Huyu mchezaji alipokuwa Arsenal alijishebedua sana akikataa kusaini mkataba mpya ili aongezewe mpunga , Mzee Wenger hatimaye akasalimu amri na kuamua kumsalimisha kwa Bwana matamaa aitwaye Morinho , ambaye kwa vile hakuwa na uchungu na hela za watu akaamua kumlipa Sanchez mihela ya kufa mtu .
Kwa bahati mbaya kinyongo na laana ya Wenger vikamfuata Alexis kila alipogusa mpira , akaanza kustukiwa na kupigwa benchi , na baada ya Morinho kuondoka hali imekuwa mbaya zaidi , na sasa anatafuta namba kwenye Ndondo cup .
Wenger ana nini lakini , mbona kila mchezaji anayeondoka kwa nyodo anaishia kubaya ?