
 
Back
Top Bottom