Lady Jay Dee amka, kiti chako kinataka kuchukuliwa

Lady jay dee huwezi kumlinganisha na hao ni dhambi kubwa sana! Ni sawa na kumfananisha Mh Sugu na Young killer! Tena wote mnao mlinganisha Jide na rubby nikiwafahamu wote nawapeleka mahakama ya makosa ya jinai ICC!!
 
Ni wakati wa mabadiliko...hatutaki kuwaona watu walewale,wakifanya yaleyale,kwa nafasi zilezile...!Tumechokaaaaa,Muda wa mabadiliko ndio huu.

mnayataka mabadiliko kwa nguvu mtawabadilisha mpaka wazazi wenu maana hao mlio nao wakitambo sana wapigeni chini
 
Lady jay dee huwezi kumlinganisha na hao ni dhambi kubwa sana! Ni sawa na kumfananisha Mh Sugu na Young killer! Tena wote mnao mlinganisha Jide na rubby nikiwafahamu wote nawapeleka mahakama ya makosa ya jinai ICC!!
Haha umeuwa mkuu haa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Mheshimiwa huo mfano wa MJ naona kama ni irrelevant.... Anyweiz kila zama na nabii wake
 
Tatizo lenu mnaandika pasi na kujua dhima ya mada.Mnachanganya "NJEO" kwa wasanii hawa wawili.
Kama hii story imeegemea "Past tense" basi Jide ni mzuri na hakuna mfano.
Kama hii story imeegemea kwenye "present tense" basi ni wazi Vanessa anakuja juu zaidi na kummeza jide (kwa sasa)

Hii haina uhusiano na ukali wa msanii mmoja mmoja mana wamekuwa juu kwa nyakati tofauti.
 
Mheshimiwa huo mfano wa MJ naona kama ni irrelevant.... Anyweiz kila zama na nabii wake
Wala sio irrelevant ndugu yangu na hata ukiangalia hits nyingi za MJ ni zile za 1980's to mid 1990's!Inawezekana alikuwa hajashuka kimuziki lakini sidhani kama kuna ngoma ya MJ ya mid 1990's kuja huku ambayo unaweza kulinganisha na pini kama Thriller, Billie Jean, Heal The World, Black or White, Liberian Girl n.k! Hii Liberian Girl hadi leo nikiisikiliza mwili unanisisimka! Hebu na wewe jikumbushe halafu nitajie wimbo wake mmoja uliotoka frm mid 1990 ambao unaweza kuulinganisha na angalau LG achilia mbali Thriller au Heal the World!!!

 
Last edited by a moderator:
Reactions: me1
Huu mziki wetu hivi sasa umekua. Mambo ya msanii kuona yuko top all time umeisha hakuna kiti cha mtu watu wanafumua tu ngoma kali videos kali hili ndilo swala la kujivunia sana kwetu. Tena wazidi kuongezeka kina Vanessa wengi Jide atabaki kama Legend na wengine walioUweka huu mzika kwenye Map
 
Ahsante... ingawaje mada imeandikwa Kiswahili lakini kuna watu bado hawaelewi!
 
Jide wakati wake ulisha kwisha..
 

