Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Habari za siku, hope ya’all good.
Ladies nasikia March 8 ilikua ni siku ya wanawake Duniani, hongereni hata sikujua nimesikia tu kwenye radio. Nawapongeza pia kwa kupewa hadhi kubwa hapa duniani kuliko kiumbe yoyote, na aliyewaumba amewapa hadhi ya uungu maana kupitia nyie mungu anakamilisha hatua yake ya uumbaji kwa kuhifadhi na kuzaa watoto…So nyie ni Miungu yetu humu duniani baada ya MUNGU, Lakini kunasehemu moja tu mnapofeli …
Inawezekana umehitimu masomo yako labda miaka 5,1,2,3,4,6 iliyopita lakini hujapata kazi maisha yamekubabua hasa huna nyuma wala mbele hata hela ya pedi ,mafuta,nguo,poda umekosa au unapata kwa shida. Huna amani umri unaenda barua umesambaza kila mahali interview umefanya ila majibu positive hakuna. Siku umekaa unapigiwa simu na meneja uende kufanya usahili, Kutokana wewe umejaliwa uzuri wako wa asili meneja/HR huyo aseiye na maadili ya taaluma yake na Utu anakutamani na kukushawishi kwamba uumpe rushwa ya mapenzi kwa ahadi ya kukupatia kazi, Basi kwakua wewe una shida zinakutesa unaamua kumkubalia maana ukizingatia kama ni kufanya mapenzi tu hamna shida Utamu unapata na Kazi Unapata....My Dear friend kama ushawahi kufanya hivi au upo Dilema unataka kufanya hivo basi itakua ni moja kati ya makosa makubwa uliyowahi /unayotaka kufanya (Ikiwemo na kupoteza bikra kabla ya ndoa)…Kwanini itakua ume mess Up?
Mwili wa mwanadamu ndani yake kuna roho wa Mungu ambayo ni ile pumzi ya uhai aliyokupatia so ile ndio hua kama taa yako inayowaka ndani ndio maana mwili wako hua unaitwa ni Hekalu la Mungu. Unaporuhusu kufanya mapenzi ili kutatua shida zako basi unakua umetia doa maisha yako, doa hilo hua halitoki kirahisi. Hatima ya maisha yako ipo mkononi mwako, matendo yao ya sasa ndio hutafsiri maisha yako ya baadae. Katika maisha kuna nguvu ya asili Inayosukuma mambo Postive katika maisha yako na kuna nguvu ya asili ambayo inasukuma mambo Negative maishani mwako…Watu wanaoamini katika mungu wanaita nguvu hiyo Postive Kua ni Mungu na hiyo ya Negative wanaita Shetani, watu wa Falsafa na Saikolojia tunaita the power of Nature and Subconcious Mind.
Pindi unapoumbwa unakua upo clean kama karatasi jeupee maisha yako yankua yamejaa nuru na ile nguvu Postive au Nature inakua inasukuma mambo positive pekee kuja maishani mwako hivyo maisha yanavyoendelea ndivyo tunazidi kuchafua miili yetu kwa matendo yetu hivyo tunaifanya nature kusukuma mambo negative maishani. Hivyo basi kama HR kakuambia ili akupe kazi inatakiwa umpe penzi basi unakua umeikaribisha nature isukume mambo yaliyo negative maishani mwako..Kwa lugha nyepesi ni kwamba utakua umemkaribisha shetani maishani mwako akuongoze.
Ukishamkaribisha tu kwa kutoa penzi ili upate kazi basi maisha yako yote hutapata kazi mpaka utoe penzi, sio kwenye kazi tu hata kwenye mambo unayokua unataka kupata huduma utakuwa unajikuta mtu aliyetakiwa kukupa huduma anakuomba rushwa ya ngono kwanza. Then utaanza kujiona kua una bahati mbaya/mikosi kwa kuombwa rushwa ya ngono kumbe mwenyewe ulishaharibu mfumo wa maisha yako, umekubali shetani aamue hatima yako kutokana na matendo yako (umeiruhusu Nature iwe inasukua mambo negative maishani). Jitambue!
Mungu alipokuumba alikupa akili nautashi wa kujua mema na mabaya, kakuleta duniani alishapanga mapito yako yote. Wanadamu hatujui hatima yetu aijuae ni muumba lakini hiyo hatima yetu tunaweza kuiharibu au kuifanya iwe hatima njema..Kuharibu au kuijenga itategemeana na matendo yetu na Imani yetu thabiti juu ya muumba. Aliyekuumba (kama waamini katika uumbaji wa Mungu)anakujua! Anajua unashida gani,anajua unahitaji nini,anajua ni muda gani sahihi wa kukupatia …kakuumba yeye hawezi kukutelekeza.
