Lady Jay Dee na ujumbe wake ndani ya “yahaya vs wanaume kama mabinti”

Lady Jay Dee na ujumbe wake ndani ya “yahaya vs wanaume kama mabinti”

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
489
Naomba kwanza nikili kuwa mimi si mshabiki sana wa nyimbo nyingi za kisasa (Bongo Flava) kama ilivyo kwa miziki ya wazee sugu japokuwa zipo baadhi ya tungo ambazo zimesheheni ujumbe maalumu katika jamii zetu zinazotuzunguka.

Lady Jay Dee ni mmoja kati ya wanawake wa kisasa na wasanii ambao wameweza kujiepusha na maisha ya kukurupuka kama tunavyowaona wengine, japokuwa naye kama si kushikwa sikio na waliomtakia mema na akawasikiliza alikuwa ameanza kuelekea huko (Labda ndoa nayo ilimuokoa)

Jay Dee amekuwa akienda kwa matukio; kwa wale wanaokumbuka kipute kilichopita wakati wa kipindi cha penzi lao pevu na GADNAH hadi wakatupiana vialago kweupe, aliamua kumuimbia wimbo………… "WANAUME KAMA MABINTI" japo mwenyewe alikanusha kuwa hakumuimbia yeye lakini ukweli ulibaki palepale.hatimae penye wengi hapakosi wenye busara kama MIMI kwani waliweza kuwasuluhisha na hatimae maisha yakarudi kama mwanzo na matunda yake sote tunayaona.

Leo JIDE amekuwa na mgogoro na uongozi wa CLOUDS kiasi cha kushutumiana na kutoleana maneno makali hadi kufikishana Mahakamani, kama kawaida yake kaingia jikoni katoka na ugali "YAHAYA" ukisoma maudhui mengi ya wimbo huo, yanaonesha dhahili bila chenga kuwa ni madongo kwa mtu/watu fulani ambao, aidha anajua siri ya maisha yao na jinsi ambavyo wamekuwa wakijonesha mbele ya jamii kama watu BAB KUBWA! na wenye nafasi nyingine zaidi ya zile zinazonekana machoni pa watu. Je, wewe kama mfuatiliaji wa mambo unaona wimbo huu YAHAYA umelenga wapi na kwa nini?
 
Mkuu wanaume kama mabinti ni alikuwa papii kocha sio gadna, ila kama nakumbuka vizuri cjui wadau hebu tulikumbuke hili.
 
MODES wasipotoa hii thread ninaandamana
kwanini?

kwa sababu mie nilianzisha thread kama hii wakaifunga tena bila sababu ya mie kutumiwa ujumbe kuelezwa sababu ya kwanini waliifunga

anyway

tuendelee kujadili yahusuyo mada hii

ya modes tuwaachie modes
 
MODES wasipotoa hii thread ninaandamana
kwanini?

kwa sababu mie nilianzisha thread kama hii wakaifunga tena bila sababu ya mie kutumiwa ujumbe kuelezwa sababu ya kwanini waliifunga

anyway

tuendelee kujadili yahusuyo mada hii

ya modes tuwaachie modes

Modes ndio kitu gani mkuu?
 
Back
Top Bottom