Lady Jaydee ajichagulia jeneza la pili

Lady Jaydee ajichagulia jeneza la pili

People Need to Get a Life....

Wewe kama ni shabiki kuwa shabiki wa kazi anazotoa sio Shabiki wa Maisha yake..., Tena mimi ninamsifu na wengi wangefanya hivi unanunua kabisa jeneza lako siku ukiondoka usituachie gharama za kuanza kuchangishana (usawa wenyewe huu uchumi wa kati) na Hatujui siku ukiondoka huenda Uchumi ukawa ushakuwa wa Juu....
 
Sasa anajichagulia jeneza , Je anajua atakufa kifo gani? What if akifa kwa kumezwa na papa huko baharini? What if akifa kifo cha kuteketea kwa moto tukakosa hata kipande cha mfupa wake? What if akifa kifo cha kupotea na ndege kama ile ya Malaysian airways flight 370 ya mwaka 2014???
Ana mawazo kimo cha mbilikimo
 
Yuko sahihi, lazima ujichagulie usafiri wako, sio mpaka uchaguliwe, tusisahau kifo ni jambo la lalazima(must).
Bangi kwasana hazitofautishi maisha na kifo. Tumhurumie huyu binti. Kazi ya muziki ni ngumu sana. Unatumia nguvu nyingi kuwafanya watu wafurahi,hadi mwili unakuambia mzee nimechoka .hapo ndipo matumizi ya sawa za maumivu, bangi heroin ,cocaine no inakuwa sehemu ya maisha. No wonder wengi hugs kwa overdose ya hago madawa. ( Elvis Presley,Michael Jackson , jim hendrix, whitney houston. N.k) wote ni wahanga wa ustaa wa music. Kuwasaidia vijana serikali zingeweka sheria za kupimwa mkojo kila baadae ya muda fulani ili kuokoa maisha ya vijana wa tasnia ya music. Maana husezi kuhimili stress za music bila kutumia illicit drugs, never on earth.
 
Bangi kwasana hazitofautishi maisha na kifo. Tumhurumie huyu binti. Kazi ya muziki ni ngumu sana. Unatumia nguvu nyingi kuwafanya watu wafurahi,hadi mwili unakuambia mzee nimechoka .hapo ndipo matumizi ya dawa za maumivu, bangi heroin ,cocaine nk inakuwa sehemu ya maisha. No wonder wengi wanamuziki wameishafariki kwa overdose ya hayo madawa. ( Elvis Presley,Michael Jackson , jim hendrix, whitney houston. N.k) wote ni wahanga wa ustaa wa music. Kuwasaidia vijana serikali zingeweka sheria za kupimwa mkojo kila baada ya muda fulani kwa wanamuziki kama wafanyavyo kwenye riadha ili kuokoa maisha ya vijana wa tasnia ya music. Maana husezi kuhimili stress za music bila kutumia illicit drugs, never on earth.
 
View attachment 1741195
Picha ya Mwanamziki Lady Jaydee


Uchuro? Baada ya kutundika mtandaoni kwa mara nyingine picha za jeneza alilojiandalia litakalotumika siku akiaga dunia, mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide, amelaaniwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho.

Abadili rangi
Mwaka 2012, Jide alitupia mtandaoni picha za jeneza lake lenye mchanganyiko wa rangi ya zambarau na nyeupe lakini safari hii amebadilisha na kutupia mengine mawili yenye rangi ya krimu na nyeupe.

Maneno kuntu
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo anatumia jina la jidejaydee, juzi, mwanadada huyo, pamoja na picha hizo mbili, alisindikiza na maneno kuntu kwa chini yaliyosomeka, ‘Nimebadilisha mawazo yangu, sitaki tena lile la zambarau. Moja kati ya hayo hapo juu. Msinimaindi. Kila mtu atakufa. Nilikuwa nafikiria pia iwe kwa waalikwa tu. Sitaki kufunuliwa’.

Mashabiki wamlaani
Risasi Jumamosi liliinyaka ishu hiyo sekunde chache baada ya Jide kuitupia ambapo ndani ya muda mfupi ‘posti’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ya kulaani kitendo hicho.
Baadhi ya mashabiki walieleza waziwazi kuchukizwa na jambo hilo alilolifanya staa wao wanayempenda.

