Lady Jaydee akiwa mahakamani leo...

Nikiwa kama Mshauri Mwandamizi wa Clouds Media Group kuanzia tangu ilipoanzishwa, wakati huo Joe Kussaga akiwa anachezesha disco lake pale Motel Agip, underground, na kuhamia kwingineko, kama TAZARA Hostel, nilishuhudia mengi mno. Hata siku Joe alipoondoka kwenda Marekani kuchukua vyombo vya Clouds FM, vikiwemo FM transmitter, booster na ecxiter, tulikuwa wote.

Nilimchukulia Joe kama rafiki yangu mpendwa. Hilo halijabadilika. Naijua vema familia yake. Mengi mabaya nimeyasikia juu ya Joe. Nimeyapuuzia. Joe na mke wake Juhayna ni watu wazuri wenye moyo wa upendo. Lakini kuna tatizo.

Familia hii imezungukwa na kila aina ya uadui kiasi cha kwamba inakuwa vigumu kujua nani rafiki na nani adui. Joe ana kasoro moja kubwa: He trusts the wrong people, watu ambao wamemgeuza mradi wa kujitajirisha wao kupitia mgongo wake. Lazima ieleweke kwamba Management Style ya CMG daima imekuwa ya family business, ambapo licha ya Joe kujaribu kuweka mazingira ya kitaaluma zaidi, imekuwa kana kwamba jitihada zake daima kugonga mwamba. Joe anao uwezo wa kuiuza CMG na kuhamia Zanzibar ambako amejiimarisha kibiashara, na wala hangepata hasara yoyote ile. Joe amezungukwa na kilq aina ya wazandiki na mandumilakuwili, ambao daima huuza siri zake kwa mahasimu zake wa kibiashara. Wakati anaposhtuka kuchezewa mchezo mbaya, a lot of damage has always been done.

Nilisoma maneno ya dada yangu Jaydee. Mimi daima namwita Judith, kwa Kiswahili, Yudithi. Hebu someni Biblia mjikumbushe kidogo Yudithi alikuwa mtu wa namna gani. Mnamwona Judith Wambura Mbibo ----- sana au ni kwa kuwa hana pesa? Dada yangu yule kajipanga, msimdharau. Mmesahau alikikata kichwa cha nani? Kasomeni wenyewe Biblia mpate kuelewa somo.

Joseph, au Yosefu, Mlinzi wa Kanisa Katoliki, mbona umekubali kujidhalilisha kwa kesi hii? Au huwatambui hao washauri wako kuwa mawakala wa Lucifer, ambao nia yao ni moja tu: Kuibomoa himaya yako na kuivunjilia mbali?

Yosefu, hebu fikiria for just one moment here. Suppose... Suppose... Suppose that no matter how much power or money you have, and you use it to your advantage and win the case, do you think that will be the start or the end of YOUR DEMISE?

Ndugu yangu, I beg you, please withdraw from this case. Wanaokushauri, wote, isipokuwa mkeo Inna anayekupenda kwa dhati, wote ni mawakala wa shetani. Ndio, wako baadhi ya ndugu zako ambao nawafahamu kama watu wacha Mungu, lakini wako wengine ambao ukiwanao mnacheka, mnakula, mnakunywa na kufurahi pamoja. Lakini hao ndio ukiwageuzia kisogo tu, wanaanza kukusema na kukusengenya na kukuzushia kila aina ya uzushi na uzandiki. Wahenga walisema: Kikulacho ki nguoni mwako. Kwani Yesu alisalitiwa na nani kama sio Yuda Iskarioti ambaye alifanya hivyo licha ya kwamba Yesu alimwambia mbele ya hadhira kwamba "Utanisaliti..."

Ndugu yangu, kama unadhani rushwa ilianzia juzi, unajidanganya.

Tazama. Nawaona. Hao. Wanakudanganya. Tutamhonga Hakimu pesa nyingi atautupilia mbali utetezi wa Jaydee.

