Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Na Kalunde Jamal
Onyesho la mwanamuziki Judith Wambura Mbibo, maarufu Lady Jaydee, la kutimiza miaka 13 ndani ya tasnia ya muziki limekuwa la kipekee baada ya kuibuka Pedezyee aliyekuwa akimtunza fedha kama mtu aliyechanganyikiwa.
Lady Jaydee au kwa jina liguine Jide, Ijumaa ya wiki iliyopita alifanya onyesho kutimiza miaka 13 katika muziki, ambapo kulikuwa na burudani ya kukata na shoka.
Tukio la kuvutia katika onyesho hilo lilikuwa la Pedezyee huyo ambaye alikuwa na wapambe watatu ambapo alikuwa akipanda jukwaani huku ameshika kibunda cha fedha na kuanza kumtunza noti za shilingi elfu 10, moja baada nyingine hadi mpambe mmoja kati ya wale waliomzunguka atakapoamua kumtoa.
Alifanya hivyo mara mbili ambapo fedha iliyopatikana mara ya kwanza ukijumlisha na chache kutoka kwa mashabiki wengine Jide alimpa mama yake.
Pedezyee huyo hakuishia hapo kwani Jide alipopanda mara ya pili na kuimba kibao cha Yahaya ambacho kiliwachengua mashabiki vilivyo alipanda tena na kutunza elfu 10 moja moja zilizofika kama laki moja na alipotolewa na mpambe wake zilizobaki alimwagia mikononi mwanamama huyo ambaye anapotunzwa na yeye huzitupa chini na kufanya jukwaa lipambwe kwa wekundu wekundu au vijana wa mjini wanaziita noti hizo albino.
Onyesho hilo lilifanyika katika eneo la maegesho ya magari kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge, uliopo Kinondoni, Dar es Salaam, baada ya mamia ya washabiki kujitokeza kiasi cha kujaza eneo hilo, hadi kupishana ikawa taabu.
Hali ilivyokuwa!
Hadi kufikia saa 3:26 usiku, ukumbi ulikuwa tayari umejaa kiasi cha kukosa pa kupita wala kukaa, kitu kilichowalazimu mashabiki waliokuja kwa wingi kusimama na wengine kukaa katika mgahawa bila kujali kama wanaona vizuri au la.
Shoo ilianza Saa 4:32 usiku kwa muziki wa kizungu kama ufunguzi ambapo msanii kutoka katika bendi ya Machozi ambayo ipo chini ya Lady Jay Dee, Mayunga ndiye aliyeanza kuimba nyimbo hizo.
Ilipofika saa 5:7 usiku, Starehe ilishuhudia baadhi ya watu na magari wakirudia mlangoni kwa kukosa nafasi kutokana na ukumbi kufurika na kukosa hata nafasi ya kusimama. Licha ya kujaa watu kiasi hicho, bado hali ilikuwa nzuri na shoo ilikuwa ya kistaarabu, yenye mashamsham ya aina yake kumfanya kila aliyefika katika eneo hilo kupata alichokikusudia bila kumkera mwingine.
Irene Kinesi ni moja ya wanadada ambao wasanii waliomsindikiza Jide waanza kupanda jukwaani
Wasanii nguli wa Hip hop waliomsindikiza Jadyee katika shoo hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi Sugu, Joseph Haule na Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi nao walifanya mambo mazuri jukwaani kiasi cha kuiongezea utamu shoo hiyo. Aliyekuwa wa kwanza kupanda kwenye jukwaa ni rapa wa kazi kutoka Ukonga, baadaye bendi ya M ikiongozwa na Grace Matata kwa shoo za utangulizi.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi