Lady Jaydee ahamia hotelini

Lady Jaydee ahamia hotelini

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ' Jide ' ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika , anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara - Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.

Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash . Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005 .

Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake. Hata hivyo Ijumaa iliyopita Tulizungumza na Gardner ambaye pia ni meneja wa msanii huyo, lakini alikanusha vikali uvumi huo akisema si kweli.

Kufuatia madai hayo, mapaparazi wetu walikwenda hadi nyumbani kwa nyota hao ambapo hakukuonekana dalili za kuwepo kwa mtu ndani . Baadhi ya majirani walioulizwa, walisema mara ya mwisho walimuona Gardner miezi miwili iliyopita akiwa na basi la Bendi ya Machozi lakini hawaelewi kwa sasa wanaishi wapi na wakoje katika ndoa yao! Juzi , mapaparazi wetu walipiga kambi hotelini hapo ambapo mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo alisema, Jide anaishi hotelini hapo na kwamba kutokana na kuwa mteja wa muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango wa chumba chake anaondoka nayo.

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Jide ( jina tunalo) alithibitisha msanii huyo kuishi hotelini hapo ingawa alikataa kuzungumza lolote kuhusu ndoa hiyo, kwa kile alichodai kuwa haieleweki .

"Ni kweli Anaconda ( Jide ) anaishi pale, wewe nenda tu mapokezi kaulize utaelezwa kama hivi sasa yupo au hayupo, " alisema mtu huyo. Juhudi za kutafuta ukweli wa sakata la nyota hao zinaendelea huku ikielezwa kuwa, Gardner ndiye anayetakiwa kutoa tamko kwani ndiye anayepatika kirahisi katika simu yake ya mkononi .
 
Hahaha hilo sukule linanifurahisha sana kokote nilionapo.....ila matumbo kama una dawa ya kumsaidia Matola basi pitia link hii hapa chini

Dawa ya Minyoo Sugu

Nimeichek iyo link jamaa anasumbuliwa na minyoo tegu anasikitisha sana.....Tatizo la kula matembere wanayokojolea walevi kila siku nyuma ya nyumba, na kunywa chimpumu.
 
Last edited by a moderator:
Hahaha wanavyomuwangia! Hotel sio kama gesti, za kila ukitoka unaacha funguo reception. Kadi unazurura nayo hadi siku unaondoka na ukiipoteza wanakupa tu nyingine.

Safi sana jide, wanyime usingizi wakome.
NYOTA wa muziki wa Jide anaishi hotelini hapo
na kwamba kutokana na kuwa mteja wa
muda mrefu, hata kadi ya kufungulia mlango
wa chumba chake anaondoka nayo ..
 
Eeeeeh!!! Binamu nimerudiii ila nimekondaaaaaa!!!!!! Mic u

Pole binamu, ICU ya kukosa umbea ni mbaya sana kwako hahahaaa. Tulikumiss kiama binamu. Binamu na wewe una nyota kali kama ya ndugu yako nanhiii. Ukaanzishiwa hadi kampeni ya kukurudisha loooh umeshindikana kiama. Jamani eeeh geniveros, Dinazarde, Heloo, ladykims, amu, ram na wapenzi wote wa binamu, binamu is in the building now
 
Last edited by a moderator:
Hahaha wanavyomuwangia! Hotel sio kama gesti, za kila ukitoka unaacha funguo reception. Kadi unazurura nayo hadi siku unaondoka na ukiipoteza wanakupa tu nyingine.

Safi sana jide, wanyime usingizi wakome.

Jide ni Bosslady maana hata hotel siyo zile za Sinza kajificha ushuwani kimya.
 
Pole binamu, ICU ya kukosa umbea ni mbaya sana kwako hahahaaa. Tulikumiss kiama binamu. Binamu na wewe una nyota kali kama ya ndugu yako nanhiii. Ukaanzishiwa hadi kampeni ya kukurudisha loooh umeshindikana kiama. Jamani eeeh geniveros, Dinazarde, Heloo, ladykims, amu, ram na wapenzi wote wa binamu, binamu is in the building now

Nimerudi binamu, yani niliwamisi kiama, hadi natetemeka apa maana nina maubuyu ya haja kiama, im back na wale ambao ujio wangu umewachefua ndimu zinawahusu, hihihii....
 
Last edited by a moderator:
Hahaha wanavyomuwangia! Hotel sio kama gesti, za kila ukitoka unaacha funguo reception. Kadi unazurura nayo hadi siku unaondoka na ukiipoteza wanakupa tu nyingine.

Safi sana jide, wanyime usingizi wakome.

Duh!! JIde katisha, ila bora aiseeh abadili mazingira kidogo na kutuliza akili, maana ndoa inachosha sana kukaa wote nyumba moja lazima mkwaruzane so nadhani akikaa kwa mda kidogo lazima ammis hubby wake na mambo yatakuwa poa tu soon.
 
Nimerudi binamu, yani niliwamisi kiama, hadi natetemeka apa maana nina maubuyu ya haja kiama, im back na wale ambao ujio wangu umewachefua ndimu zinawahusu, hihihii....
Namna ya kuepuka ban za JF ni kumpuuza mpumbavu yeyote anayekuprovoke usipowajibu wanaumia sana mioyoni mwao na kama huwezi kuwapuuza basi watupe kwenye ignore list na ban kwako itabaki kuwa historia.
 
Poa poa mkuu, shukrani maana duh safari hii nimepata BAN takatifu kweli
 
Back
Top Bottom