Tazama. Namwona Hakimu. Mama. Ana familia. Ni mcha Mungu. Anaangalia upande wa kuume. Anawaona Malaika Walinzi wake. Wanaimba daima sifa za Mungu na kumkumbusha wajibu wake wa kutenda haki. Tazama. Ni usiku wa manane. Anaangalia makabrasha ya kesi yaliyo mbele yake. Anausoma kwa makini waraka usio na saini kutoka kwa washauri wako Joe. Unatoa ahadi lukuki za jinsi atakavyofaidika akiwa upande wako.

Tazama. Judith Wambura Mbibo. Yuko nyumbani na mume wake. Wamepiga magoti wakimwomba Yesu awasimamie katika kesi hii. Anamwambia Yesu kwamba ulikuwa ni wajibu wake kusema ukweli na wala si kukukashifu wewe. Anamwambia Yesu: Tazama mtu huyu. Nilijaribu kumfungua macho lakini yeye hakuzisoma hasira zangu kama hadhari kwake ili aanze kubadilika. Tazama jinsi shetani anavyomtesa. Hakika kwa dhambi hii ataangamia.

Kunakucha.

Sijui hakimu amechukua uamuzi gani. Sijui Yesu amechukua uamuzi gani. Lakini kwa vyovyote vile, ndugu yangu Joe, haki itatendeka.

Wanasheria wako wanaweza kupresent a very solid case in court, kiasi kwamba wanasheria wa Judith wakadhindwa, lakini that will be a VERY SMALL VICTORY compared to what you will lose in ALL your business empire that you have worked so hard to build, almost single-handedly?

Are you really prepared to go down this way? Do you know that you have declared war and that ALL the nation's tabloids will be actively digging into your private life? They will print truths and lies. Half truths and half lies. They will make you the source of their daily bread, now that you have opened Pandora's box.

We, who love you, but can do nothing to save you, because you cast us far and away, because you listened to wazandiki, ambao walituona sisi kuwa tishio kwao kwa kuwa tungewafichua undani wao. Tutasikitika na hatutakuwa na uwezo wa kukusaidia.

Ndugu yangu Joe. Nakuambia. Achana na hii kesi. Kwa mara ya mwisho. Achana nayo. Tangu lini maneno matupu yakavunja mfupa? Kwani wangapi wamesemwa, tena vibaya zaidi yako, lakini wameishi tena kishujaa.

Fikiria tena. Muda bado unao. Hebu ongea na Yesu, Yosefu.

PFM
 
hivi kukashifu uongozi ni kosa??mbn viongozi wa serikali wanakashifiwa na hawasemi lolote!!!iweje clouds wakasirike??me naona wanachuki binafc na jaydee na watashindwa!:disapointed:
 
Naungana na mtangulizi kumshauri Joseph kuachana na kesi hii
The issue at hand is trivial.Hatapoteza wala kupata chochote substancial kwa kuburuzana na dada yake mahakamani.Mwisho wa siku mnajichora kwa kusgadiddia trivial issues.You are a big man dont succumb to trivials.
 
prof J anaongea kwa vitendo katika kusupport lady jaydee!yeye hana maneno mengi wala vijembe katika mitandao ya kijamii!.....hii naita support ya kiutu uzima!big up prof jizze

nakupa big like kiongozi......huyo ndo the heavyweight Mc..... Kila binadamu ana mapungufu ila prof ni mfano wa kuigwa......ni miaka mingi sasa tumesikia watu wakimsema ila hautamsikia jamaa akijibu kwenye media.... Hii inamfanya jamaa awe tofauti na wengine.....naungana nawe kumpa big up...... Pamoja sana
 
Acheni dhiaka katika ili, wote tunajua kuwa Clouds Media Group inajitahidi sana kupambana na washika dau wakuu wa burudani ambao ni wasanii kwa nguvu zao za kifedha. Lady Jay Dee ameshawashinda kwenye show yake ambapo CMG walimsimamisha Mwana FA.

Siku zote duniani hakuna mbabe awe na fedha, madaraka, cheo na hata nguvu ya kijeshi hawezi kuonea wa tabaka la chini maisha yake yote kama hamjui tazameni mifano ya watu hawa Hitler, Saddam, Osama, Gadafi, Hosni Mubarak. Morsi, yule tajiri aliyemwagiwa tindikali na wengine wengi

Prof. Jay yuko karibu na Jide katika matatizo haya akiwa kama mkongwe wa bongofleva ili kumpa support ya kisaikolojia kwenye tatizo ili, pia kwa nyie mnaosema Prof kachakaa je wewe huko kama ulivyozaliwa? Binadamu tunabadilika kutokana na wakati na matatizo mbalimbali ya kimaisha kama maradhi, nyakati, uwezo n.k. Husitukane mamba kabla hujavuka mto.

