Land cruiser ya utalii

baba nanihii

Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
69
Reaction score
116
Habari za mihangaiko wana jamvi nimejikusanya nimenunua land cruiser hard top sasa nataka niigeuze itumike kwenye kazi za utalii sasa sijui wapi wanafanya maboresho ili iwe ndefu kidogo kama zile zinazo onekana Arusha na kwa anayefahamu bei itakua msaada zaidi. Natanguliza shukrani.
 
Njoo arusha kuna kampuni inafanya hizo kazi za kutengeneza mabody kwa jina maarufu warbus hiyo kampuni inaitwa hanspaul ipo njiro na wamepewa kibali cha kufanya hizo na kampuni ya toyota
 
Hongera sana, Nenda Moshi kuna vijana wanafanya kwa bei nzuri sana otherwise Rajinder Motors Moshi ndo kazi zao ila wako juu
 
Yaan wewe wa ajabu kwel kweli kwann ulinunua bila kuwa na malengo sahh. Huko tunakuita kukurupuka sasa fanya hv niuzie 7m ukanunue bajaj inatosha kwa utaliii hahahahahahaha kweli mjin mipango.
 
Moshi na Arusha wanarekebisha ila andaa million kumi plus
 
Hanspaul mechanics arusha wanatengeneza na kuuza haya mabodi hadi ulaya wapo Arusha njiro
 
Yaan wewe wa ajabu kwel kweli kwann ulinunua bila kuwa na malengo sahh. Huko tunakuita kukurupuka sasa fanya hv niuzie 7m ukanunue bajaj inatosha kwa utaliii hahahahahahaha kweli mjin mipango.
Acha dharau, kaomba msaada, either umsaidie kama huna msaada kwa kimywa.

Tujifunze ustaatabu. Na sio kila uzi uchangie
 
Hanspaul ndo suluhisho lako mkuu, kule kwetu land cruiser dili sana
 
Njoo arusha kuna kampuni inafanya hizo kazi za kutengeneza mabody kwa jina maarufu warbus hiyo kampuni inaitwa hanspaul ipo njiro na wamepewa kibali cha kufanya hizo na kampuni ya toyota
Arusha na Moshi wanafanya hiyo kazi..Kampuni zinazojulikana sana ni Rajinder Motors (Moshi) Na Hanspaul(Arusha) Hizo kampuni bei zao ziko juu sana....kuna makampuni madogomadogo ambazo bei zao ziko chini kidogo....ila andaa sio chini ya mill 12
 
Yaan wewe wa ajabu kwel kweli kwann ulinunua bila kuwa na malengo sahh. Huko tunakuita kukurupuka sasa fanya hv niuzie 7m ukanunue bajaj inatosha kwa utaliii hahahahahahaha kweli mjin mipango.
Sijakurupuka na sio kila kitu kitaenda sawa na mipango yako
by the way mjanja naye ni mshamba pia
 
Asante ndugu zangu kwa maelekezo yenu
Mkuu ulinunua Land cruiser Pick Up ama hiii iliyofunikwa?

Maana warbus nzuri zinaanzia kwenye Land cruiser/Land Rover /Nissan Pick Ups!

Other wise Nenda Rajinder Moshi au Hanspaul Arusha.

Jaribu hao vijana wa Moshi as well
 
Ni hardtop next week ntaenda Moshi kwaajili ya kuifanyia maboresho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…