Laana ya mzazi(Radhi): Ni kweli kuna kitu hicho?

Laana ya mzazi(Radhi): Ni kweli kuna kitu hicho?

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Wakuu habari zenu!

Nimeona nilete hii mada ili tuweze kuijadili na kupata ukweli na uzoefu kutoka kwa watu mbali mbali. Hivi, maneno ya wosia anayoacha marehemu kwa watu waliobaki huwa yana uhalisia katika utekelezaji?

Na kwa nini? Kwa mfano, marehemu aliacha laana ya kuwa fukara kwa mtoto wake na kweli ikatokea.

Je, kuna uhusiano gani katika uhalisia wa jambo na maneno ya mtu aliyekufa. Ni kweli wengine huwa na mtazamo wa mbali wa kuweza kufocus jambo na kuliona kabla ya wengine, lakini wengine ni maneno tu! Inakuwaje hapa!

Karibuni
 
  • Thanks
Reactions: AMB
Mi naona inategemea hiyo laana imetolewa kwa misingi ipi..maana unaweza ukakuta mzazi husika amemuonea mwanae katika kutoa laana hiyo..so nadhani haitoweza kumpata..ila pia ukirejea kwenye vitabu vitakatifu mfano biblia inasema "laana isiyo na sababu haimpati mtu"nimesahau kitabu gani..ila huo mstari upo
 
Wakuu habari zenu!

Nimeona nilete hii mada ili tuweze kuijadili na kupata ukweli na uzoefu kutoka kwa watu mbali mbali. Hivi, maneno ya wosia anayoacha marehemu kwa watu waliobaki huwa yana uhalisia katika utekelezaji?
Na kwa nini? Kwa mfano, marehemu aliacha laana ya kuwa fukara kwa mtoto wake na kweli ikatokea. Je, kuna uhusiano gani katika uhalisia wa jambo na maneno ya mtu aliyekufa. Ni kweli wengine huwa na mtazamo wa mbali wa kuweza kufocus jambo na kuliona kabla ya wengine, lakini wengine ni maneno tu! Inakuwaje hapa!

Karibuni

laana ni vile mtu anayedai kulaaniwa anavyoiperceive..ukichukulia kwamba ni laana lazima ikuchanganye kichwa!!
 
Maneno yanaumba ndugu, kwa wale tunaoamini katika ukristo ukisoma kitabu cha mwanzo wakati mungu anaumba dunia na vyoote viijazavyo utaona uumbaji unaanza kwa maandiko ya "Mungu akasema" iwe nuru na ikawa nuru.. "Mungu akasema" na liwe anga katikati ya maji kutenganisha ardhi na mbingu ikawa hivyo... etc etc...

Hivyo basi kiimani maneno yanaumba. na kwa vile hata sisi wanadamu tumepewa uwezo wa kimungu kwa yeyote atakaekua na imani hata kama ni ndogo kama chembe ya haradari basi atakachokisema kitakuwa katika ulimwengu wa kiroho na kitadhihirika katika ulimwengu wa mwili with time.

kwa mtazamo wangu issue hapa ni je hizi laana zinaweza vunjwa na how do we break them? mimi nishawahi ivunja laana... ntaawaambia....
 
Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

  • Kumbe kutokuwaheshimu tu, siku zako za kuishi zinapungua.
  • Ukiwaheshimu siku zako za kuishi zitakuwa nyingi na zenye mafanikio.
 
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
Mshua's, ebu tuambie kama yupo mtu yeyote unayemjua, aliyekosa utii kwa wazazi wake na akafanikiwa kufikia maisha ya uzee.
 
Last edited by a moderator:
I think laana/curse is a Bad Karma (what goes around, comes around) since energy can not be created nor destroyed. If you radiate negative energy I believe it will be back to you or even your generations and vice versa is also true. This is Physics.
 
laana ni uthubutu usiokubalika katika jamii.
 
Mind over Matter...

Akili ya mtu ni very powerful hata wewe sasa hivi ukiamini kwamba una malaria unaweza ukaugua.., au ukianza kujiona kwamba unakufa na ukakata tamaa basi utakufa...

Hivyo basi kama wewe kweli umemtendea mzazi wako kosa.., kila kitu unachofanya kisipofanikiwa utajua kwamba hakifanikiwi sababu ya zile laana.., kwahio mwisho wa siku utakusa confidence hata yale ambayo huwa unaweza kuyafanya utayafanya kwa kuogopa ogopa hence mwisho wa siku hautafanikiwa...

Kama ujuavyo kujiamini katika kufanya kitu ni nusu ya kufanikiwa kufanya kile kitu, na bila kujiamini huwezi kufanya kitu.., Kwahio laana zitafanya kazi kama unaamini katika laana. Ukizingatia waliosema Dua la Kuku halimpati Mwewe hawakukosea.., ila kama yule mwewe akianza kuamini Dua la kuku kwamba linampata huenda hata zile hesabu zake za kuiba kifaranga atazikosea hence kuokota jiwe badala ya kifaranga
 
Wakuu habari zenu!

