Land Rover Festive Arusha 2024

Land Rover Festive Arusha 2024

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
(VIDEO ipo chini)
IMG_7590.jpeg

Tamasha la Land Rover 2024 ni tukio la kipekee linalofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, katika viwanja vya Magereza Grounds, Kisongo, jijini Arusha. Tamasha hili litafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi Oktoba 14, 2024, na limeandaliwa na Mhe. Paul Makonda, likilenga kuwakutanisha wamiliki, wapenzi, na mashabiki wa magari ya Land Rover.

Lengo kuu la tamasha ni kuadhimisha historia na uwezo wa magari ya Land Rover, hasa katika matumizi yake kwenye mazingira magumu na safari za umbali mrefu. Pia, moja ya lengo muhimu ya Tamasha hili ni kuvunja rekodi ya Guinness World Record iliyowekwa na Ujerumani kwa kuwa na msafara mkubwa zaidi wa magari ya Land Rover. Rekodi ya sasa ilivunjwa huko Bavaria, Ujerumani mnamo Agosti 2018, ambapo magari 632 ya Land Rover yalishiriki kwenye msafara huo. Hii ilikuwa ni hatua kubwa ambayo iliwekwa katika kumbukumbu za Guinness kama msafara mkubwa zaidi wa magari ya aina moja.​
IMG_7587.jpeg

Kwahiyo mwaka huu Arusha Tanzania chini ya Mh. Makonda wamepanga kuvunja rekodi hii kwa kuwaleta pamoja wamiliki na mashabiki wa Land Rover kutoka ndani na nje ya nchi, ili kushiriki katika tukio hili la kihistoria. Tamasha hili, lina lengo la kuwa na parade ya magari zaidi ya 1000 ili kuipiku rekodi ya Japan na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kupitia tukio hili kubwa. Miongoni mwa shughuli zitakazojumuishwa ni:​
  1. Safari ya Arusha National Park, ambapo washiriki (hapa inaelezwa ni magari 300 kati ya yale 1000+) watajaribu magari ya katika hali halisi ya safari za porini na kuweka rekodi nyingine ya kuwa hifafhi ya wanyama pori ya Arusha itakua hifadhi ya kwanza duniani kuingiza magari ya aina moja kwa wingi zaidi na kwa wakati mmoja.​
  2. Maonyesho ya kibiashara, yanayowapa nafasi wazalishaji wa magari na vifaa vya magari kuonyesha bidhaa zao mpya kwa hadhira pana.​
  3. Burudani na michezo ya kifamilia, kwa ajili ya kuvutia washiriki wa rika zote na kutoa burudani kwa familia nzima.​
IMG_7605.jpeg

Tamasha hili linatarajiwa kuvutia watu kutoka sehemu mbalimbali, likiwa ni fursa ya kipekee kwa kampuni za magari, wataalamu wa magari, na wafanyabiashara kukutana na kujadili fursa mbalimbali za kibiashara. Mbali na hayo, tamasha hili litakuwa na faida nyingi kwa taifa kwa ujumla kama vile:​
  • Kuchochea Utalii: Arusha ni moja ya miji maarufu kwa utalii nchini Tanzania, na tamasha hili litaleta wageni kutoka sehemu mbalimbali, wakiwemo watalii wa ndani na nje. Hii itasaidia kukuza sekta ya utalii, kuongeza idadi ya watalii wanaoitembelea Tanzania, na kuingiza mapato kupitia matumizi ya hoteli, migahawa, na huduma za utalii.​
  • Kukuza Biashara ya Magari: Tamasha hili litatoa fursa kwa wafanyabiashara wa magari na vipuri kuonyesha bidhaa na huduma zao kwa wateja wapya. Hii si tu itasaidia kukuza mauzo, bali pia itaongeza uwezekano wa ubunifu na ushirikiano mpya katika sekta ya magari. Zaidi, itavutia makampuni ya kimataifa kuwekeza katika soko la Tanzania.​
  • Ajira na Fursa za Kibiashara: Maandalizi na uendeshaji wa tamasha kama hili huhitaji nguvu kazi kubwa, ikiwemo usimamizi wa shughuli, uuzaji wa bidhaa, usafiri, na usalama. Hii inamaanisha kuwa kutakuwa na ajira za muda kwa wakazi wa Arusha na maeneo jirani. Pia, biashara ndogo na za kati zitapata fursa za kuuza bidhaa na huduma zao kwa washiriki wa tamasha.​
  • Kukuza Uwekezaji wa Kimataifa: Washiriki kutoka nchi mbalimbali watapata fursa ya kuona mazingira ya biashara ya Tanzania. Hii inaweza kuvutia wawekezaji wa kimataifa kuwekeza katika sekta ya magari, utalii, na huduma nyingine zinazohusiana, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi.​
  • Kuchangia Pato la Taifa: Kwa ongezeko la biashara, usafirishaji, na huduma zitakazotolewa wakati wa tamasha, taifa litanufaika kupitia kodi na ada mbalimbali, hivyo kuongeza mapato ya serikali. Matukio makubwa kama haya yanasaidia kuongeza pato la taifa kupitia shughuli za kiuchumi zinazozalishwa wakati wa tukio.​
IMG_7599.jpeg

