Laki 5 ni mtaji kwenye kilimo, ufugaji au uvuvi?

Laki 5 ni mtaji kwenye kilimo, ufugaji au uvuvi?

fite fite

Senior Member
Joined
Feb 27, 2017
Posts
113
Reaction score
94
Habari JF members.

Maisha ni watu na watu ni maisha, mawazo chanya 20 sio sawa na mawazo chanya 3. Ukweli unauma lakini ni tiba.

kwa mazingira ya Tanzania Kuna mtu akipata laki tano kwake ni sawa na kupata million 500.

Yaani kuna watu wana mazingira magumu kimaisha tofauti na tunavyodhania na kuwachukulia sema wengi ni nadhifu Sana hata ukimuona huwezi amini kuwa Hana hata 2000 mfukoni.

Kuna watu wakipata 1000 hiyo ni bajeti ya mlo wa siku. Sasa inapotokea anapata laki 5 kwake ni sawa na million 500.

Naomba tuambizane ukweli.

Laki 5 ni mtaji kwenye kilimo, ufugaji au uvuvi?

Tunaomba mchanganuo ni kilimo gani, ufugaji gani au uvuvi upi ambao kwa hiyo laki 5 unaweza kuikuza na kuizalisha zaidi.

Nimeandika hivi kwa Sababu Jana nikiwa safarini mkoani Tabora. Kuna kijana aliniomba ushauri kwenye hili akitaja kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kutokana na kutokuwa na uzoefu kwenye hii nyanja nimeona kushare nanyi ili tuweze kumsaidia kama sio yeye na wengine zaidi.

Ahsanteni.
 
Kama yupo serious aje nimpe connection ya uvuvi kwa hiyo pesa yake, nadhani hatajutia.
 
Back
Top Bottom