Lady Jaydee ajichagulia jeneza la pili

Lady Jaydee ajichagulia jeneza la pili

Hapa ndipo wafia dini wanaponiacha hoi, wanakwambia tenda mema uende peponi, blah blah lakini kwenye kifo wanaogopa, sasa kama mnaipenda pepo kwanini muogope kifo?

We all gonna die.
 
Hapa ndipo wafia dini wanaponiacha hoi, wanakwambia tenda mema uende peponi, blah blah lakini kwenye kifo wanaogopa, sasa kama mnaipenda pepo kwanini muogope kifo?

We all gonna die.
Nadhani watu hawaogopi kifo bali maumivu ya kufa
 
Nadhani watu hawaogopi kifo bali maumivu ya kufa
Wanayajuaje maumivu wakati hawajawahi kufa?

Yote kwa yote ni njia lazima tuipite hata iwe vipi, kwa hiyo Jaydee kuchagua jeneza lake sioni tatizo, kuna wengine hukata sanda zao wanaishi nazo kwenye makabati/sanduku,
Kuna wengine huandika urithi,
Kuna wengine huchagua hadi nyimbo za kusindikizwa nazo wakifa,

Kujiandaa ni jambo muhimu sana sababu ile ndio safari yako ya mwisho na yenye ulazima.
 
View attachment 1741195
Picha ya Mwanamziki Lady Jaydee


Uchuro? Baada ya kutundika mtandaoni kwa mara nyingine picha za jeneza alilojiandalia litakalotumika siku akiaga dunia, mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide, amelaaniwa vikali na mashabiki wake kwa kitendo hicho.

Abadili rangi
Mwaka 2012, Jide alitupia mtandaoni picha za jeneza lake lenye mchanganyiko wa rangi ya zambarau na nyeupe lakini safari hii amebadilisha na kutupia mengine mawili yenye rangi ya krimu na nyeupe.

Maneno kuntu
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo anatumia jina la jidejaydee, juzi, mwanadada huyo, pamoja na picha hizo mbili, alisindikiza na maneno kuntu kwa chini yaliyosomeka, ‘Nimebadilisha mawazo yangu, sitaki tena lile la zambarau. Moja kati ya hayo hapo juu. Msinimaindi. Kila mtu atakufa. Nilikuwa nafikiria pia iwe kwa waalikwa tu. Sitaki kufunuliwa’.

Mashabiki wamlaani
Risasi Jumamosi liliinyaka ishu hiyo sekunde chache baada ya Jide kuitupia ambapo ndani ya muda mfupi ‘posti’ hiyo ilikuwa na maoni mengi ya kulaani kitendo hicho.
Baadhi ya mashabiki walieleza waziwazi kuchukizwa na jambo hilo alilolifanya staa wao wanayempenda.

Sehemu ya maoni
“Kifo kipo kwa kila binadamu lakini hatutakiwi kukifikiria hivyo dada (Jide) unamkosea muumba wako.
“Wewe ni kioo changu, ila kwa hili kwa kweli sijalipenda.
“Jamani dada mbona unatutisha au haupo sawa leo?
“Wewe wajina umefikiria nini lakini?
“Kama umeshaona unakufa sema tujue.
***

“Duh! Dada fanya maombi hiyo ni roho ya umauti.
“Dada nini tena mbona unamkufuru Mungu? Hata kama una machungu kiasi gani, huwezi kufanya hivyo kwani ni mipango ya Mungu. Muombe akusamehe.
“Wewe Jide wewe huogopi lakini?

“Najua sote tupo njia hiyo lakini kwa nini leo umeamua kutuandikia hivyo? Naomba mipango ya shetani ishindwe!” ilisomeka sehemu ya maoni hayo iliyoungwa mkono na baadhi ya mashabiki wake waliojawa na simanzi.

Mchungaji amuunga mkono
Akizungumzia tukio hilo, mchungaji maarufu jijini Dar alisema kuwa, kila mtu anatakiwa kujiandaa kwa kuwa kila nafsi itaonja umauti hivyo ni vema kujiandaa kwa kutenda mema.“Maandalizi yanayopaswa kuwa makubwa ni ya kiroho kwa kuhakikisha unatenda mema ili kupata tiketi ya kwenda peponi na kukwepa adhabu ya Jehanamu,” alisema mchungaji huyo.

Kutoka Risasi Jumamosi
Kifo ni haki yetu lakini si vema kumchuria mtu au kujichuria kwa kuwa ni tukio lisilozoeleka katika maisha ya mwanadamu.

View attachment 1741210
Huyu si aliwahi kusema kuna siku alinusurika kujiua kwa msongo!? Nahisi hali imejirudia
 
Wanayajuaje maumivu wakati hawajawahi kufa?

Yote kwa yote ni njia lazima tuipite hata iwe vipi, kwa hiyo Jaydee kuchagua jeneza lake sioni tatizo, kuna wengine hukata sanda zao wanaishi nazo kwenye makabati/sanduku,
Kuna wengine huandika urithi,
Kuna wengine huchagua hadi nyimbo za kusindikizwa nazo wakifa,

Kujiandaa ni jambo muhimu sana sababu ile ndio safari yako ya mwisho na yenye ulazima.
Kwenye dini tunasoma habari za 'hari za Kifo' (mateso yenye maumivu makali)labda wamejulia huko
 
We nae... khaaa




Nikifa mazishi yangu nataka yawe ya mwaliko maalum – Lady Jaydee
Bongo5 EditorMarch 26, 2015 - 2:05 pm
Lady Jaydee haogopi kufa na infact anataka mazishi yake yawe na mwaliko kama vile harusi zilivyo.

page

Katika muendelezo wa post zake ‘controversial’ Lady Jaydee ameweka picha za majeneza mawili ya kifahari ambayo anapenda akifa azikwe.

11084796_1613949208837446_1981732043_n

Hata hivyo ana masharti – mazishi yatakuwa ya mialiko maalum na hatopenda mwili wake ufunuliwe.




“I’ve changed my mind Sitaki tena lile la purple Moja kati ya hayo hapo juu #MsiMind #KilaMtuAtakufa #Msiogope Nilikuwa nafikiria pia iwe invitees only #SitakiKufunuliwa,” ameandika
 
watu maarufu wanapitia mengi sana, huenda ashaambiwa hatoboa mwezi mwaka/mwezi fulani
 
Inatakiwa apatikane mtu wa kumliwaza JIDE ,inaonekana ana msongo wa mawazo sana,yule mnaijeria mwenye rasta alikuwa poa sasa sijui kitu gani kiliwagombanisha.
 
Back
Top Bottom