Asante mleta uzi, leo umenipa kuwafahamu vizuri sana hawa wanaojiita team kiba, nimegundua wanaugonjwa wa kukariri, ukiangalia arguments zao kuhusu kiba ni copy and paste ya hizi nazoziona kwenye huu uzi, eti kwa vile tu kiba alishafanya vzr huko nyuma, hata asipofanya vzr sasa bado wanaona yupo juu, ona sasa wanachobishana hapa, eti kisa jide alikimbiza huko nyuma hizi damu changa za akina v money haziwezi mpita, sasa mwambieni kama anajiamini afanye ujinga aliofanya kiba, ajitie uqeen wa bongo flava akae benchi miaka hata miwili tu alafu arudi na zile mbwembwe za nimekuja kufuta vumbi kiti changu, kama kama kibakuli wenu anayeng'ang'ania jina la uking ambalo halimtaki hata kwa mbali, kiba kashaonja joto ya jiwe, ya kufungia sauti kabatini miaka 3, jide kuna siku alisema, anauwezo wa kukaa mwaka mzima bila kufanya kazi na bado akala na kunywa, kweli atakula na kunywa kwa vile yeye ni mtoto wa kike, na anahazina ya jina, lakini wakati huo huo tunaskia kauza bar, Alivyouza bar alisema something big is coming (in wema sepetu's voice) lakini mwaka unakatika sasa sijaona something big wala small, labda mniambie anajenga kiwanda sehemu, mara nyumba inapigwa mnada, trust me hata kama alitengeneza jina kiasi gani akiendekeza huu ukimya ambao bado haujaeleweka kama ni wa kufulia au wa makusudi, ule wimbo wake wa historia utamuhusu.
 
Hivi mnatumia vigezo gani kusema HAWEZI kumfikia miaka 800? Hivi kweli unaamini toka ndani kabisa ya moyo wako kwamba Jide alifikia hatua ya juu kabisa mwanamuziki kuwahi kufikia?! Do you?

Bahati nzuri sana kuwahi kutokea kwa jide, hakuwahi pata competition ya maana kwa wasanii wa kike, its all like alikuwepo peke yake tu kwenye soko la wasanii wa kike, ndio maana sifa zote zinamuangukia na mtu huwezi bisha coz who else was there? Na kitendo cha jide kuwepo peke yake, macho ya watu wote kumtazama yeye tuu, akapata kichwa, jeuri na kujiamini kupita kiasi, majina yote ya kibabe babe akajiita. So nakubaliana na wanaosema kumfananisha na hawa wasanii wa kike wapya sio sawa, NI KWELI SIO SAWA, lakini from now onwards she an't a shit anymore.
 

Wewe Kweli upo slow so nani kama jide tanzania sahv?kwa sauti na mashairi
 
Kila zama na kitabu chake..

Zama zilee alikuwaga jide, ray c n.k

Zama za juz juz walikuwa wakina linah, mwasity....n.k

Zama za leo tuna v-money, rubiii.....n.k

Umemaliza
 
Wewe Kweli upo slow so nani kama jide tanzania sahv?kwa sauti na mashairi

Sasa hivi as u said, but not anymore, unless atoke kwenye usingizi aliolala, soma vizuri kichwa cha habari cha uzi, anakumbushwa kuzinduka otherwise atasahaulika, hatujasema kashashuka lah! Ila akumbuke tu kuwa she was just all alone in the market na ndio maana alikuwa hata akae mwaka hajatoa wimbo bado alionekana yupo juu, hakukuwa na mwingine wa kumuongelea, ila from now kama anajiamini akae chini hata mwaka tu ajiite legendary hawezi kushuka,pamoja na sauti yake ya kisabato na mashairi unayosema then uone kama hajabaki historia, soko la music la sasa sio lile walilotawala kipindi kile, mfano nzuri ni kiba, pamoja sauti yake nzuri lakini kitendo cha kukaa benchi miaka mi3 karudi kawa kama new msanii anayetafuta kutoka. Kishabiki utakataa lakini kiuhalisia hali ndivyo ilivyo na wote tunaliona hilo.
 

Apo umetisha kaka
 
Paula, kuna mahali nimesema wazi kwamba kwa heshima ya Jide watu tunaacha kuzichambua tuzo zake hususani zile zinazoitwa za nje... wewe umezungumzia moja ya hayo mambo ambayo watu wanajitia upofu na kutoyaona! Na in fact, kilichopo hapa ni kwamba wafu wa kambi mbili wanazikana wao kwa wao huku wakitarajia muujiza uje uwafufue kwavile tu nao walipata kuwa world citizens! Thanks....
 
You said it all PK!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…