1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Hadi keshokutwa bado najiuliza kitu gani kinafanya watu wamuone K anafaa kuwa namba 1?
Ni mzuri kwenye kuongea huku amekaza uso, ila hana mikakati ya kiuongozi,
Nikumbushe,ni jambo gani amelisamia ipasavyo na likaleta matokeo chanya toka awe msimamizi..!
Hii nchi inahitaji ama kutawaliwa na Jeshi kamili au Mtu mwenye ujasiri wa kuwa tayari kwa lolote hata kufa alimradi atetee rasilimali na fedha za umma.
Vinginevyo pawe na katiba mpya yenye utawala wa Kiraia unaotokana na umma kwa ajili ya umma .
Katiba iliyopo ni ya kijeshi iliyovikwa vazi la Kiraia chini ya Watu wachache ndani ya CCM .
Kwa sasa tunachaguliwa viongozi watakaolinda mali za dhulima walizo nazo watawala kwenye mifumo yote.
Kuanzia majaji ,wakuu wa vyombo vya usalama , Wastaafu na waliopo kwenye madaraka ya juu . Wote ukiangalia muda wao wa utumishi ni miaka isiyozidi kumi ndani ya nyazifa zao za juu . Lakini wanautajiri wa kutisha na bado wanatumia dola kushinikiza utawala wanaoutaka wao.
Ni kakundi kadogo sana kwa watu. Lakini kana Jesuri kubwa sana kwa sababu ya kuegemea majeshi kuwatisha wananchi.
Sasa tujiulize ni vipi Raia ambaye anaihofia nafisi yake kwa kiwaogopa wezi wa mali za umma na vinaraka wa wazungu akawa Mzalendo.
Kwa Katiba hii ni Bora mwanajeshi awe mtawala mana ni Mzalendo ambaye yupo Tayari kuifia nchi yake. Hawa Raia wanatumia majeshi kutawala lakini wanalinda nafsi zao na mali zao huku wananchi na hata wanaowalinda wakiwa na maisha duni sana.
Kasimu Majaliwa ana uthubutu wa Kukemea wala Rushwa lakini wengine ni wanalinda Nafsi zao. Hata Yule Naibu wake hana Authority ya kukemea Rushwa . Na anajua kuwa hana. Na anajua kwa nini hana na ananua watu tunajua hana.
Ndani ya CCM kwa sasa ni Kasimu na Makonda . Mwingine ambaye wamemdhibiti kihuni ni Polepole.
Vinginevyo tutaenda na Lisu ili waovu wasitamalaki na kujimilikisha hii nchi.
Makampuni yote ya Wageni kama wahindi,waarabu na Wachina yanafanikiwa kutokana na mipango mizuri lakini na usimamizi mzuri wa kuwadhibiti wazi.
Kasimu ana uwezo wa kusimamia mipango ya serikali ambayo ni mizuri tangu Mwalimu Nyerere lakini inakosa wazalendo wa kuisimamia.
Tanganyika imeuzwa kwa wageni wachache wakishirikiana na Watu wachche waliojivika ngozi ya utawala wa kidemokrasia chini ya Katiba ya Kijeshi na Kidikteta .
Katiba iliyopo ikipata kiongozi mzalendo tunapata maendeleo ya haraka sana .
Lakini katiba iliyopo ikipata Mtawala Mbinafsi na Fisadi atachukua mali zote za nchi na kujilimbikizia mali yeye na marafiki zake chini ya mwavuli wa uwekezaji. Kifupi tukizubaa hii nchi itagawanywa bipande vipande kama Kongo kwa sababu ndiyo nchi iliyobaki yenye amani na Rasilimali nyingi amabazo zinaishia mikononi mwa Wachche kwa kasi sana huku Pakiwa na kundi dogo la machawa ,mashoga ,wasagaji , wezi na wauza madawa na magendo wakiwa wanaishi maisha ya anasa na kufurahia kwa dhihaka na ulaghai kazi njema sana ya uumbaji wa Mungu kwa Nchi ya Tanganyika.
Wahuni na wafuasi wao tutawakataa 2025 kwa namna yoyote.