Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Afaanalek! Ashakum kwikwikwi
Anacheeka!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Afaanalek! Ashakum kwikwikwi
Anacheeka!
we Mphamvu mbona matusi ndio zako!! ShamelessKinakuuma nini bibie? Kutiwa atiwe mwenzio, kiuno ukatike wewe... Inahuu?
we Mphamvu mbona matusi ndio zako!! Shameless
Lafudhi yako ndo ilonfanya nncheke mkuu! Cheichei mkuu.
Nimemueleza stable woman (ingawa nina shaka na hiyo stability yake) hapo juu kuwa asiwe na shaka na lafudhi yangu na awage na amani tu.
Heheeee ! Haya mkuu, kuhusu stability yake huenda jina la kitabu lasadifu yaliyomo. Atakua stable haswaa si umeona lafudhi yake kwenye neno la mwisho mi sikumuelewa alitaka kusema nini. Hivi ni shameless eenh?Nimemueleza stable woman (ingawa nina shaka na hiyo stability yake) hapo juu kuwa asiwe na shaka na lafudhi yangu na awage na amani tu.
Heheeee ! Haya mkuu, kuhusu stability yake huenda jina la kitabu lasadifu yaliyomo. Atakua stable haswaa si umeona lafudhi yake kwenye neno la mwisho mi sikumuelewa alitaka kusema nini. Hivi ni shameless eenh?
Abeeee! Kwikwikwi......Ajitiatia.......Mi si mtaalamu sana lakini nadhani shameless halina mantiki kwa jinsi alivyolitumia.
Stability wapi dada, kashindwa kuvumilia lafudhi yangu vingine ataviweza kweli? Kuhusu maneno wanayotumia mi mwenyewe sielewi, naona wanajitiatia tu...
Kitaaluma tungesema hivi:
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.
Kwa hiyo hapa chanzo kikubwa cha lafudhi ni mazingira alimo huyo mtumiaji lugha, mazingira hayo ni kama yalivyotajwa hapo juu. Lugha mama pia inaweza kuwa chanzo cha lafudhi tofautitofauti, kwa mfano katika kiswahili, hawa watu wakizungumza wazungumzaji wa kiswahili watajua wanatoka mkoa gani au ni kabila gani:
Lafudhi sio kitu kibaya, lakini pia huweza kubadilika kwa kutambua au bila kutambua (hii inaweza kutokea hadi umri wa miaka ishirini na). Lakini chanzo kikubwa cha lafudhi ni mzaingira alimo huyo mzungumzaji.
- Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa
- Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili
- Ukikaa nchale, ukichimama nchale
- Wewe unakamuaga mangombe tu moja kwa moja
- Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu!
umechambua vizuri mkuu...ila kwa maono na maarifa kidogo ya lugha. Lafudhi kwa kiasi kikubwa husababishwa na lugha mama, mazingira ni kidogo sana kutokana na sababu za maingiliano. Mchango wa lugha mama katika lafudhi hauna shaka kabisa kwa mtamkaji wa lafudh fulan.
Ila kwa upande mwengne mazingira hufanya mtu kutekwa na kubadilishwa kutoka lafudh yake ya kwanza hadi mpya kutokana na wenyeji wake.
Kwa mfano mim ni mluguru labda, alafu nimezaliwa tanga mathalani sina ninachojua katika kikaguru, kwa bahat mbaya huku nilikozaliwa wazazi wang hawaongei kilugha chochote zaidi ya kiswahili. Unakuta nawakuta watu na lafudhi zao zenye athari za lugha mama lakin mim nitakuwa kati ya mswahili na lafudhi ile husika.