John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Laana Inatajwa Sana. Ni kitu Gani.
Neno laana liko kwa namna mbili, kibiblia.
Aina ya kwanza, ni kupoteza sifa ya kukubaliwa na Mungu kwa jambo lolote lile. Na hii chanzo chake ni lile anguko la mwanadamu tangu mwanzo.
Aina ya pili, ni apizo alitoalo mwanadamu kwa mwenzake, au alitoalo Mungu mwenyewe kwa mwanadamu, ili afikiwe na ubaya fulani, au asifikiwe na mema aliyokusudiwa.
Laana aina ya kwanza
Laana hii ya kwanza, inatokana na asili yetu, ambayo ilionekana tangu Adamu, kuhasi maagizo ya Mungu, ambayo hata sisi sote tuliopo leo, asili hiyo ipo ndani yetu. Ni sawa na unavyomwona mdudu kama mende, ukimtazama tu tangu akiwa mtoto, utamchukia hata kabla hajaonyesha hali yake ya kupenda uchafu, kwa sababu unajua asili hiyo ipo ndani yake. Atakuja kuwa mchafu tu.
Ndivyo ilivyo kwetu sisi, Tayari Mungu alishaona tangu tunazaliwa, kuwa tutamuasi tu, mfano wa baba yetu Adamu.
Na ndiyo maana akaandaa mpango wa kuzaliwa upya mara ya pili, kupitia Yesu Kristo. Hivyo mtu yeyote anayezaliwa mara ya pili, anaondolewa katika laana hiyo ya kukataliwa na Mungu, na anakuwa mwana wa baraka. Laana hii haiwezi kuondoka bila damu ya Yesu.
Hiyo ndiyo sababu maandiko yanasema Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu. Maana yake ni kwamba, tunapokombolewa na yeye, tunafanywa kuwa watu wengine kabisa wenye asili nyingine wasio na laana, wenye kukubaliwa na kupendwa na Mungu.
Katika Wagalatia 3: 13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Hivyo wewe kama umeokoka, na kupokea Roho Mtakatifu, unaitwa mbarikiwa, unaitwa mtoto wa Mungu kwelikweli.
Laana aina ya pili, ipo katika maapizo ambayo huyatoa Mungu mwenyewe au mwanadamu.
A. LAANA ZINAZONENWA NA MUNGU
Mungu anaweza kukutamkia laana, hata kama utakuwa umekombolewa na yeye. Unaweza kushiriki mabaya. Laana hizi zinaweza kukufanya usipoteze wokovu wako, lakini zikakukosesha mambo mengi sana duniani.
Kwa mfano, zile laana alizowaambia wana wa Israeli, kwamba watakapoacha sheria zake, basi watatawanywa katika mataifa yote, watakuwa mikia na siyo vichwa, nchi itazuliwa baraka zake, wataondokeshewa adui zao, n.k. (Kumbukumbu 28:45)
Mfano mwingine ni kama ile aliyoilaani nchi, na nyoka pale Edeni. Akasema ardhi itatoa miiba, na nyoka atakwenda kwa tumbo (Mwanzo 3:14, 17). Pia, kwa kumwambia Kaini kuwa atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani (Mwanzo 4:12).
Wapo watu wengi wanaokutana na maapizo hayo ya Mungu kwa kufanya dhambi au MAKOSA YA MAKUSUDI. Namna ya kueupuka laana hizi ni kutii agizo la Mungu. Ukizizoea, zitakufanya uangukie kabisa kwenye kundi lile la kwanza la kukataliwa kabisa, la watu ambao hawajaokoka.
Waebrania 6: 4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena, hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. 7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
Mifano ya laana za Mungu
1. Mungu alimlaani yule nyoka kwa kwa sababu ya kuwadanganya Adamu na Hawa (Mwa 3:13-15).
2. Ardhi ikalaaniwa kwa ajili ya Adamu na Hawa (Mwa 3:17-19).
3. Bwana akamlaani Kaini kwa kumuua Abili (Mwa 4:11-16).
4. Bwana akamlaani Kanaani na wazao wake (Mwa 9:25-27).
5. Israeli atabarikiwa kama atakuwa mtiifu kwa Mungu, na kulaaniwa kama hatakuwa mtiifu, (Kumb 29:18-28).
6. Gehazi na wazao wake walilaaniwa kwa ukoma wa Naamani (2Wafalme 5:20-27).
7. Bwana alilaani taifa la kale la Israeli kwa kutokulipa zaka na matoleo (Mal 3:8-10).
8. Yesu aliulaani mti wa mtini nao ukafa (Mk 11:12-14, 20-21).
9. Yesu akailaani miji ya Korazini, Bethsaida na Kapernaumu (Lk 10:10-15).
Kinyume cha Laana ni Baraka. Unapotii amri za Mungu, umejiwekea mazingira mazuri ya kupokea Baraka.
B. LAANA ZINAZONENWA NA MWANADAMU
Hizi nazo zimegawanyika katika makundi mawili.
Kundi la kwanza ni la watu wa Mungu/wenye haki
Kwa mfano, utakumbuka Hamu alipoona uchi wa baba yake. Nuhu alikuwa mtu wa Mungu. Nuhu aliulaani uzao wake. Hivyo watu wa Mungu wamepewa mamlaka hiyo, na hadi sasa. Ndiyo maana Bwana Yesu alisema, mtakalolifunga duniani, limefungwa mbinguni, na akatusihi pia tuwe watu wa kubariki kuliko kulaani. (Mathayo 16:19).
Unapokosewa na mwenye dhambi epuka kutoa neno la madhara kwake, kwa sababu hakika jambo hilo litampata na kumuangamiza kabisa. Ndicho alichokifanya Elisha mtu wa Mungu kwa wale vijana waliomdhihaki kuhusu kipara chake (2Wafalme 2:23-24). Aliwalaani; ndipo ghafla, wanyama dubu wa kike wawili walitokeza kutoka msituni na kurarua vijana 42 miongoni mwao.
Kundi la pili ni laana zitokazo kwa watu
Watu wenye nia mbaya, hususan wachawi, nao pia huweza kusema jambo likatokea, Utakumbuka kisa cha Balaamu mchawi, alipoajiriwa na Mfalme Balaki kwenda kuwalaani Israeli wa Mungu, lakini alishindwa akajikuta anawabariki badala ya kuwalaani. Akasema hakuna uchawi (Hesabu 23:23).
Ikiwa wewe umeokoka, huna haja ya kuogopa laana za kundi hili, kwa sababu haziwezi kukupata, kwa sababu unalindwa na nguvu za Mungu. Hizi huwa zinawapata watu ambao wapo nje ya mfumo wa Kristo Yesu.