Lady Jay Dee akerwa kuzushiwa kutundikwa mimba

Lady Jay Dee akerwa kuzushiwa kutundikwa mimba

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304


Mwanamuziki nguli wa kike hapa Tanzania Lady JayDee ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao walimuelewa vibaya baada ya kupost picha jana na kusema kuwa tumbo lake limevimba na kusema ana mimba..

"Imebidi nifute post Ili nielezee upya. Hivi watu hamuelewi Kiswahili au ni nini? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani, nikimaanisha mlo na nilipost nakula hapo awali, Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina?
Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakayewatoa katika shida zote mpaka mnishikilie mimba mimba.. Hebu niacheni basi khaaa, Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa." aliandika Jide

Unalipi la kumwambia Jide hapo?
 
Na yeye anadhani watoto ni ugonjwa.Umri unamruhusu asijipotezee muda
 
Hehehe ukiendekeza IG unaeza kufa siku sio zako
 
Ni kweli baadhi ya watu wapuuzi sana. Wanaacha au wanashindwa kufanya ya kwao, kucha kutwa kumfuatilia binti wa watu.
Mwacheni na maisha yake.
 
Kutokuwa na mtoto ni stress sana huku duniani
 
Mungu atampa naye atapakata ikifika wakati! Pole mami!
 
Watoto anatoa Mungu kwa wakate wake , acheni kunyanyasa wanawake wasiokuwa na watoto wangali hai ?? hata wewe mwenye nao omba sana , watoto hao hao wanaweza kukutoa Roho ! MMezidi wacheni aseme tu ...Hata Biblia inasema

""heri tumbo lisilozaa maana siku ya mwisho katika hukumu kutakuwa hakuna baba, wala mtoto wote tutahukumiwa na kupewa tulichopanda sawa kwa sawa""
 
Jide kumbe anamaneno Machafu sana lol.Inaelekea hakufunzwa na wazazi wake vizuri.Mtu mzima kuwaambiwa watu upuuzi ni upuuzi kuliko aliowaambia.Kasikia watu wanashida ya Raisi wa kuondolea watu matatizo?

Hili ni Bonge la kashfa kwa Watanzania na Raisi aliyepo Madarakani.Maneno machafu anawaambia washabiki wake ati waachane nae! ajui mlo anaoupata unatoka kwa hao hao anaowatusi.

Angesema tu hana Mimba na wamemuelewa vibaya ingetosha.Huyu atakuwa dini kaiweka pembeni Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Judith ni Mpuuzi awaombe radhi Watanzania.
 
Back
Top Bottom