Lady Jaydee alivyowafunga midomo Mawingu

Mdakuzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,294
Reaction score
6,872
Na Kalunde Jamal
Onyesho la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo, maarufu Lady Jaydee, la kutimiza miaka 13 ndani ya tasnia ya muziki limekuwa la kipekee baada ya kuibuka Pedezyee aliyekuwa akimtunza fedha kama mtu aliyechanganyikiwa.
Lady Jaydee au kwa jina liguine Jide, Ijumaa ya wiki iliyopita alifanya onyesho kutimiza miaka 13 katika muziki, ambapo kulikuwa na burudani ya kukata na shoka.
Tukio la kuvutia katika onyesho hilo lilikuwa la Pedezyee huyo ambaye alikuwa na wapambe watatu ambapo alikuwa akipanda jukwaani huku ameshika kibunda cha fedha na kuanza kumtunza noti za shilingi elfu 10, moja baada nyingine hadi mpambe mmoja kati ya wale waliomzunguka atakapoamua kumtoa.
Alifanya hivyo mara mbili ambapo fedha iliyopatikana mara ya kwanza ukijumlisha na chache kutoka kwa mashabiki wengine Jide alimpa mama yake.
Pedezyee huyo hakuishia hapo kwani Jide alipopanda mara ya pili na kuimba kibao cha Yahaya ambacho kiliwachengua mashabiki vilivyo alipanda tena na kutunza elfu 10 moja moja zilizofika kama laki moja na alipotolewa na mpambe wake zilizobaki alimwagia mikononi mwanamama huyo ambaye anapotunzwa na yeye huzitupa chini na kufanya jukwaa lipambwe kwa wekundu wekundu au vijana wa mjini wanaziita noti hizo albino.
Onyesho hilo lilifanyika katika eneo la maegesho ya magari kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge, uliopo Kinondoni, Dar es Salaam, baada ya mamia ya washabiki kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu.

Hali ilivyokuwa!

Hadi kufikia saa 3:26 usiku, ukumbi ulikuwa tayari umejaa kiasi cha kukosa pa kupita wala kukaa, kitu kilichowalazimu mashabiki waliokuja kwa wingi kusimama na wengine kukaa katika mgahawa bila kujali kama wanaona vizuri au la.
Shoo ilianza Saa 4:32 usiku kwa muziki wa kizungu kama ufunguzi ambapo msanii kutoka katika bendi ya Machozi ambayo ipo chini ya Lady Jay Dee, Mayunga ndiye aliyeanza kuimba nyimbo hizo.
Ilipofika saa 5:7 usiku, Starehe ilishuhudia baadhi ya watu na magari wakirudia mlangoni kwa kukosa nafasi kutokana na ukumbi kufurika na kukosa hata nafasi ya kusimama. Licha ya kujaa watu kiasi hicho, bado hali ilikuwa nzuri na shoo ilikuwa ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake kumfanya kila aliyefika katika eneo hilo kupata alichokikusudia bila kumkera mwingine.
Irene Kinesi ni moja ya wanadada ambao wasanii waliomsindikiza Jide waanza kupanda jukwaani
Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo. Aliyekuwa wa kwanza kupanda kwenye jukwaa ni rapa wa kazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Mawingu wamemaindi sana

"To know the enemy is half the victory"
 
Hakika namkubali sana mwanadada huyu nguli wa muziki wa Bongo fleva...

Hongera sana dada Lady J Dee
 
Huyo mbona miaka mia kufikia level zake,hao bado sana,walie tu.mwaka huu..
 
Sasa Clouds wanamzibia riziki gani huyo mdada kama ameweza kukusanya idadi kubwa ya watu kwenye hicho kitamasha chake?

All that beef was nothing but a publicity stunt to generate interest in her newly released album and boost ticket sales for her mini-concert that she played on the parking lot of her business establishment.

In the music business it's very hard to maintain longevity, relevance, and yet still be on top. Not even Michael Jackson could do that. And 13 years in the industry is no joke. It's a lifetime. In that span many one hit wonders have come and gone. But somehow she's managed to hang around.

So, purportedly she's been on top of the game for some time but in recent years her status had started to peter out as more and more hungry upcoming artists were gunning for that top position.

The only way for her to find relevance again was to repackage her offering by creating a different persona, coming up with a new nickname of Anaconda (not sure about what the significance of that non-venomous serpent is), and last but not least employ just about every artist's favorite tactic when they are about to release a new album, i.e. start a beef with somebody who will garner you the much needed publicity that you are looking for.

Enter her beef with Clouds radio and it's top management brass. Look at the timing of it. Does any right minded person believe that timing to coincide with the release of her new album was an accident? I damn sure don't think so. It was very much by design. And of course, she had to play her position of the underdog going up against a leviathan in the showbiz.

That position assured her of public sympathy and support which she got. In the end, she made a killing and laughed all the way to the bank. Some of her ardent fans came out a bit light in the pocket thanks to the 50K cover charge for her mini-concert.

Clouds came out unscathed. I haven't seen, read, or heard anything about it losing any commercial ads due to that so called beef. If anything, I think it's listenership has increased though some folks won't readily admit that they do tune in to it religiously.

So there you have it ladies and gentleman, boys and girls. Just waiting to see what she'll do next. Waiting to see what else she got up her sleeve(s).
 

Umeandika sana Binchuchu... but what is it that hurts you most about this lady..!??
 
Umeandika sana Binchuchu... but what is it that hurts you most about this lady..!??

Why do you think I'm hurting?

Where do you see the hurt? Can you pinpoint exactly where it is in what I wrote?

Good grief! I'm just opining like everybody else is and what I wrote is rather innocuous if you'd read it without any preconceived notions. But I highly doubt you read it like that.

Now, is it the alternative viewpoint that I am expressing that is making you think I'm hurting? Au kwa kuandika sana ndo umeona kwamba naumia? Umekisoma na 'kukielewa' nilichoandika? Au unabwabwaja tu kwa vile umeona Bwa'Nchuchu kaandika hivyo lazima kiwe ni kibaya na anaumia sana? Unashangaza sana wewe.

I'm sorry dude, but that's a very parochial outlook you are holding. And I can also be just as parochial by asking you 'but what is it that hurts you most about Clouds that you relish so much every perceived bad news that has to do with them..!??

If you have a fertile brain, you will realize how asinine your question is. But I doubt you will because you are a birdbrain.
 
Bwanchuchu kubali MwanaFatuma kafunikwa mama Ngwear anasubiri ahadi ya MwanaFatuma.
 
Akili za wabunge wa CCM hizi
 
Jaydee dam dam na ccm ndo mana tamasha lake lilinoga a kujaa washabiki kutoka ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…