Barua ya wazi kwa kingereza mnaitaje?
Ok,Ridhiwan kikwete najua pesa ni zako na wala hatukupangii matumizi lakini tusikilize kwa sikio la tatu sisi wapenzi wa soka.
Imekua ni TABIA sio TZ tu hata uko duniani matajiri wengi ununua au kuwekeza kwenye Team za mpira na timu izo sio haba uwa zinafanya vizuri sana..Matajiri haswa wa Mafuta hupendelea kuwekeza kwenye timu za mpira wa miguu
Mfano:
~PSG
~Newcastle utd
~Manchester City
Ni baadhi ya timu kubwa duniani zinazomilikiwa na wachimba mafuta(Waarabu) Na sio haba zinafanya vizuri sana kwenye ligi zao
Turudi huku bongo pia matajiri wengi wamewekeza kwenye mpira kama MO dewji,Azam,GSM na Silent Ocean ambao wanamiliki au wamewekeza kwenye Soka.Ushindani wa timu hasa mapacha wa k/koo umekuwa common mpaka unakinai sasa..
Kuna kipindi Azam ilileta upinzani kwenye ligi na ikachukua ubingwa ila nae miaka ya hivi karibuni ni kama ametundika daruga!!
Kupitia Team utayoanzisha natumai italeta Upinzani kwenye ligi yetu na itaongeza ushindani ili tusiwakweze sana hawa ((Mapacha wa kkoo))
Japo na wewe ni shabiki kindaki wa timu moja wapo kwenye hao mapacha wa kkoo..ikishindikanaa[emoji117] (ONGEA NA MSHUA--IZZO BIZNEZ)
Wako mtiifu KENGE mmoja
Nawasilisha