GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Sina uhakika kama Kikwete alikuwa na ndoto ya kuja kuwa Rais wa Tanzania. Mwinyi alipomteua kuwa Mbunge na Waziri, alimfuata na kumwomba amwondolee uwaziri amwachie ubunge. Badala ya Mwinyi kulipokea ombi lake, alimtia moyo kwamba yeye ni kijana mwenye akili hivyo ataimudu hiyo nafasi. Kilichofuatia baada ya miaka kadhaa ni Historia.
Samia alipoitwa Ikulu ya Zanzibar kujulishwa kuwa kateuliwa kuwa Waziri, alishtuka sana. Hakuwa na uhakika wa kuyamudu hayo majukumu.
Kwa nafasi aliyo nayo sasa huhitaji kujiuliza kama aliyaweza majukumu ya uwaziri au la!
Ali Hassan Mwinyi alihudhuria mkutano mkuu wa CCM mwaka 1984 kama wajumbe wengine, lakini alirejea Zanzibar akiwa na "jina" jipya, Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar.
Vipi akina Lusinde na Msukuma? Japo wana Elimu ndogo, lakini wameweza kuwashawishi wananchi wao kuwachagua kuwa wawakilishi wao bungeni.
Unajifunza nini kwa hiyo mifano? Unaowaona wapo juu wanaweza wakawa hawajakuzidi akili, na huenda, hata majukumu wanayoyafanya wewe ungeyamudu vizuri zaidi kuwazidi. Kilichowatofautisha wao na wewe ni kitu kimoja tu, ujasiri.
Walithubutu, japo inawezekana ni kwa kujaribu, na wakaishia kuwa hivyo walivyo sasa.
Na wewe unaweza kuthubutu kufanya lile ulitamanilo na likaishia kuwa kweli.
Ongeza ujasiri kidogo tu uone kitakachotokea.