Sehemu ya maoni
“Kifo kipo kwa kila binadamu lakini hatutakiwi kukifikiria hivyo dada (Jide) unamkosea muumba wako.
“Wewe ni kioo changu, ila kwa hili kwa kweli sijalipenda.
“Jamani dada mbona unatutisha au haupo sawa leo?
“Wewe wajina umefikiria nini lakini?
“Kama umeshaona unakufa sema tujue.
***

“Duh! Dada fanya maombi hiyo ni roho ya umauti.
“Dada nini tena mbona unamkufuru Mungu? Hata kama una machungu kiasi gani, huwezi kufanya hivyo kwani ni mipango ya Mungu. Muombe akusamehe.
“Wewe Jide wewe huogopi lakini?

“Najua sote tupo njia hiyo lakini kwa nini leo umeamua kutuandikia hivyo? Naomba mipango ya shetani ishindwe!” ilisomeka sehemu ya maoni hayo iliyoungwa mkono na baadhi ya mashabiki wake waliojawa na simanzi.

Mchungaji amuunga mkono
Akizungumzia tukio hilo, mchungaji maarufu jijini Dar alisema kuwa, kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa kuwa kila nafsi itaonja umauti hivyo ni vema kujiandaa kwa kutenda mema.“Maandalizi yanayopaswa kuwa makubwa ni ya kiroho kwa kuhakikisha unatenda mema ili kupata tiketi ya kwenda peponi na kukwepa adhabu ya Jehanamu,” alisema mchungaji huyo.

Kutoka Risasi Jumamosi
Kifo ni haki yetu lakini si vema kumchuria mtu au kujichuria kwa kuwa ni tukio lisilozoeleka katika maisha ya mwanadamu.

View attachment 1741210
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ameshaweka wazi mazishi yake yatakuwa ni kwa mwaliko maalum...yaani huendi tu kindezi.. Ila hajazungumzia swala la bajeti
Kalogwa au kajiloga
Atambue Ulimi Unaumba
Atakipata anachokiomba lakini itakuwa mapema sana kuliko anavyotarajia
Mungu ana wakati wake na Shetani ana wakati wake
Kwa mtindo huu shetani ana nafasi kubwa ya kufanya yake
Kama ni kutafuta umaarufu basi unakuja lakini utakuwa wa muda mfupi halafu utasahaulika milele

Naomba Mungu anipe busara na maisha marefu kuishi hapa duniani
 
Being dead is being dead.

Does the casket make a difference?
 
People Need to Get a Life....

Wewe kama ni shabiki kuwa shabiki wa kazi anazotoa sio Shabiki wa Maisha yake..., Tena mimi ninamsifu na wengi wangefanya hivi unanunua kabisa jeneza lako siku ukiondoka usituachie gharama za kuanza kuchangishana (usawa wenyewe huu uchumi wa kati) na Hatujui siku ukiondoka huenda Uchumi ukawa ushakuwa wa Juu....
Kuna yule mzee yeye kajijengea hadi kaburi lake freeeesh kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooh muziki stress kipi hakina stress? Mara oooh kutokuwa na mume na watoto kumempa stress, wenye watoto na waume/wake wangapi wamekufa kwa stress hizo hizo na wengine kujiua? Mnapoandikaga urithi mbona huwa hamsemi mnajichulia kufa?

Kufa kila mtu atakufa tu, uogope kifo au usikiogope ila mwisho wa siku wote safari yetu ni moja. Hapo hana tofauti na wanaosema nikifa mnizike chato, yeye kachagua jeneza swaaafi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooh muziki stress kipi hakina stress? Mara oooh kutokuwa na mume na watoto kumempa stress, wenye watoto na waume/wake wangapi wamekufa kwa stress hizo hizo na wengine kujiua? Mnapoandikaga urithi mbona huwa hamsemi mnajichulia kufa?

Kufa kila mtu atakufa tu, uogope kifo au usikiogope ila mwisho wa siku wote safari yetu ni moja. Hapo hana tofauti na wanaosema nikifa mnizike chato, yeye kachagua jeneza swaaafi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo hana tofauti na wanaosema nikifa mnizike chato, yeye kachagua jeneza swaaafi kabisa.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kidongo cha zege hiki
 
Back
Top Bottom