Lango la Kiroho la July 1 na uhusiano wake katika Ulimwengu wa Giza

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Tarehe 1 Julai inawakilisha lango kuu la kiroho la katikati ya mwaka (Mid-Year Portal) linalogawa kalenda katika pande mbili sawa.

Katika mifumo ya kiroho, tarehe hii si siku ya kawaida, bali ni majira ya mpito ambapo milango ya kiroho hufunguka ili kuruhusu mabadiliko ya kiutawala, tathmini ya nusu mwaka iliyopita, na kuweka misingi ya miezi sita ijayo.Katika ulimwengu wa giza, lango hili hutumika kama msimu mkuu wa kufanya tathmini ya uharibifu uliofanyika tangu Januari na kupanga mikakati mipya.

Nguvu za giza hutumia muda huu kutengeneza vizuizi vya kiroho ili kuzuia mafanikio, afya, na ustawi wa watu usikamilike katika nusu ya pili ya mwaka.

Vilevile, mawakala wa ulimwengu wa giza hutumia siku hii kufanya matambiko na kufanya upya maagano ya siri (Renewing Covenants).

Kupitia madhabahu zao, wao huongeza nguvu kwenye laana za kifamilia, magonjwa, au mikosi ili vitu hivyo viendelee kutawala na kufuatilia hatima za watu hadi mwezi Desemba.

Kwa upande wa kiuchumi, kwa kuwa miezi sita ya mwisho ndiyo kipindi ambacho watu hukimbizana kukamilisha malengo yao, ulimwengu wa giza hupandikiza roho za uharibifu.

Hii hupelekea baadhi ya watu kukabiliwa na changamoto za ghafla kama kufilisika, kupoteza kazi, au mivurugano ya kibiashara inayolenga kufuta mafanikio yote yaliyopatikana mwanzoni mwa mwaka.

Ili kushinda hila hizi, unashauriwa kusimama kidete kiimani kupitia maombi ya mamlaka na kufunga (saumu) ili kukomboa wakati na miezi iliyobaki.
Huu ni wakati wa kuvunja kila agano lisilo la kimungu na kuharibu madhabahu zote za giza zilizopangwa kukuzuia usivuke salama kwenda kwenye hatua inayofuata.

Nimalizie kwa kusema.. lango hili linakutaka usiwe mnyamazaji, bali uweke sauti ya ushindi juu ya maisha yako kwa kutamka maneno chanya ya baraka, amani, na ulinzi.

Ukifanya hivyo, unakuwa umeiteka miezi sita ijayo na kuilazimisha ikuzalie matunda mema badala ya mabaya yaliyopangwa na ulimwengu wa giza.
 
Asante kwa elimu nzuri
Tamka maneno haya pamoja nami
Mwezi huu wa Julai, ninatamka baraka na mafanikio makubwa katika kila kazi ya mikono yangu, nikiamini kuwa milango mipya ya fursa inafunguka na kila ninachokigusa kinaenda kusitawi na kuzaa matunda mengi.

Ninapokea amani ya kweli inayotawala akili na moyo wangu, nikitembea kwa utulivu na kuona suluhisho la kila changamoto bila hofu yoyote kuniyumbisha.

Kila hatua yangu inalindwa ninapoingia na ninapotoka, niko salama mwezi huu wote, na hakuna mabaya yatakayonikaribia mimi pamoja na familia yangu.

Julai hii itakuwa ya kicheko, ushindi, na salama tele!πŸ’–πŸ’–
 
Haya mambo wengi ndo tunaanza kuyaelewa kwako broo, Shukran sana .
 
AMINA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…