Lady Jaydee ashiriki kwenye wimbo rasmi wa Kombe la Dunia

Lady Jaydee ashiriki kwenye wimbo rasmi wa Kombe la Dunia

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Msanii mkongwe wa muziki nchini Judith Mbimbo maarufu kama Lady Jaydee ameshiriki kuimba wimbo maalum wa kombe la dunia 2014 akishirikiana na David Correy na rapper wa Kenya, Octopizzo

Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.

Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza wiki hii jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
 
At least she is representing us kwa kuimba since our national team we do fail to qualify...big up jay dee
 
Acha uongo jaydee atabaki kuimba umbea na kumuimba mumewe... jlo na pitbul ndo wameimba wimbo wa kombe la dunia
 
Acha uongo jaydee atabaki kuimba umbea na kumuimba mumewe... jlo na pitbul ndo wameimba wimbo wa kombe la dunia

Sio kwamba Jide ataimba wakat wa uzinduz hapana ila yy ataimba kuipromote bidhaa ya cocacola ambayo ni mdhamin wa kombe la dunia yeye pamoja na hao wenzake
 
najiuliza hivi huo wimbo utapigwa kweli kile kituo cha redio chenye bif na jide?
 
Acha uongo jaydee atabaki kuimba umbea na kumuimba mumewe... jlo na pitbul ndo wameimba wimbo wa kombe la dunia

Shakira aliimba wimbo wa kombe la dunia Waka waka
Lakini K'naan pia aliimba wimbo wa kombe la dunia Waving Flag kwa kupitia Coca Cola.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Komandoo.....!jiepushe tu na siasa mbichi
 
Back
Top Bottom