My dear sister kitu kinachofanya tunashindwa kupata yale yanayofaa tuyapate ni kutokua na Subira! Tunapenda kuwahisha mambo ili tupate yale ambayo tunayataka kwa muda Fulani tunaotaka ila tunasahau kua yatakiwa tupate yale yanayostahili/yatufaoyo kuyapata kwa muda ufaoa. Subira na utii wako ndio ghalama pekee ambayo unatakiwa uilipe kwa Mungu ili upate yale unayostahili kupata. Kama huwezi kusubiri upate yale unayostahili kwa muda unaostahili ila unataka upate yale unayoyataka kwa muda unaoutaka hivyo jua unamkaribisha Shetani maishani mwako maana utakua huna tena subira, tama itakua imejaza moyo wako na shetani ndie anayetoa vitu vya tamaa.
Haijalishi umekaa nyumbani bila ajira, umekaa muda gani bila mume,umekaa muda gani bila mtoto kamwe usiruhusu matatizo yako yakawa Advantage ya kukupata kirahisi, wewe ni wa thamani na mwili wako ni wa thamani ndio maana Mungu kakuamini na kukupa heshima ya kuufanya mwili wako ukamilishe uumbaji. Shida zako na mateso yako yasikufanye uishushe hadhi hiyo uliyopewa kwa kuwaacha mameneja wakutumie kadri wawezavyo. Muda ukifika utapata yote mazuri yaliyoandaliwa ajili yako..Huna haja ya kuwahisha mambo hadi unaamua kugawa penzi ili upate ajira. Jithamini, U wathamani mno!
In other hand mnaweza sema kua labda ninapendelea sijazungumzia wanaume wanaoombwa rushwa hiyo na kuwapa maHR wanawake..My Dear Dunia hii imekaa kuume hata huko kwa Mungu mambo yamekaa kwa mfumo dume..tendo la kufanya mapenzi limekaa kiume yaani siku zote mwanaume hua ni mfanyaji hata kama kalazimishwa na mwanamke. Hata kama mwanaume akilazimishwa na mwanamke kwake litakuua jambo la kujisifia ila kwako mwanamke litakua jambo la aibu ndio maana kamwe huwezi wanamke hawezi mwambia mwanaume wake kua “baby come here, I wanna fucck you”! Atasema baby “come here I wanna you fucck me”…kama vitendo vya wanaume kuombwa rushwa vipo basin i kwa kiwango kidogo mno na kwa upande wake yeye mwanaume hana hasara!
Sikupangii jinsi ya kuishi, ni ushauri na siku zote ushauri unaweza chukuliwa au kuachwa ila jua wewe ndio unaweza kujenga au kubomoa hatima ya maisha yako kutokana na matendo yako, fanya kila aiana ya upuuzi kwenye sinia hili tunaloita dunia ila HESHIMU MWILI WAKO NI WATHAMANI (A wonderful made) . Lakini pia kwenu watu mliopewa dhamani ya kua kwenye ngazi za juu katika mashirika na makampuni jitahidini muwe na utu na kujali maadili ya kazi zenu. Kama unataka kumsaidia mtu saidia then mwache aende sio umtake kimapenzi, hata usipomtaka kimapenzi basi msaada wako usiwe fimbo ya kumchapia. Umnyanyase kiakili na kimwili kisa bila wewe asingepata kazi hiyo. Saidia kisha futa kabisa katika kumbukumbu zako kua uliwahi kusaidia mdada Fulani kupata kazi katika kampuni uliyopo. Hupati faida yoyote ukitangaza kama uliwahi msaidia mtu Fulani.
-Life is full of Surprises and Possibilities, Tuheshimiane .
Naombeni radhi kama nitakua nimetumia maneno yasiyo na staha
Ahsanteni
-Da’Vinci
==Updates==
Post hii niliiandika kwa wema kabisa, lengo ilikua kuwatia moyo wadada ambao wana changamoto za maisha kua wasikubali kutumiwa kimapenzi ajili ya shida zao. Pia kuwaonya watu wenye tabia ya kuomba rushwa ya ngono.. Ila kuna watu wamekuja kubadiri upepo/Lengo kuu la mada hadi inaonekana kua mimi nawasema vibaya wadada. Sio vizuri kufanya hvo jamani, mimi siwezi kukaa na kuandika mambo ya kuwasema vibaya..wote tu wanadamu hakuna mkamilifu..Sawa tu jamani