Pole sana Jide na Gadna na hongera sana Prof. Jay kwa support unayotoa ni zaidi ya fedha ni utu uliotukuka. Salute
 
Briwn ad wahenga wanaema hujafa hujaumbika, wala usitukane mamba kabla hujavuka mto

Ninahakika kesho yako wewe huijui

na alivyochakaa ananitia shaka!!
 
Naungana na wale wote wanaoona haja ya kumaliza hili saga nje ya mahakama a.k.a suluhu muafaka.

Sikuunga mkono tangu pale Jide alipoanza haya malumbano na wala simuungi mkono sasa, lakini pia siungi mkono kuona clouds wanaendelea kuvutana na huyu bibie.

Inawezekana Jide alipata ushauri mbaya ambao sasa naona umehamia kwa clouds.

Ushujaa ni kuona mnazimaliza tofauti zenu kwa amani.

Pamoja na kuwa sikupendezwa na hatua alizochukua Jide wakati ule lakini bado haimaanishi kama siuamini pia uwezo wake kimuziki.

Na hata wakati nasikiliza kipindi cha top twenty clouds huwa najiuliza iwapo kama mashabiki wamechagua wimbo wa Jide, je hautoingizwa kwenye kinyanganyiro kwa kuwa tu Jide ana tofauti na clouds ?

Kama madhumuni ni kupata wimbo mkali, tofauti zenu zinatosha kuukosesha wimbo nafasi hata kama unakidhi haja ya wasikilizaji ?

Kama ni kweli shindano huendeshwa kwa matakwa ya wasikilizaji, ni nini nafasi ya wale wanaoukubali wimbo wa Jide ? au nao wanashirikishwa kwenye tafauti zenu ?

Hili ni hata kwa Dina wa leo tena na kipengele cha juzi, jana na leo, vipi kama atakayepiga simu atachagua nyimbo ya Jide, mtamwambia chagua nyimbo nyingine huyo tuna ugomvi nae ?

Napata ukakasi kudhani kama ni kweli matakwa ya wasikilizaji yanazingatiwa au ni "upangaji wa matokeo".

Kuunga mkono mwenendo wa aina hii inahitaji moyo mgumu kwa kweli.
 
na alivyochakaa ananitia shaka!!

Huna tofauti na wale ambao wanafuatwa na wazazi wao mjini, na kwa kuwa tu ni ofisa fulani, na baba amevaa suti ambayo haieleweki rangi yake kwa jinsi ilivyochakaa, na chini ametinga masendeu a.k.a katambuga basi unaamua KUMKANA .

kama sio kuitafuta laana ni nini ?

UTU hubaki kuwa UTU.
 

Legally speaking hii kesi ni non-starter, kwanza sijui tu ni "loya" gani alimshauri Joe kufungua kesi hii. Hivi wakili wake anaweza vipi kuthibitisha kuwa hayo maneno yaliandikwa na Judith? Kumbuka hiyo ni electronic media, ushahidi wa namna hiyo ni mgumu sana hapa Tanzania, hata kwa kesi za jinai ambapo ni categories fulani tu za ushahidi wa aina hiyo ndio unaopokelewa mahakamani. Technically Joe stands 60% to lose this case.

Ingekuwa bora yeye binafsi angemtafuta Judith wamalize hayo mambo nje ya mahakama. Tatizo jingine Judith anaonekana kuwa underdog hivyo public itakuwa na sympathu naye kuliko Joe "tajiri" tena "mwanaume". Hiyo ni reputational suicide. Unless tu kama anataka kumlipa Judith legal fees na kuumia kwa jina lake, Joe aendelee na kesi hii.
 
Wandugu,

Lazima mumelewe na kumsoma vizuri Binti Machozi. Hakuna mwanadamu aliyekamilika na kila mmoja wetu hufikia ukomo wake wa uvumilivu. Kutofautiana na kuelewana ni jambo la kibinadam pia. Muhimu tusivunjiane utu na heshima zetu.

