Wakipekee
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 6,194
- 10,711
Salute wanaJF,
Hakika maisha yako kasi sana. Msimu uliopita John Boko alikua mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania. Ndio alikua na goli 16. Kila kona mashabiki wa Simba walimuimba kwa nyimbo nzuri na za kupendeza. Kwa lugha rahisi alikua kipenzi cha wanamsimbazi.
Mwaka 2019 kuna kijana alikuja bongo na timu toka umakondeni huko msumbiji. Alikua na timu yake isiyojulikana sana katika ukanda wetu huu wa Cecafa.. Ndio namanisha UD songo. Likapigwa mbugi bomba sana pale kwa mkapa. Ohoo kuna kijana mmoja alikua na jezi namba 17 mgongoni. Alikua hakabiki aliwapiga sana chenga viungo na mabeki wa simba. Hakuna aliyeamini kama simba iliyotoka kucheza robo fainali ya mabingwa Africa ingeteswa na timu isiyojulikana tena kwa "mchina"!... Uwanja ambao ndo ulikua machinjioni kwa wale waliojileta bongo kupambana na simba. Ilikua kama miujiza dakika 90 zikaisha kwa goli moja moja!
Kumbuka mechi ya kwanza iliisha kwa sare ya bila kufungana. Kwahiyo simba akawa ametoka kwa kigezo cha kufungwa nyumbani. Watu walishangaa. Lakini hiyo haikua stori kubwa badala yake kuna balaa jipya likawa limeibuka. Habari kubwa kwenye anga la michezo Tanzania. Ni kuhusu yule jamaa mwenye jezi namba 17. Ndio jina lake lilisomeka " L MIQUISSONE ". Unataka nimusunilie kilichofatia?? Hapana hakuna asiyejua kua msimu uliofatia alisajiliwa simba. Naam akaanza maisha mapya TZ.
Mwanzoni sikumkubali sana nilijua ni mchezaji wa kawaida tu. Ohoo kadiri siku zilivokua zinasonga kiwango chake kilizidi kupanda. Kila kona akawa ni stori ya mji. Mashariki walimkubali, magharibi wakamhusudu,kusini wakamuimba na kaskazini waliamini huyu ni messi mweusi. Hata yule mtangazaji nguli hapa bongo baraka mpenja alipagawa na kujiuliza hilo swali.
Nanukuu maneno yake ya July 19 2020 simba walipocheza na alliance school ya mwanza. " Nani anaona kama mimi? Kondeboy anaonesha ugenstar! Huu anoufanya ni ukatili.. Huyu ni messi au vipi??". Aloo hii ndo siku niliamini huyu chalii miquissone hakua mchezaji wa kawaida hata kidogo. Maana goli alilofunga lilinikumbusha goli la mo salah alilowapiga Chelsea. Kwa wale wadau wa PES wanaita zungusha. Hatari sana.
Msimu wa mwaka Jana ulikua msimu bora sana kwa miquissone. Hakuna mchezaji hapa bongo alisitahili kukaa juu yake kiubora. Sizungumzii idadi ya mabao lakini umuhimu wa mchezaji kwa ujumla. Kama huamini basi waulize Plateau FC ya naijeria jamaa aliwakusanja kisha akawageuza kadiri alivotaka. Hata timu bora zaidi barani Africa, ally ahly walikumbana na balaa zito hadi wakaamua kumsajili.
Washindi siku zote hupongezwa ikafika siku ya kuwapongeza wachezaji waliofanya vizuri msimu uliopita. Katika hali isiyotarajiwa mchezaji aliyekua bora hakupewa tuzo balada yake akapewa MTU mwingine. Sijajua TFF walitumia kigezo gani kumpa Boko uchezaji bora balada ya Jose miquissone!. Au kwa kua Boko ni mTz? Au kisa alifunga magoli mengi? Hapana kama inshu ni kufunga walimpa tuzo ya ufungaji bora kwanini tena apewe tuzo ya uchezaji bora? Hadi leo sijajua kigezo kilichotumika. Ni miezi michache imepita toka Boko akabidhiwe tuzo hiyo ya mchongo. Sasa imegeuka laana.
Laana inayomtesa sana. Hakuna tena mwanasimba anaetaka kumuona mchezaji bora akicheza!. Wote wamemchoka Boko sahivi anapiga tu maboko. Anakosa magoli ya wazi..! Je kiwango kimeshuka!? Labda lakini mbona imekua ghafla hivo? Mi nazani ni muda wa yeye kutubu na kuomba radhi kwa kukubali kupokea ile tuzo ambayo haikua halali yake.
Anyway niishie hapo. Nimekumbuka tu vituko vya TFF huenda wao ndo wamemloga Boko nani anajua?
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app