Kusema kweli ni ngumu sana mtu kukufundisha kutongoza. Mi mwenyewe ata sijui kutongoza ila nikikutana na mwanamke nikamuelewa, maneno hua yanakuja hapohapo kulingana na mazingira tuliyopo.
Kitu kimoja kikubwa sana cha msingi pindi unapokutana na demu mpya, mkali, na unataka kuanzisha nae mazungumzo, jitahidi sana USIWE SERIOUS! Jitahidi kuwa kawaida na kuongea nae kawaida kama unavyoongea na wanawake wengine ambao huwataki. Wanawake hua wanaogopa sana mtu ambae yuko serious hasa mwanzoni.
Mfano: Umemuona mdada mzuri kasimama juani na unataka kuongea nae. Badala ya kumfuata na kuanza kumuambia "dada habari yako? samahani naomba kuongea na wewe" wewe mfate kama unamjua vile, mwambie "sasa wewe nawe... ndio umeona usimame hapo juani? si usogee hapa kwenye kivuli?" Wakati unaongea hayo wewe usisimame, unatembea zako kuelekea kwn kivuli. Mara nyingi (sio zote) mdada atakufata. Na hata asipokufata poa tuu acha aendelee kuchomwa na jua we unaenda zako kutulia kwenye kivuli.[emoji6]