Labda nifukuze wafanyakazi wangu nikuajiri wewe

Labda nifukuze wafanyakazi wangu nikuajiri wewe

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Nikiwa kati kati ya interview nzito, Mara ghafla simu ya HR ikaita, akaipokea huku akisikiliza kwa makini anachokiongea mpiga simu, akamjibu mpiga simu kuwa "labda niwafukuze wafanyakazi wangu nikuajiri wewe" hiyo kauli mpaka leo haijafutika kwenye akili yangu tangu niisikie akijibiwa mpiga simu,

Lengo la uzi huu ni kujadili kwa kina sisi wasaka ajira tunakwama wapi?

Aliyesema asiyekujua hakuthamini, na waarabu wa pemba hujuana kwa viremba,
alikuwa sahihi kwa asilimia mia moja, je niliwezaje kufika hatua ya kuitwa kwenye interview ambayo tangazo la kazi halikuwepo, jibu ni kwamba nilipereka maombi hivyo hivyo sehemu husika kwa msaada wa kiongozi wa dini wa kanisa letu ambaye anafahamiana na HR, japokuwa nasubiri kuitwa nikaanze kufanya kazi endapo neema za mwenyezi Mungu zitakuwa upande wangu,But Hii hatua kwangu ya kuitwa na kufanyiwa usaili kwangu ni hatua kubwa sana maana tangu nianze kuaply kazi sehemu mbali mbali sikuwahi hata kupigiwa simu,

Hivyo basi huenda namna nnavyofikiri kwa sasa ninakaribia kwenye jibu sahihi, nilichojifunza ni kwamba watu wanatafuta connection ila hawazipati kumbe connection zipo vichwani mwetu, ma HR ndio hawa hawa tunaosali nao makanisani na misikitini, ndio hawa hawa wanaokuja kununua vitu dukani kwa Mangi, ndio hawa hawa wanaohudhuria mikutano ya CCM ndio hawa hawa tunaosali nao kwenye jumuiya ndogo ndogo mitaani n.k
MACHACHE NILIYOJIFUNZA​
  • Usiombe kazi kwa kupiga simu!
  • Hakikisha una connection!
  • ukiitwa kwenye interview chagua kuongea ukweli sababu ukiongea uongo kuutetea uongo ni kazi kubwa sana,
  • usimkabidhi barua au CV yoako kibarua wa hapo ofisini hakikisha unampa boss mwenyewe au mtu anayehusika.
Je wasaka ajira tunakwama wapi? Ulipataje connection (ulitumia mbinu gani)? Ni jibu gani la ajabu uliwahi kupewa au kulisikia wakati ukiomba kazi?
 
Kwasasa, mimi jambo la kuomba kazi Nimelifuta kabisa kichwani mwangu.. Kila mmoja ashinde mechi zake

.. .. ..
Hizi System zinavichekesho na huanza pale ambapo HR nayeye huhangaika na barua kutafuta kazi, akishapata hufanya kama yeye ndio Mwenye Mali, kumbe nayeye amesitiriwa tuu
 
kuna bwege aliwahi nichinjia baharini akiwa HR wilaya flani na tunatoka mtaa mmoja huwa nna kinyongo nae mpaka kesho pumbavu yule na kujifanya mtu wa dini.
 
Back
Top Bottom