Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #41
Ruta,Hilo nalo neno...unanifanya nishtuke ukirejea home nianze kunusa nusa isjekua unanitupia vijembe bibi jinga mali yako inaliwa mie nimelala tuu.
Shombo zingine zina harufu kali acha tu.
RUTA ,wewe mswahili safi ,labda alifanya kwa dhamira ,kwan nan asiye jua kuwa shombo n MAKRUKH, akaona nataka nijuilikane kama leo nimechoea maneno ya huku kwetu kisiwani
loh hii shombo unamletea nani?
Mmmmmmh ngereja akirudisha umeme nitarudi.....
Mkuu salute! Nimeipenda sana post yako,nimekugongea ka like ila natumia tochi
Shombo ni hili.... na wanaonusishwa ni hawa
Napita kimya kimya
Na wale wanaovaa vya kuazima,halafu wanajitapa kwenye mashughuli..
Ujumbe mzito sana huu
wanaojisahau na kurudi na shombo majumbani wafunguke tusikia miziki yao kwa wale wanaowaringishi hizo shombo!
Ama kweli kuna Waswahili JF!
Pilau ale yeye tena kwa kificho huku akjijua ni mwizi tu.............akiwa kwenye chumba alichokishindilia komeo tena la viro ili asije kubambwa na mwenye mlo wake.............baada ya uporaji wa pilau ya watu aja mtaani na huanza kutubehulia.........na kuacha mafuta ya pilau na vipunjepunje vyake mdomoni.......
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Mwingine ametoka kumtafuna kuku wa watu khalafu kwa kasi ya ajabu hurukia kitandani kwa mkewe na kumshulizia manukato yatokanayo na siagi ya samli aliyopikiwa kuku wa watu aliyemtafuna ............kwa kufanya hivyo ni mithali ya kumtambia mkewe ya kuwa amejinoma kuku wa watu..........lakini swali ni
Hivi, hiyo shombo amletea nani?
Kwa nini asiende bafuni akaoga na kutakata na abakie akichekwa na dhamira yake badala ya kuwaadhibu waliokuwamo na wasio kuwamo..........kama ile hadithi ya panya aliyekusudiwa kuuawa na mtego lakini mtego ukamnasa nyoka ambaye mwenye nyumba aliposikia umenasa akawahi kummalizia panya gizani na matokeo yake akaumwa na nyoka mwenye hasira na kufa hapohapo.........matangani ng'ombe na kuku walichinjwa kumsindikiza mwendazake............na hivyo kukamilisha maono ya panya ya kuwa mtego ulomlenga yeye wataingia waliomo na wasiokuwamo........
Hivi walakini...........hiyo shombo amletea nani?
Mkuu, hii lugha ya Makwaya wa kuhenga sijaielewa asee.., would you pliiiiz elaborate?:doh:
Kweli kabisa ruta mwanga nyuki tupa mawe
umeharibu kunilinganisha na Makwaia...................lugha nzito yenye manjari kama hii ataitoa wapi..................you have to be me to do it the way I do it............