Ninavyomfahamu Binti Machozi, na ninalisema hili kwa kujiamini, si kwa kubahatisha, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Wambura Mbibo alijitahidi kadri ya uwezo wake wote kumaliza tofauti zote na uongozi wa CMG. Lakini baada ya kukutana na nyodo, dharau na kibri, alisali na kumwomba Mungu amsamehe kwa hatua ambayo alikuwa amefikia, na hatua ambayo alikuwa ameifikia.

Kumwambia mtu kwamba nikifa usije kwenye maziko yangu, kuanzia leo usipige nyimbo zangu kwenye redio yako, pamoja na kutoonesha video zangu kwenye luninga yako, ni jambo zito na la kusikitisha.

Joe akaona amedhalilishwa, amekashifiwa, presha ikapanda. Mtu mkubwa na mzito kama yeye mwenye uwezo wa kumwona Rais wakati wowote akaona katusiwa na binti mdogo Jide. Wapambe nao wakatia neno, wakachochea kuni moto uwake vizuri, japokuwa kuni zilikuwa mbichi.

Akaitwa mwanasheria: Jide katutusi, tunakwenda mahakamani kumfundisha adabu. Fungua kesi.

Hiyo ilikuwa amri. Si ombi wala ushauri. Amri ya Bwana Mkubwa, Joseph Kussaga, a.k.a. The Big Boss.

Haya. Tungoje kuona na kusikia viroja vitakavyotokea kuhusu The Big Boss kwenye magazeti pendwa, a.k.a. ya udaku.

Joe hajui jinsi alivyojiharibia. Watakapoinasa hii hao wa udaku, watamchimba mpaka aione dunia chungu, akitamani dunia ipasuke na kummeza. Waandishi na wahariri wa magazeti haya wanamwona Jide kuwa kipenzi chao na shujaa wao kutokana na utunzi wake, msimamo wake na umahiri wake. Sijawahi kusikia wimbo hata mmoja wa Jide ambao hauna ujumbe. Hata mmoja. Wangapi hawaukumbuki ule wimbo wa Wanaume Kama Mabinti?

Jina hili, Judith au Yutithi, Joe litambue, ni jina kubwa. Ni usaliti tena mkubwa kwako wewe, Joseph au Yosefu Mlinzi wa Kanisa Katoliki, kukiasi cheo chako na kumwumiza mwamini mwenzako, ndugu yako, Yudithi.

Yesu alituasa tupendane kama yeye alivyolipenda Kanisa.

Je, ni wangapi kati yetu tunaofanya hivi kwa vitendo?

Narudia tena. Ndugu yangu, mdogo wangu Joe, PLEASE STOP THIS MADNESS! YOU ARE PLAYING WITH THE POWER OF GOD. SURELY YOU KNOW GOD DOESNT LIKE TO BE TRIED?

One way or another, utashindwa vibaya sana hii kesi. The burden of proof lies with you. You have to convince the Court, beyond reasonable doubt, that what you claim is true. In her counter-claim, Judith will present ALL, if not, most of what she claims to have done by you to sabotage her musical career.

When the Judge makes his/her decision, pray tell that you will be on the righteous' side. For if worse comes to worse, with one swift blow, with the Hand of God, literally bring down hellfire upon your empire leaving you to be just a mere piece of history.

What are the odds of you winning or losing this case? I dont know. But what I know that people like Judith are never to be messed with.

Please, before it's too late to turn around, drop this case like a hot potato. It will burn you.

You have nothing to lose, but you have much to gain: Your respect, your name and your public image.

In fact, IF I were you I would call a Press Conference tomorrow and annlunce that you are dropping the defamation case, and that you are asking Judith Wambura Mbibo to come down so that you may settle your differences.

Kugombana na kupatana, huo ndio uungwana.

Kila la heri Joe, lakini kwa hili la kesi, mimi kama kaka yako tangu enzi za "Oya Msela", sikuungi mkono!

Nafunga kauli yangu. Sitasema tena nawe, Joe.
 
Huyu anayejiita MwanaHaki ni mshambenga kama nini sijui. Bado kidogo watu watamvisha khanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…