Kwa ujumla, tamasha hili si tu linawapa fursa wapenzi wa magari ya Land Rover kujumuika, bali pia lina faida kubwa kwa uchumi wa Tanzania, sekta ya utalii, biashara, na uwekezaji

Mbali na hayo, tamasha hili limeibua hisia tofauti miongoni mwa watu, huku wengine wakilipongeza na wengine wakionyesha wasiwasi kuhusu athari zake kwa uchumi na biashara za ndani. Pamoja na faida nyingi zilizoainishwa, kuna maoni kutoka kwa wadau wengine kama vile MamaSamia2025 aliyeelezea mtazamo wake kuwa tamasha hili linawapa faida kubwa zaidi wamiliki wa chapa ya Land Rover badala ya Taifa.

Mdau huyu anahoji kwamba, licha ya tamasha hili kuvutia, Watanzania bado wanafanya kazi bila malipo ya moja kwa moja katika mazingira ya ubepari, ambapo kila kitu kinapaswa kuwa na malipo. Kwa mtazamo wake, anasema kuwa tamasha hili linaonekana ni kama jitihada za kutumia rasilimali za ndani, hasa fedha na muda, kuwafanyia matangazo ya bure TATA Motors, kampuni inayomiliki Land Rover. Anataja kuwa gharama zilizotumika na washiriki wa tamasha hili, kama vile mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Arusha, zinawafaidisha zaidi wamiliki wa chapa hiyo kuliko washiriki wenyewe.

Wasiwasi wake unahusu ukweli kwamba tamasha linaweza kuwa ni sehemu ya matangazo ya Land Rover bila Watanzania kupata faida ya moja kwa moja ya kifedha kutoka kwa kampuni hiyo. Mdau huyu anashauri kwamba ingekuwa bora kama tamasha hili lingeandaliwa na Land Rover yenyewe, badala ya kuonekana kama jitihada za binafsi za kuwafanyia matangazo ya bure kampuni hiyo kubwa. Soma uzi wake hapa.

Kwa upande mwingine, wadau wengine ikiwemo Mpasuaji wa Manesi alijibu hoja hizi kwa kutoa ufafanuzi wa malengo halisi ya tamasha.

Yeye ameeleza kuwa lengo kuu la tamasha hili ni kuvunja rekodi ya Guinness kwa kuwa na msafara mkubwa zaidi wa magari ya Land Rover duniani hivyo Tanzania inatarajia kuvunja rekodi hiyo na kuweka historia mpya. Hii ndio sababu kuu ya tamasha, na ndio maana taratibu zote, kuanzia umbali wa magari kwenye msafara hadi uchukuaji wa picha, zinafuata masharti ya Guinness World Records. Hata helikopta itahusika katika uchukuaji wa picha ili kuhakikisha kila kitu kinazingatiwa kwa mujibu wa vigezo vya rekodi ya dunia.
IMG_7595.jpeg

