Lack of Official Colours of the National Emblem on President's Podium

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,441
Reaction score
11,669
Kutokana umuhimu wa hotuba za Rais, pale anapohutubia, katika sehemu maalum, yaani podium, ni vyema kabisa iwe na nembo ya Taifa yenye kuakisi uhalisia wa asili wa rangi zake. Uwepo wa rangi zisizo hakisi uhalisia huondoa kabisa kusudio halisi za uwepo wa rangi husiko.

Katiba ya 1977 inazitaja alama za Taifa kuwa ni: Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, na Nembo ya Taifa.

Maelezo kamili ya Nembo ya Taifa pamoja na alama na rangi zake yanapatikana kwenye Sheria ya Alama za Taifa, Sura 10 na Kanuni za Alama za Taifa. Hizi ndizo zinatoa mamlaka ya kisheria kwa nembo hii ya Taifa. Inatumika kwenye nyaraka rasmi za serikali, pasipoti, sarafu, na majengo ya umma kama ishara ya mamlaka.

Maana ya alama
a. Ngao ni "Ulinzi wa Taifa"
b. Mwenge ni "Uhuru na mwanga wa elimu"
c. Mkuki na Jembe ni "Ulinzi na kazi"
d. Pembe za Ndovu ni "Maliasili na wanyamapori"
e. Mlima Kilimanjaro ni "Fahari ya Taifa"
f. Mwanaume na Mwanamke ni "Usawa wa kijinsia"
g. Pamba na Karafuu ni "Uchumi wa Bara na Zanzibar"
h. Uhuru na Umoja ni "Kauli mbiu ya Taifa"

Ni kosa la jinai kuitumia nembo vibaya au bila kibali - adhabu yake ni faini au kifungo. Inatumika tu na taasisi za serikali, balozi, na nyaraka rasmi.

Nembo ya Taifa ni muhuri wenye saini ya nchi, na ikionekana kwenye hati, maana yake ni hati rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Attachments

  • IMG_20260510_100443.jpg
    IMG_20260510_100443.jpg
    61.5 KB · Views: 15
  • IMG_20260510_100900.jpg
    IMG_20260510_100900.jpg
    68.8 KB · Views: 14
  • IMG_20260510_100628.jpg
    IMG_20260510_100628.jpg
    54 KB · Views: 16
Kutokana umuhimu wa hotuba za Rais, pale anapohutubia, katika sehemu maalum, yaani podium, ni vyema kabisa iwe na nembo ya Taifa yenye kuakisi uhalisia wa asili wa rangi zake. Uwepo wa rangi zisizo hakisi uhalisia huondoa kabisa kusudio halisi za uwepo wa rangi husiko.

Katiba ya 1977 inazitaja alama za Taifa kuwa ni: Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, na Nembo ya Taifa.

Maelezo kamili ya Nembo ya Taifa pamoja na alama na rangi zake yanapatikana kwenye Sheria ya Alama za Taifa, Sura 10 na Kanuni za Alama za Taifa. Hizi ndizo zinatoa mamlaka ya kisheria kwa nembo hii ya Taifa. Inatumika kwenye nyaraka rasmi za serikali, pasipoti, sarafu, na majengo ya umma kama ishara ya mamlaka.

Maana ya alama
a. Ngao ni "Ulinzi wa Taifa"
b. Mwenge ni "Uhuru na mwanga wa elimu"
c. Mkuki na Jembe ni "Ulinzi na kazi"
d. Pembe za Ndovu ni "Maliasili na wanyamapori"
e. Mlima Kilimanjaro ni "Fahari ya Taifa"
f. Mwanaume na Mwanamke ni "Usawa wa kijinsia"
g. Pamba na Karafuu ni "Uchumi wa Bara na Zanzibar"
h. Uhuru na Umoja ni "Kauli mbiu ya Taifa"

Ni kosa la jinai kuitumia nembo vibaya au bila kibali - adhabu yake ni faini au kifungo. Inatumika tu na taasisi za serikali, balozi, na nyaraka rasmi.