Nimeona nilete hii mada ili tuweze kuijadili na kupata ukweli na uzoefu kutoka kwa watu mbali mbali. Hivi, maneno ya wosia anayoacha marehemu kwa watu waliobaki huwa yana uhalisia katika utekelezaji?
Na kwa nini? Kwa mfano, marehemu aliacha laana ya kuwa fukara kwa mtoto wake na kweli ikatokea. Je, kuna uhusiano gani katika uhalisia wa jambo na maneno ya mtu aliyekufa. Ni kweli wengine huwa na mtazamo wa mbali wa kuweza kufocus jambo na kuliona kabla ya wengine, lakini wengine ni maneno tu! Inakuwaje hapa!

Karibuni

Ndio tupate faida hapa..
 
Ni Kweli

Kiukweki kabisa laana ipo na laana haitoki kwa mzazi tu inatoka kwa Mungu. Kwa mfano kijana hukuwatendea vyema wazazi wako na mnatofautiana kwa namna moja ama nyengine na mzazi hariziki kutokana na tabia yko au hali hiyo.

Na mzazi anakupenda mwanawe hali ya kuwa anaumia moyoni. Na kukupa lana hawezi kwa upendo wake. Bs automatic Mungu anakulaani na inakupata laana ile. Kwa upande wa pili unamkuta mzazi anampa laana mwanawe kakin haimpati laana ile kwakua si kila anachosema mzazi nimekulaani ndo ukalaaniwa. Hutegemea na matendo yko je yanamridh mungu ama laa. Na maana mzazi hutamka tu nimekupa laana lakin Mungu ndie anaekupa laaana.
 
Kiukweki kabisa laana ipo na laana haitoki kwa mzazi tu inatoka kwa mungu. Kwa mfano kijana hukuwatendea vyema wazazi wako na mnatofautiana kwa namna moja ama nyengine na mzazi hariziki kutokana na tabia yko au hali hiyo. Na mzazi anakupenda mwanawe hali ya kuwa anaumia moyoni. Na kukupa lana hawezi kwa upendo wake. Bs automatic mungu anakulaanu na inakupata laana ile. Kwa upande wa pili unamkuta mzazi anampa laana mwanawe kakin haimpati laana ile kwakua si kila anachosema mzazi nimekulaani ndo ukalaaniwa. Hutegemea na matendo yko je yanamridh mungu ama laa. Na maana mzazi hutamka tu nimekupa laana lakin mungu ndie anaekupa laaana.
Usiotee maneno Mungu akupe laana ya kazi gani?
 
Hakuna laana.
Hizo ni tishio ili kuweka jamii sambamba. Sio kitu kibaya, lakini NI TISHA TOTO TUU. hakuna laana.
Imani za laana ziko katika makundi ya imani za dini, ushirikina, na miujiza ambayo vyote ni "soundi tuu".

Wengi tunaishi na kulea familia bila fikra kama hizo na tumefanikiwa - kimaisha, kimaendeleo, na tuna mtazamo wa kisasa kuhusu maisha. Watoto wetu wamejifunza ku question everything and anybody. To find and respect that what is proved to be true.
Lakini pia tuna jali sana tamaduni zetu ambazo zina tukumbusha sisi ni nani kama Waafrika.
 
I think laana/curse is a Bad Karma (what goes around, comes around) since energy can not be created nor destroyed. If you radiate negative energy I believe it will be back for you or even your generations and vice versa is also true. This is Physics.

Umewezaje kusoma na kuchanganua alafu ushindwe kuandika Kiswahili? NADHANI HUKUTAKA BAADHI YETU TUKUELEWE, ASANTE!
 
Umewezaje kusoma na kuchanganua alafu ushindwe kuandika Kiswahili? NADHANI HUKUTAKA BAADHI YETU TUKUELEWE, ASANTE!

Maana fupi ya niliyo yaandika ni hii :
Ukifanya mazuri yatarudi na ukifanya mabaya ni vivo hivyo. Si lazima yakurudie wewe, yaweza kuvirudia hata vizazi vyako.
 
Kama hujamkosea mzazi hakuna laana.

Na laana hairithiwi yaani ya baba yako haiwezi kua kwako.
"Lakini ninyi mwasema, Kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. -------- "Ezekieli: 18: 20-22
 
Embu jaribu kuzinguana na wazazi..halafu uone impact yake....itakuthibitishia swali lako....
 
Ukimkosea mzazi wako na usimtake radhi akakunenea maneno mabaya huchomoki.
 
Back
Top Bottom