Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,215
- 3,076
Mpe binadamu mwenzio heshima anayostahili!
Kama ni mpuuzi je wale wanaomjadili si wapuuzi pia..?!
Ni mtazamo tu I dont wanna to offend anybody.
Napenda nirekebishe baadhi ya kauli ambazo zimezungumzwa na baadhi ya wachangia maoni wa website moja hivi, (jina si muhimu kutaja).
Ila najua watasoma kwani kila mara wamekuwa wakiingia na ku copy paste ishu za humu kuziweka kwenye ubao wao na kuanza kuzijadili.
Kwenye site hiyo ambayo wengi wao hujiita wasomi na kusema sana wengine, kuna waliosema kuwa mkoa wa Mara kuna makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo na zilizobaki zingine zote ni koo tu.
/
Napata mashaka sana na upeo wa kufikiri wa huyu BINTI MACHOZI na majibu haya yananifanya nimwone ni mwanamke anayependa visasi, majungu na kutokubali kushindwa hata kwenye hoja za kawaida tu ambazo zinahitaji majibu ya moja kwa moja pasipo kuchambuana.
Labda kama ipo hivi hata huko nyumbani, basi ni balaa kwa "Mzee wa Majahazi":
wakiingia na ku copy paste ishu za humu =tafsri yake ni nini, kwamba za humo ni za busara sana au hazipaswi kujadiliwa popote?. Nini dhana ya kuja kusomea humu na kwenda kujibia kwenye blog yake ambapo kinadharia hoja imetokea humu ambao yeye anahisi hao wanao waeleza hawaingii humu?
kuziweka kwenye ubao wao = wao kina nani? sio hao ambao pia wapo humu JF?
Kwenye site hiyo ambayo wengi wao hujiita wasomi na kusema sana wengine = hujiita wasomi wapi? na kama hivyo sivyo, ya nini kusema "wanajiita" ?
Sikuelewi. Unapinga nini hapa? Kwamba JD sio mpuuzi? au?
Wapi nilipopinga zaidi ya wewe kushindwa kujibu swali nililouliza?!
Hoja muhimu hapa ni kujaribu kuheshimu maoni ya mtu hata kama hukubaliani nayo na wala sio kutumwita mpuuzi. Kama waona alichoandika ni pumba basi tuandikie mchele ili tuweze kupembua mchele kutoka kwenye pumba.
Kichuguu,Kumbe Jay Dee ni mshashi, nilikuwa sijui; nadhani hilo ndilo kabila la mzee Wassira pia. Pamoja na udaku huo, ni kweli Jay Dee kaongea point nzito kabisa kuhusu tabia yetu mbaya ya stereotyping.
Wanapomjadili anyamaze na kujifunza kutoka katika majadiliano yanayomhusu yeye. Hajajua mpaka leo gharama ya umaarufu?(hata kama ni umaarufu uchwara)Mwacheni jamani dada wa watu mbona mnamsakama sana.Ahsanteni
WAKURYA NA WASIZAKI HAWAZUNGUMZI LUGHA MOJA WALA MILA HAZIFANANI....KAMA AMBAVYO SITE MOJA YA KU COPY PASTE NA WATU WAKE WALIVYOONGELEA
Napenda nirekebishe baadhi ya kauli ambazo zimezungumzwa na baadhi ya wachangia maoni wa website moja hivi, (jina si muhimu kutaja).
Ila najua watasoma kwani kila mara wamekuwa wakiingia na ku copy paste ishu za humu kuziweka kwenye ubao wao na kuanza kuzijadili.
Kwenye site hiyo ambayo wengi wao hujiita wasomi na kusema sana wengine, kuna waliosema kuwa mkoa wa Mara kuna makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo na zilizobaki zingine zote ni koo tu.
Na kuwa katika Category ya wakurya ndio kuna wazanaki ambao ni pamoja na JK Nyerere na wasizaki ambao ni kina sisi na kuwa wote tunaongea lugha moja. By the way mama yangu ni mu Ikizu sijui nae watamuweka category gani maskini ya Mungu??
Lugha ambayo na hakika kuwa matamshi yao ni sawa sawa ni Ikizu na Sizaki.
SALAAM KWA BABA:
Wa Ikizu na Wasizaki wanasema Bhaa
Wa Kurya wanasema Tata
SALAAM KWA MAMA:
Wa Ikuzu na Wasizaki wanasema Iya
Wa Kurya wanasema Mayi
SALAAM KWA BIBI:
Wa Ikizu na Wasizaki wanasema Koko
Wa Kurya wanasema Ghoko
Swala la maneno kukaribiana linaweza kuwepo kwenye lugha zozote za kibantu kwa mfano
Nyoka ni kiswahili, kikwetu ni Inzoka lakini kwa lugha ya kizulu pia ni Izinyoka
Chumvi inaitwa " munyu/ Umunyu" na makabila mengi tu....
Nakupenda kwa kichaga NAKUKUNDA, kirundi na kinyarwanda NDAGUKUNDA, na hizi ni nchi tatu tofauti...
au basi labda afrika nzima hakuna makabila zote ni koo??? maana maneno mengi tu ya lugha za afrika yanafanana, sio lazima kuwa msomi sana kutambua ulimwengu unaendaje, Dunia yenyewe shule tosha.
Wambura ni jina langu na sio surname yangu kama ambavyo wengi wanadhani, kuna makabila mengine Wambura ni mwanaume kama Wakurya ila kwa sisi Wambura wengi ni wanawake.
Baba yangu anaitwa Lameck Isambwa Mbibo (RIP)
Niliandika tu kuwa mimi kabila langu ni Msizaki na sio Mkurya kama ambavyo watu wengi wanadhani.. Ila naona imechukuliwa kana kwamba nakana ukabila
Chanzo: http://www.ladyjaydee.blogspot.com/
Wanapomjadili anyamaze na kujifunza kutoka katika majadiliano yanayomhusu yeye. Hajajua mpaka leo gharama ya umaarufu?(hata kama ni umaarufu uchwara)
Binti umenena. kwani hakuna mtu aliyechagua wazazi wa kumzaa wala kabila wote wamejikuta katika ukoo/kabila fulani. Hivyo kujumuisha ki-ujumla siyo sahihi.source: ladyjaydee.blogspot.com
Uniite mzanaki, mkurya, mjita, mjaluo, mkwaya, mkerewe I do not change. Jamani hii issue mbona broken record. Hivi kutoka mkoa wa Mara ni laana?
QUOTE]
Acheni kuchinjana mura inaweza kuwa laana.
Hapo kwenye red sidhani, hakuna mayi kwenye ukurya , mayi ni kwa wajita, mkurya humsalimia mama, bhabha.
Mi sioni kwa nini JD anaikuza sana hii ishu na kujikita muda mwingi kubishana na JF, thats wastage of time maana watu wa jf wengi wakiamua kwenda naye papendicular sidhani kama atatoboa. so sisy just chill hata kama dunia shule tosha, hata shule ya ukweli ina umuhimu. so acha vijineno vya kitaa as if huna exposure. Ni hizi hizi critisism ambazo zinakusaidia in one way or another
she has all the rights to say what she feels!!!!!!