Mi nadhani tatizo kubwa ilikuwa ni strategies tu manaake kama ni collabo wapo wasanii walianza collabo mapema ila hazikuleta matokeo chanya.
Kwa mfano AY sio kwamba alianza collabo yake kubwa US moja kwa moja hapana. Kama una kumbukumbu mkuu kati ya mwaka 2007~08 alifanya collabo na P~Square ngoma ilikuwa inaitwa 'Fresh' by that time p~Square ndio walikuwa on fire na walikuwa wamefanikiwa kuliteka soko la Africa vizuri.
So kikubwa nadhani ilikuwa ni mpango mkakati lakini pia tusi~under rate nguvu ya social networks. Collabo ya AY na Sean Kingston wa US ni ya juzi sana mwaka 2012 au 2013 kama sijakosea lakini pia tukumbuke wasanii kama akina Juma Nature, Jide, Babuu (Inspector), akina Solo Thang et al hawakufanikiwa kutusua sababu kubwa pia ikiwa ni wadau wa muziki kuwanyonya.
Wasanii kwa mfano walifanya kazi kubwa na nzuri infact nyingi zenye kuelimisha ila waliokuwa wanajiita ma~promoter waliwanyonya sana wasanii na kuwakatisha tamaa baadhi ya wasanii wenyewe.
Lakini pia sumu kubwa iliyowadumaza wasanii wetu wengi nadhani ni ulimbukeni na kuiga starehe za kijinga baada ya kufanikiwa kupata vijisenti vyao kidogo. Kwa mfano baada ya msanii kutoa hit song akapata pesa badala ya kujipanga kuendelea kutoa ngoma juu ya ngoma wengi walikimbilia starehe, anasa na kuishia kuwa mateja.
Angalia watu kama akina Ferooz album ya yake ya safari na hit songs kama boss, au starehe zilimfanya akapiga hela ndefu hadi kufikia kupewa zawadi ya gari (jeep) lakini badala ya kujipanga na ku~focus kwenye kuwekeza kwenye muziki starehe zikamponza akapotea, akina Q chillah, Chiddy Benz, Daz Baba akina T.I.D, Ray C etc etc wote walikimbilia unga hadi wengine tumewapoteza na vipaji vyao akina Langa na Ngwair (R.I.P) to them.
Kimsingi nadhani kikubwa walifanya mziki usiokuwa na mkakati endelevu.
Tuanze na hilo la collabo ya AY na P Square. Kwenye post yangu moja nimetumia msisitizo maneno "KUSHIRIKISHWA" na sio "KUSHIRIKISHA".
Kwavile muziki wetu ulikuwa haujavuka mipaka; KUWASHIRIKISHA watu kama P-Square au 2Face ilikuwa ni kujifurahisha tu ingawaje wao walikuwa TOP in Africa. Ukiwashirikisha; wimbo unakuwa ni wako mwenyewe na sio wa P-Square. Na kv ni wako mwenyewe, P-Square au 2Face hawataipigania ngoma yako ichezwe kule kwao unless kuwe na makubaliano ya pembeni! Na kama mwenyewe hauna connection na media za nje basi ngoma yako itaishia kupigwa East Africa kama nyimbo zingine kwavile ndio ngome yako ingawaje umemshirikisha msanii mkubwa! Ni kutokana na hilo ndio maana collabo za aina hiyo huwa hazifanyi vizuri nje!
Kinyume chake, UKISHIRIKISHWA, tunafahamu ngoma ni ya yule aliyekushirikisha! So, kama ni Mnigeria; it's obvious ngoma itaenda kupigwa Nigeria. Na kama ulishirikishwa na wakali kama P-Square; ina maana sauti yako ita-trend sana pande hizo!
Tukirudi kwa Diamond, pamoja na yote vile vile alikuwa na zari moja! Collabo ya kwanza kabisa nje ya EA, ikafanya vizuri na kuzoa Channel O.
Zile Channel O hazikumvimbisha kichwa na badala yake kwake alizichukulia ni exposure. Akaanza kufanya collabo kwa fujo huku pia akishirikishwa kwa fujo. Ikawa akienda Coke Studio; yeye ni collabo.
Hii ikamfanya hata wale ambao hawakuipenda Number One Remix na Davido, si ajabu wakaja kuangukia kwenye Nanaa na Flavor, au Coco Baby na Yemi, au Bum bum na Iyanya, au Love Boat na kcee; n.k.
Kwahiyo ilikuwa ni ngumu sana kwa Wanaija kutomsikia Diamond kwa sababu alikuwa amekaba kila kona!
Kinyume chake; wakati bado artist ni Unknown, muziki wenu unknown; kwa mazingira kama hayo ni ngumu sana kutoboa na ngoma moja hususani kama umeshirikisha na sio kushirikishwa!
Hayo masuala ya kunyonywa, mapromota n.k yanaingia sana kwenye suala la maslahi na sio kuutoa muziki nje ya EA. Hata US; wasanii wananyonywa sana na ndio maana baada ya kushituka wakaanza kuanzisha label zao na makampuni makubwa yakitaka kufanya kazi na wao; inakuwa ni mkataba kati ya kampuni kubwa na label na sio kampuni na msanii! Lakini pamoja na yote hayo; hiyo haikuwahi kuwazuia kutusua nje ya US!
Social networks; sipuuzi mchango wake lakini tusisahau hata hao Wanaija waliokuwa wanatisha Africa yote enzi hizo; na wao hawakuwa na social networks lakini hiyo haikuwazuia muziki wao kuchezwa kila kona ya Africa. In short, level of playground ipo the same. Zaman sote hatukuwa na social networks na hivi sasa sote tunazo social networks na kwahiyo system inabaki in equilibrium.