Lakini DPP tulikushauri ufute hii kesi ya Mbowe haina uhalisia wowote

Mimi kama Wakili mkongwe ndani na nje ya nchi kwakweli sijawahi kushudia kesi yenye vituko na mikamganyiko mingi kama hii inayomkabili Mwenyekiti
Usikivu wa kenge ni hadi pale ubongo utakavyochungulia nje ya fuvu la kichwa chake🏃.
 
Kesi hii isifutwe ili CCM na Serikali yake dhalim izidi kuwekwa uchi ili iwe fundisho Kwa wote
 
Wanaweza kuwa wanazo akili lakini zimeshikiliwa na mtu au kikundi cha watu wengine bila wao kujua au wanajua. Tuzidi kumuomba Mungu mwenye haki ,kama mbowe na kundi lake walikusudia kuyatenda maovu haya basi wapate malipo yao kwa haki ile wasitahilio. Lakini kama ni mashitaka ya uongo kama waluvyoshtakiwa wakina Petro basi haki ya Mungu isimame upande wao. Hilo tu.
 
Kituko cha leo shahidi wa jamuhuri amefumaniwa na desa kizimbani aliloandikiwa na mawakili wa jamuhuri kwasababu ameshindwa kukariri ushahidi wa uongo aliofundishwa.
 
Unaamini kuna ushahidi?
 
Shahidi anakwenda wa nusu Sasa, na ushahidi haunyooki zaidi ya aibu na kudhalilisha mahakama kwa kuishirikisha kwenye siasa chafu! Uza ubongo huo boss maana unakaa nao kwa hasara.
 
Hawana akili
 
kituko cha leo shahidi wa jamuhuri amefumaniwa na desa kizimbani aliloandikiwa na mawakili wa jamuhuri kwasababu ameshindwa kukariri ushahidi wa uongo aliofundishwa.
My friend, amini usiamini hiyo sio kweli. kwenye izo mishe, shahidi ukimfundisha lazima ataboronga tu kwenye cross examination. ambacho huwa kinafanyika kwa hao jamaa ni kumkumbusha tu yale aliyoongea polisi as per his witness statement n.k, ila ukimfundisha mambo mapya anawez akupigwa swali la ajabu akakosa nafasi ya kuja kwako kuuliza jibu kwasababu taayari yupo kizimbani, na ataharibu kesi yote, hivyo ilo jambo huwa halifanyiki, labda kama hakuan wakili wa utetezi. nimekuwepo huko kwenye prosecution zamani, kuna siku utakuja kuelewa, ila sio leo.
 
Mpe huu kama ushauri wa mwisho, asipoelewa basi kaamua kufa na tie shingoni
 
Kama walivyong'ang'ana na kesi ya rugemalira hadi wakaamua kunyoosha mikono au walivyong'ang'ana na kesi ya mhasibu wa takukuru nayo wamenyoosha mikono
 
Kama walivyong'ang'ana na kesi ya rugemalira hadi wakaamua kunyoosha mikono au walivyong'ang'ana na kesi ya mhasibu wa takukuru nayo wamenyoosha mikono
Tofautisha awamu ile na awamu ya samia. ukifanikiwa hilo utakuja kunishukuru.
 
Wacha chadema waendelee kujifariji.
 
Shahidi kafumaniwa na desa kizimbani waliongeleaje hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…