Labda sijui kutongoza sababu ya aibu nilizo nazo

Pombe unakunywa?

Embu jaribu siku utashngaa hata mistari inakotokea😀😀😀
Mjumbe hebu mwelezee kidogo booster iliopo katika chupa ya Chui lite😂!!! Nina hakika akipewa kadi ya chama lazma atakuwa balozi
 
"Ila hips napenda sana.pia mwanamke mstaarabu mpole, mcheshi.asiwe kama hawa ambao nakutana nao kila mara wa kutaka ku spend tu. Nimeshachoka hayo Maisha".

Kwa hitimisho hilo Mkuu bado hujaeleweka unataka msaada gani Mkuu? kama una pesa una feli wapi Mkuu, kama huna tafuta pesa confidence itakuja automatically.
 
Kusema kweli ni ngumu sana mtu kukufundisha kutongoza. Mi mwenyewe ata sijui kutongoza ila nikikutana na mwanamke nikamuelewa, maneno hua yanakuja hapohapo kulingana na mazingira tuliyopo.

Kitu kimoja kikubwa sana cha msingi pindi unapokutana na demu mpya, mkali, na unataka kuanzisha nae mazungumzo, jitahidi sana USIWE SERIOUS! Jitahidi kuwa kawaida na kuongea nae kawaida kama unavyoongea na wanawake wengine ambao huwataki. Wanawake hua wanaogopa sana mtu ambae yuko serious hasa mwanzoni.

Mfano: Umemuona mdada mzuri kasimama juani na unataka kuongea nae. Badala ya kumfuata na kuanza kumuambia "dada habari yako? samahani naomba kuongea na wewe" wewe mfate kama unamjua vile, mwambie "sasa wewe nawe... ndio umeona usimame hapo juani? si usogee hapa kwenye kivuli?" Wakati unaongea hayo wewe usisimame, unatembea zako kuelekea kwn kivuli. Mara nyingi (sio zote) mdada atakufata. Na hata asipokufata poa tuu acha aendelee kuchomwa na jua we unaenda zako kutulia kwenye kivuli.😉
 
Aisee!!
 
Daah unanikumbusha mbali sana kijana miaka ya 98 nilikuwa mpole kama wewe na hata washikaji class wanakutumia Dada mkali eti unamwitaji halafu Mimi enzi hizo mpole kama wewe kuwaangalia mademu kwangu moyo unadunda sana ila Mimi nilikuwa mtu wa stori nyingi sana ilikwenda mpaka namaliza chuo sijawahi kuduu na demu yeyote ila sasa mimi mwenzio nilikuwa na Dada mmoja mkali sana huku mtaani alitokea kunizimikia na nikapewa stori na washikaji ndiyo huyo sasa ni mke wangu na kwa kweli nimepitia mengi sana kukaa naye kwa miaka 10 pasipo kuduu nikisoma na kwa sasa tumeshafunga ndoa na amenizalia watoto wawili wa kiume na wa kike. Kiukweli mwombe sana Mungu akuepushie mbali na hofu akupe confidence ya kuweza kuongea nao anza kidogo dogo msalimie mchekeshe mtanie mwishoni utaona ni hali ya kawaida itapita tu ni umri fulani ikipita utajiona wa kawaida na maduu utawazoe tu.
Fanya hii homework ndugu yangu!!
 
Bravo
 
Mimi napenda wanawake wenye hips na makalio ya wastan. Ila hips napenda sana.pia mwanamke mstaarabu mpole, mcheshi.asiwe kama hawa ambao nakutana nao kila mara wa kutaka ku spend tu. Nimeshachoka hayo maisha


Hawa wanaotaka kuspend tu hua unawatongozaje??? Wanakutongoza wenyewe??
 
jikite kwenye ujezi wa taifa ndugu mfano huu muda ungeutumia kwenye kujifunza ufugaji wa kuku na magonjwa yake huoni kama ungekua umeutendea haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…