Pia, mdau huyu anaangazia faida za kibiashara ambazo zitapatikana kwa jamii inayozunguka tamasha hili. Anaeleza kuwa tamasha hili litawanufaisha wafanyabiashara wengi, kuanzia wale wanaoleta wanyama pori, wauza nyama choma, watalii, hadi wamiliki wa nyumba za wageni. Sekta kama usafirishaji (bodaboda n.k), wauza vipuri vya magari, na wauza vinywaji wote watapata fursa ya kuuza bidhaa na huduma zao kwa washiriki wa tamasha hilo. Zaidi ya hayo, tamasha litatangaza jiji la Arusha kimataifa, kuongeza idadi ya watalii, na kuwapa fursa media houses kupata maudhui ambayo yatawapa kipato kupitia views za mtandaoni.

Pia anasema kuwa, tamasha hili ni fursa kubwa ya kujenga connection za kibiashara, kwani wamiliki wengi wa magari ya Land Rover ni watu wenye uwezo mzuri kiuchumi. Hivyo, washiriki wa tamasha hili watapata nafasi ya kujenga mitandao mipya ya kibiashara, jambo ambalo haliwezi kupimwa kwa fedha moja kwa moja. Soma reply yake hapa.

Ingawa maoni haya yanatofautiana, ni wazi kwamba Tamasha la Land Rover 2024 lina faida kubwa kwa taifa kama litaendeshwa vizuri. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata manufaa ya moja kwa moja kutoka kwenye matukio haya, hasa katika kuhakikisha kuwa wanafaidika kifedha badala ya kufanya kazi za bure kwa makampuni makubwa.


View: https://www.youtube.com/live/D2mWLyd17wc?si=VBZohWIBYRhpsd1u
==============================​

DAY 2
Leo ikiwa ni siku ya pili ya tamasha la Land Rover Festival Arusha, Zaidi ya magari 300 aina ya Land Rover yameanza safari kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Arusha jijini Arusha. Lengo kuu la safari hii ni kuvunja rekodi ya dunia kwa kuwa na idadi kubwa ya magari ya aina moja yaliyoingia kwa pamoja kwenye hifadhi ya wanyamapori.
IMG_7622.jpeg


Katika siku ya kwanza ya tamasha hili, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, alitangaza kwa umma kuwa Arusha imeweka rekodi mpya ya kimataifa. Msafara wa magari 1034 ya Land Rover uliandaliwa, na hivyo kuvunja rekodi ya awali iliyowekwa na Ujerumani miaka sita iliyopita ya magari 632.
IMG_7621.jpeg
 
Watangazaji wa TBC wanaotangaza Live watangazaji wenu wanapotosha wanaita Landrover Parade badala ya Landrover Festival jina rasmi watoeni au wakanyeni

Huwezi kwenda kutangaza event ya mtu ana jina Rasmi halafu wewe utunge lako
 
Naona kama imetengeneza unnecessary traffic jam hapa Arusha, weekend wengine tunaitumia kufanya mishemishe zetu zaidi ya ajira, sasa leo ni mwendo wa bodaboda au kutembea kwa miguu kitu ambacho kimekuwa kero.
 
Sio Festival, ni parade.
Festival huwa ni tamasha la kiutamaduni mahususi kwa jamii fulani na huwa linafanywa kila msimu, pia Festival hainzishwi na mtu mmoja tu kama parade
Kwa uelewa wangu. Festival ni tukio au sherehe inayofanyika kwa sababu maalum, kama vile sherehe za kidini, tamaduni, au matukio mengine ya kijamii. Mara nyingi, festival hujumuisha shughuli kama vile muziki, ngoma, sanaa, chakula, na michezo, na huwa ni fursa kwa watu kujumuika na kusherehekea mambo ya pamoja katika jamii zao. Festivals zinaweza kuwa za kitaifa au za eneo fulani, na zinasaidia katika kuimarisha utamaduni na mila za jamii husika. Na kama umeshawah kufika Arusha, utakubaliana na mimi kwamba inawezekana Arusha ukawa unaongoza kwa watu wanaopenda Land rover (ni kama utamaduni wa wenyeji wa Arusha)​
 
Back
Top Bottom