Laana ya Umri inavyoitafuna China

Laana ya Umri inavyoitafuna China

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwa sasa nchini China watu wenye umri wa miaka 35 wanakutana na laana ya kuwa na umri huo.

Kwa sasa Wachina wengi wenye umri wa miaka 35 wanakumbana na tishio la kukosa ajira ama mikataba yao ya ajira kutokuongezwa kutokana na kuonekana kuwa wana umri mkubwa.

Uchina ambayo kwa sasa ina utamaduni wa kufanyakazi kuanzia saa tatu Asubuhi mapaka saa tatu usiku, unaojulikana kwa jina la "996", imekumbwa na shinikizo la kufanya kazi kwa masaa mengi Ili kukidhi uhitaji wa bidhaa na huduma kwenye soko la China na nje ya China.
 
Kwa Sasa nchini China watu wenye umri Wa miaka 35 wanakutana na laana ya kuwa na umri huo.

Kwa sasa wachina wengi wenye umri wa miaka 35 wanakumbana na tishio la kukosa ajira ama mikataba yao ya ajira kutokuongezwa kutokana na kuonekana kuwa wana umri mkubwa.

Uchina ambayo kwa sasa ina utamaduni wa kufanyakazi kuanzia saa tatu Asubuhi mapaka saa tatu usiku, unaojulikana kwa jina la "996", imekumbwa na shinikizo la kufanya kazi Kwa masaa mengi Ili kukidhi uhitaji wa bidhaa na huduma kwenye soko la China na nje ya China.
Walegeze sheria za uzazi ili kuijaza tena nchi.
 
Kuna kitu sijakielewa. Kama nguvu kazi ni chache mpk kufikia kuongeza muda wa kazi inakuwaje mtu wa miaka 35 akaonekana hafai kuwa kazini wakati kuna uhitaji wa nguvu kazi?
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Sababu ni nini ?
Sababu kubwa zipo tatu.

1 . Baada ya Japan nchi inayofuatia Kwa kufanya kazi kwa muda mrefu ni China. China Kwa Sasa kufanya kazi Kwa masaa mengi ni kitu kinachohitajika kwa mtu kubaki kwenye ajira.

China ni nchi inayosimamiwa na chama cha kikomunisti Lakini sehemu kubwa sana ya uchumi wake unaendeshwa na makampuni binafsi ya kibepari.

Hayo makampuni Yana ushindani mkubwa sana na Ili yakidhi nguvu ya kushindana ni lazima wafanyakazi wake wafanye kazi kwa bidii na Kwa muda mrefu sana.

Tatizo soko la ajira ni dogo kuliko idadi ya vijana wenye ujuzi na stadi ya kazi hizo na kutokana na udogo Wa soko la ajira, watu wanaotaka kufanya kazi kwa ujira wowote ule wanazidi kuongezeka.

Maana yake watu wenye umri wa miaka 35 na kuendelea wameonekana kuwa baada ya kufanya kazi kwa muda fulani huonekana kuchoka haraka na kushindwa kuhimili shinikizo la kufanyakazi nyingi na kwa muda mrefu.

2. Mahitaji ya bidhaa sokoni ni makubwa.

3. Viwango vya elimu viko Juu sana na vijana wengi Wana stadi za kazi wakati soko la ajirano dogo.
 
Kwa sasa nchini China watu wenye umri wa miaka 35 wanakutana na laana ya kuwa na umri huo.

Kwa sasa Wachina wengi wenye umri wa miaka 35 wanakumbana na tishio la kukosa ajira ama mikataba yao ya ajira kutokuongezwa kutokana na kuonekana kuwa wana umri mkubwa.

Uchina ambayo kwa sasa ina utamaduni wa kufanyakazi kuanzia saa tatu Asubuhi mapaka saa tatu usiku, unaojulikana kwa jina la "996", imekumbwa na shinikizo la kufanya kazi kwa masaa mengi Ili kukidhi uhitaji wa bidhaa na huduma kwenye soko la China na nje ya China.
miaka 35? kwa nini akose ajira au ulimaanisha miaka 55?
 
Najua watu wengi mnasema hamjaelewa Kwa kuwa mnawaza mambo ya kustaafu. China kazi nyingi zipo kwenye mfumo wa Mkataba.

Lakini hoja siyo umri bali wenye kazi zao wanataka mtu anayeweza kufanya kazi kwa muda mrefu, kazi kubwa na kwa ustadi mkubwa.

Kwa ivo imeonekana shinikizo la kufanya kazi kwa masaa 12 mfululizo, watu wenye miaka 35 na kuendelea hawawezi.
 
Back
Top Bottom