Lady Jaydee: Mashabiki wa mikoani hamuoneshi ushirikiano ndiyo maana mikoa mingine siji kufanya show

Lady Jaydee: Mashabiki wa mikoani hamuoneshi ushirikiano ndiyo maana mikoa mingine siji kufanya show

Mwambieni akafanye show nigeria.
Akija huku mkoani tutamkojoza
 
Jdee siku hizi kavurugwa kama si kuvurugika.sijui ni nini kinampata huyu mwanadada,anazeeka vibaya kuanzia akili hadi matendo.
 
Mbona kaongea poa tu mdadaz

Commando hayumbishwi na mtuu
 
Huyu dada siku hizi keshakwisha kabisa. Shwain!!!
 
Watu wa mikoani malalamiko yenu nimeyasikia ila na mimi nina ya kwangu pia naomba myasikilize kwa umakini ili tuweze kwenda Sawa .
——————————————————————————————————————————————————————
Ukitoa Mwanza, Dodoma , Arusha , Geita na Mtwara kidogo muitikio wenu huwa unakuwa mdogo sana kwenye shows hii inakatisha tamaa kuwatembelea ——————————————————————————————————————————————————————
Pili mna kasumba ya kusema hamuamini kama msanii amefika hadi apitishwe kwenye PA awapungie mkono kama mbunge anaomba kura jimboni |
Radio zipo, TV zipo na simu mnazo za mkononi hiyo ni njia nzuri ya kutumia pamoja na vipeperushi|
Binafsi mambo ya kupita na kupunga mkono siyapendi hata kidogo na nikiitwa na promoter kitu cha kwanza namwambia hakikisha umefanya matangazo watu wameelewa otherwise sitaki mambo ya PA ——————————————————————————————————————————————————————
Hizi ni Zama za PA kweli jama ??
Na kisingizio huwa flani alitangazwa anakuja hakuja
Binadamu wote si Sawa, na tusihukumiwe kwa makosa ya watu wengine ambayo hayatuhusu
——————————————————————————————————————————————————————
Tatu , wengi wakifika mlangoni wanaomba kupunguziwa bei ya kiingilio [emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Mtu anapoandaa shughuli ya kuwaburudisha mjue ameshapiga mahesabu kajua amegharamia kiasi gani na anataka gharama zake zirudi na apate faida pia , na nyie pia hapo hapo awape burudani |
Tujitahidi kuwa waelewa na kwenda na wakati ili kuepusha kero ndogo ndogo pamoja na malalamishi |
Ndio mwisho wa siku unajikuta mtu unarudi mikoa ile ile ambayo watu wanajitokeza na kuelewa |
Asanteni kwa mapenzi mema |
Ila Dodoma nitarudi very soon , sijui mmeniloga ‍♀️‍♀️ Ila pia huwa nafata Nyomi [emoji3][emoji3][emoji3]
——————————————————————————————————————————————————————
Halafu katika wasanii ambao hawabagui crowd ni mimi, maana JayDee ni wa watu wote wale Classy wa Serena na hata masela wangu vilevile.
Kwahiyo hajatengwa mtu wala nini |
Sehemu nilizowahi kupita nyie ni mashahidi kuwa nishafika hadi vijijini mwenu na kulala sehemu yoyote ile bila kujitia u star |
Mimi ni mtu humble sana , ila tu nina misimamo yangu pia .
dbe074c5175feb8d770f7b97b8608646.jpg
Kwani yy haishi ndani ya mkoa o ule c mkoa?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mashabiki wa mkoani ni pasua kichwa haswaaaa pamoja na wehu wake ila Jide kawaambia ukweli maana mpaka leo wanataka msanii abembee kwenye gari la PA mchana kutwa na kisa kuwaaminisha kua yupo na bado wataenda kujaa hotel aliyofikia wakiwa na picha zake wanamfananisha kwanza alafu mlangoni wanaomba wapunguziwe.
Piga show zako Serena mama wakiuza korosho,chai,kahawa lazima watakuja Dar kushangaa hapo ndipo wanalipa bila utata maana tunawashika mkono waje kusafisha macho.
 
shoo zenyewe mnaimbia kwenye CD pumzi ikikata mnasikika mnaimba wawili wawili. nani aje!?
 
Usije tena mikoani,umeshachuja kwanza.Tutasikiliza miziki ya CD Bar na kwenya mahoteli,tumeshazoea kwa sasa.
 
Jide namuheshimu sana lakini amekosea. Yeye alipaswa kitafuta namna ya kuendesha shows zake huko kwa washabiki zake. Kusema mapungufu ya mashabiki inamuharibia tu.
 
Back
Top Bottom