Nembo ya Taifa ni muhuri wenye saini ya nchi, na ikionekana kwenye hati, maana yake ni hati rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
haina umuhimu wala ulazima wowote ikiwa pembeni kuna bendera ya Taifa
hata hivyo,
ikiwa unazifahamu tayari rangi za bendera na ya ngao ya taifa, unaweza kuziweka pale saikolojikali na mambo yakaisha tu bila kuziona phisikali.
 
Mkuu, kumbuka kuwa Katiba ya 1977 inazitaja alama za Taifa kuwa ni: Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, na Nembo ya Taifa.

Je! Katiba yetu imeipa Bendera ya taifa hadhi ya ukuu kuliko Nembo ya Taifa? Vipi kuhusu Sheria ya Alama za Taifa, Sura 10 na Kanuni za Alama za Taifa?

Mkuu, kabla hujakurupuka kujibu hoja iliyopo, jikite kwanza kujua mantiki na maudhui yaliyotolewa na mleta hoja.
 
sual

suala la kiongozi mpya wa nchi kuiga kila kitu kwa kwa kiongozi aliepita halipo gentleman,

Kila kiongozi mpya anaingia na aina yake ya utambulisho katika bendera ya raisi na mahali pa kusemea. Na hiyo sio kwa Tanzania tu bali Africa na duniani kote.

Angalia hiyo nembo wa rais wa Kenya wakati huo akiwa Uhuru kenyata, halafu check bendera ya raisi ruto na podiam yake ya sasa kama vinafanana na hiyo ya Uhuru.

Hakuna ufanano wa rangi wala mtindo wa hizo podiam, ni sawa na utofauti wa ile podiam ya hayati Nyerere , hayati Mwinyi, Dr.Kikwete, hayati Dr. magufuli na Dr.Samia.

Kila moja alikua ana utambulisho wake 🐒
 
Kutokana umuhimu wa hotuba za Rais, pale anapohutubia, katika sehemu maalum, yaani podium, ni vyema kabisa iwe na nembo ya Taifa yenye kuakisi uhalisia wa asili wa rangi zake. Uwepo wa rangi zisizo hakisi uhalisia huondoa kabisa kusudio halisi za uwepo wa rangi husiko.

Katiba ya 1977 inazitaja alama za Taifa kuwa ni: Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, na Nembo ya Taifa.

Maelezo kamili ya Nembo ya Taifa pamoja na alama na rangi zake yanapatikana kwenye Sheria ya Alama za Taifa, Sura 10 na Kanuni za Alama za Taifa. Hizi ndizo zinatoa mamlaka ya kisheria kwa nembo hii ya Taifa. Inatumika kwenye nyaraka rasmi za serikali, pasipoti, sarafu, na majengo ya umma kama ishara ya mamlaka.

Maana ya alama
a. Ngao ni "Ulinzi wa Taifa"
b. Mwenge ni "Uhuru na mwanga wa elimu"
c. Mkuki na Jembe ni "Ulinzi na kazi"
d. Pembe za Ndovu ni "Maliasili na wanyamapori"
e. Mlima Kilimanjaro ni "Fahari ya Taifa"
f. Mwanaume na Mwanamke ni "Usawa wa kijinsia"
g. Pamba na Karafuu ni "Uchumi wa Bara na Zanzibar"
h. Uhuru na Umoja ni "Kauli mbiu ya Taifa"

Ni kosa la jinai kuitumia nembo vibaya au bila kibali - adhabu yake ni faini au kifungo. Inatumika tu na taasisi za serikali, balozi, na nyaraka rasmi.

Nembo ya Taifa ni muhuri wenye saini ya nchi, na ikionekana kwenye hati, maana yake ni hati rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa nini mnahangaika na majitu ya hovyo?
 
Tatizo ni pale watawala wanapozoea kukiuka katiba na sheria pasipo hata kujali. Wao kazi yao ni kujificha katika kisingizio cha eti ni kudumisha mila na desturi ya Mtanzania.

Katiba na sheria zimewekwa ili zihifadhiwe na kulindwa. Ukiukwaji wake kwa makusudi ni ushenzi kama mwingine wowote ule. Mazoea ya watawala kupindisha hovyo matakwa ya katiba na sheria ni uhayawani.
 
Back
Top Bottom