Ukweli ni kuwa Dinho amepungua sana kiwango. Hata kwenye Champs League alikuwa akijipiga chenga mwenyewe na kufurahia hilo lisilo na tija. Dinho allikuwa na muda wake, akatumikia. Maisha yanaendelea. Other younger players are poised to take over ther mantle.
Ila siko sure kuhusu kumchukua Grafite na kumuacha Pato (kama ilikuwa lazima mmoja wao tu ndiye abaki).
Si issue sana Dinho kuachwa, kumbuka Romario aliachwa 2002.
Kocha ndiye mwenye uamuzi wa kumuacha au kumchukua, si hizo the so-called 'jumuia za kimataifa' (not Brazilian!).
Kuhusu mafanikio ya Dunga kama mchezaji, nikuuliza Chang Chomba je ni wachezaji wangapi wameshinda kombe la dunia? Dunga aliweza huku akiwa ni nahodha wa timu.
Je ni makocha wangapi wamefanikiwa kama Dunga wakiwa wachezaji? Ni wachache sana. Na Dunga ni mmoja wao.
Watu kadhaa wameumia kwa kuachwa wachezaji wao vipenzi. Ni uamuzi wa makocha. Ila tukubali Dinho wa sasa si 'yule'.
Kumbuka Domenech naye kamuacha Nasri...
Kwanza napenda kukupa pole kwa kutokuwa mfuatiliaji wa soka.
nimekunukuu hapo juu ukidai kuwa Dinho ktk Chmps league alikuwa anajipiga chenga mwenyewe na kufurahi.
Sasa naomba unithibitishie ni mechi gani ambaye Saint Gaucho amejipiga chenga.
Suala la pili ni kuhusu striker aliyepaswa kwenda south.
Julio Baptista mshambuliaji wa AS Roma amecheza mechi ngapi msimu huu?
Na je amefunga magoli mangapi msimu huu?
Na je katengeneza mangapi?
Kisha ukipata jibu geuka kwa Pato.
Kisha fuatilia DATA zake za msimu huu.
Pia kuna kauli umeitoa ukidai kuwa Kocha ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.
Teh teh kwani kocha huwa hakosei? basi Wenger atafia Arsenal
Na kuhusu mafanikio ya Dwaf Dunga ni kuwa ameshawahi kuwa nahodha wa timu 1994 na kunyanyua ndoo ya dunia...but naomba unisaidie je ana mafanikio mengine alipokuwa mchezaji?
Sasa turudi kwa Saint Gaucho.
Dinho amebeba kombe ka dunia, kabeba champs league kitu ambacho Dwaf Dunga hajathubutu.
Kabeba La Liga kitu ambacho huyo sakala wenu hajawahi kufanya.
Keshawahi kuwa mwanasoka wa dunia mara mbili kitu ambacho huyo Dwaf wenu hajawahi kufikiria.
kachaguliwa kuwa mwanasoka bora wa miaka 10 ilopita.
Sasa nataka kukusaidia...
Usikurupuke kumponda mtu eti kisa kuna watu wanamponda.
Unatia aibu