Lady Jaydee akiwa mahakamani leo...

Lady Jaydee akiwa mahakamani leo...

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,786
Reaction score
5,963
JIDE.png

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.


Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
JIDE1.png

Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.


 
Na Prof J ni Mlinzi wake ama???
 
Duh! Kama ni hivyo basi hatareeee. Mlinzi ana kitambi cha kiti :A S-fire1:

We Majomba bado upo? Vipi Moboksi huko!

Ajuza amekomaa kwenye gemu kawatunishia misuli watoto wa magorofani. Hatareeeee kama vipi wajipange tena upya you know! Afu ni Mbebs wa ukweeeli unajua, si ajuza!

CC: Smile
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: LD
Waombane msamaha wayamalize kiutu uzima. ya nini kupotezeana muda bwana. JD hapo atang'ang'ana weeeee hadi aone kibao kimeandikwa NO WAY.
 
Ningetamani wanishtaki na mie kwa kuwauliza Clouds Group nini kiliwasukuma haraka sana "kununua" msiba na habari zote za msiba wa Ngwair? Kwa nini walikuwa wepesi kiasi kile kutafuta tiketi ya Miliard Ayo ili kuhakikisha anawahi kule na wao ndo wanakuwa chujio na pipe la habari zote kutoka RSA kuja Tz juu ya msiba, postmortem na usafirishaji wa maiti? Na mwisho "kazi au majukumu" yao yalimfanya nini Jide cha kumsababishia kushindwa kutimiza majukumu yake ya kijinsia?
 
Wabongo tuna matatizo sana na zarau za kipuuzi,sasa j anaweza akawa mlinzi???? Tuache tabia hizo.
 
Kuna watu humu wametumwa na Cloud media sijui kina Kussaga ni mabasha wao wamekomaa kutoa dhihaka kwa komando dhidi ya manyonyaji kina kusaga.
 
Back
Top Bottom