Laini za Simu zilizosajiliwa nchini zafikia Milioni 80.7, Vodacom yaongoza kwa Wateja, TTCL na Airtel zashuka

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
MAWASILIANO: Takwimu za Mawasiliano ya Huduma za Simu kwa Robo Mwaka (Juni - Septemba 2024) zinaonesha kulikuwa na ongezeko la Laini 4,137,981 za Mawasiliano ya Mtu kwa Mtu (P2P) na Laini Milioni 1.02 za Mawasiliano ya Mashine (M2M) hivyo kuwa na jumla ya Laini Milioni 80.7.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Mtandao wa tiGO uliongeza usajili wa Laini 1,940,468 ukifuatiwa na Haloteli Laini 1,249,745, Vodacom ilisajili Laini 1,047,768, Airtel ilipoteza Wateja 15,159, na TTCL ilipoteza Wateja 64,607.

Aidha Mtandao wa Vodacom umeendelea kuongoza kwa kuwa na laini nyingi zaidi nchini ikiwa na Laini 24,136,856, tiGo 23,458,325, Airtel 19,492,734, Halotel 10,971,582 na TTCL 1,586,724.

 
Matapeli wamesajili line ngapi?
 
Line nyingi tu ni kwa ajili ya "ile hela tuma kwenye namba ...."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…