pole sana mpendwa.
mama tuli ni kweli unaweza shirikishwa lakini mwenzio moyo upo kwa mwingine. Nakubaliana na afrodenzi alivyosema ni ngumu kumuelewa mtu. Katika mahusiano kuna mambo ambayo tusipofanyiwa tunajihisi hatupo katika mahusiano sahihi au wapenzi si sahihi kwetu na inawezekana hisia hizo ni za kweli. Unaweza kujifeel kawaida utakaposhirikishwa ila ukajifeel vibaya. Imagine una mpenzi, muda unampigia muonane anakwambia yupo mkoani kikazi! Unajisikiaje kwa kutopewa japo taarifa tangu awali. Ni mambo madogo madogo lakini yanaweza chujisha mahusiano.
mpendwa nilifikiri namba yako ni ile ile kumbe umebadili maana nilikupigia sijakupata! Ndio nini kubadili badili namba? Nitumie hiyo mpya. Halafu post yako ya mwanzo kama umesikitika vile. Hebu funguka kidogo.
Ni kweli hakuna recipe ambayo inaweza kuwagusa watu wote...Ila zipo ambazo zinawagusa wengi...Kama una idea ya kitu kinaitwa normal distribution, basi utakubaliana nami kwamba mawazo ya Hus yanawagusa wengi....Pia soma ushuhuda wa Kokutona!!
mmmmhhh hilo waliseme wengine na sio wewe.wengine hatupendi.
kwa hiyo ndo yale yale? Just boom boom and no fyucha?hatutarajii.
Nimeupenda sana mchango wako kwa sababu upo katika uhalisia wa maisha ya kweli na si haya ya kidotcom.
Nimalizie kwa kulonga kimombo.
A successful marriage requires a lot of give-and-take between husband and wife. Not from husband to wife or from wife to husband. The same applies to a boyfriend-girlfriend relationship.
pole bila ushauri?mwambie Rejao akupe desa!
ngoja nitafute dikshenare.Nimeupenda sana mchango wako kwa sababu upo katika uhalisia wa maisha ya kweli na si haya ya kidotcom.
Nimalizie kwa kulonga kimombo.
A successful marriage requires a lot of give-and-take between husband and wife. Not from husband to wife or from wife to husband. The same applies to a boyfriend-girlfriend relationship.
Bahati mbaya natumia katochi kangu nimeshindwa ku-like....very good point.
we mwaga tu sera bana,au ushakaa kaunta dragon? Nakuja ngoja nimuage Husn.Na huku upo
naona mabinti wanashauriana mambo yao
hapa nikichangia ntaharibu hali ya hewa tu
sababu haya mambo bwana hayanaga fomula
Ni ile ile mpendwa wangu labda network ilikuwa inazingua! Mengi yameshaongelewa, na ulichokiandika hapo ni kweli kabisa!!! Kuna watu wanasema mapenzi hayana fomulae(fine).........ila mapenzi yasimfanye mtu kuwa mpumbavu au mzembe kiasi cha kushindwa kusoma hata alama za nyakati ilihali dalili zote zinaonekana kabisa! Kwa mdada makini na mwenye determination na future yake lazima awe makini na achukue tahadhali sio kila siku ni kutoa tunda alafu mwenzako anapotea.....then anarudi tena kwa ajili ya tunda, sasa hapo utahesabu una mtarajiwa kweli??? Mpenzi anakutishia kukuacha kwa sababu hujampa tunda, basi kwa kutofikiri nawe unatoa eti unahofia kukimbiwa.......does it make sense kweli??? Kila siku unayoenda kumtembelea wewe ni wakupelekwa gest tu au kwenye geto la wenzake, jiulize huko kwake kunani??? Lol......uandishi wangu wa mwanzo usikustue sana, ni kweli......today am not feeling well my dear!!
babu unanidai kikombe cha kahawa. Lol.
Mkuu,
Michango mingi kwenye uzi huu haikubaliani na wewe.....Mwanamume ni donor .....kama huwezi kutoa mafweza na mazawadi basi pole sana....Kwa hapa MMU, sample size yako itakuwa kama vile haipo!!
Ni kweli kabisa HUS... Yamenikuta hayoo. Kuja kujua mshkaji hakuwa kweli serious kuwa na future na mimi nilikuwa too late. Ilinipain sana, sbbu nilikuwa nimejitoa kiukweli na alikuwa na ananipa matumaini chanya. Leo nimesoma hii thread no nimetafakarii na nimegundua kuna ukweli kabisa, na yaliyonitokea ni kweli yanaendana na idea yako.
Kwa wanaume msio wakwwli kwa wapenzi wenu, please at the beggining of mahusiano yenu, ni vema ukawa muwazi kabisaaa on what kind of relation unahtaji kwa hyo mpenzi wako. i.e wakuzugia, short time, long term friendship without marriage, mchumba na baadae awe mke e.tc. Mnatuuumizaga sana psychologically.
FaizaFoxy,naomba tuwe marafiki!Mie umeniwekea "speed governor":
"Thread hii ni maalum kwa wadada hasa waliopo kwenye mahusiano ila bado hawajaolewa..."
Nilipita kusalimia tu, lakini nipo nawachungulia tu, mambo mazito haya mie yamenizidi kimo.
kwanza pole kipipi. Tutaongea mengineyo pembeni. Pili ni kweli uliyosema, hakuna anayeishi kwa formular kwamba jana iwe sawa na leo na kesho. Hapo kwenye kushindwa kusoma alama za nyakati ndo huwa nawashangaa wadada! Unakuta mdada kuna kila dalili anaoneshwa kuwa haitajiki lakini anataka hadi atamkiwe. Khaaaa!
which begs a question Koku,huwezi kuwa rafiki na mtu mpaka mvalishane pete?
Hus,
Mwakani utafute nafasi pia, uwashauri wajukuu zangu ambao wameshusha thamani matunda yao na kuyatumia kukamatia kila kitu hadi kunguru!!
Ni kweli kabisa unachosema. Na sidhani kama hata kuna ambao wameelewa nilichoandika. Licha ya hivyo, ndoa ni partnership. Inahusisha watu wawili katika hali na mazingira yote - shida na raha, milima na mabonde, road bumps, na kadhalika.
Ni imani yangu kuwa ushirikiano unaimarisha ndoa (mahusiano). Ushirikiano unaifanya ndoa iwe na upendo. Kwa hiyo hii dhana ya kwamba mwanaume ndiyo mtoaji na mwanamke ndiyo mpokeaji mimi naikataa kabisa. Imepitwa na wakati.
Lakini kwa vile ndoa huhusisha watu wawili (yeah, wakati mwingine zaidi ya wawili), I am all for couples defining their own roles in their own marriage/ relationship. Imposing my values on others is just not my shtick.
Au wewe unaonaje kaka? Nimepotoka?