Laini za Simu Milioni 1.9 zisizo na Usajili Rasmi kuzimwa leo Februari 13, 2023

Nipe muongozo, mimi nimesajaliwa na mtu namba ya nida nilikua sijapata. Sasa ninayo, je Naweza kuihakiki kwa kutumia namba yangu au mpaka aliyenisjalia??
Kwa kutumia yako haiwezekani mpaka aliyekusajilia ,njia rahisi na uhakika zaidi ni kumuomba akutumie namba yake ya Nida maana hiyo inakuwa kama ufunguo kwenye kuhakiki au yeye mwenyewe anaweza kuihakiki kea kuthibitisha kuwa anaitambua namba yako asipo iconfrim namba yako itakuwa kama ya tapeli na kufungiwa..
 
Halotel wamebahatishaje sijui kua na hata hawa Milion 8 halafu hatuwekagi hata hela kwenye laini zao maana mtandao wao ni kinyonga style
 
Bora wewe… mie walintumia saa 9 usiku… niliifuta tu kwa kicheko
 
Sidhani kama watazima maana kuna pesa nyingi sana hapo kwenye 1.9mil.

Kampuni za simu wana mkono mrefu kuliko huyo tcra na kodi inayolipwa ni kubwa plus miamala ya siku kutokana na hizo 1.9mil.
Zitakuwa ni line ambazo hazitumiki
Kwa mfano unakuta mtu anadaiwa songesha elfu 50 anaamua kuachana na hiyo line
 
Mtunza funguo amesafiri hivyo wataongeza muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…