Lango la kuzimu Selander Bridge

Lango la kuzimu Selander Bridge

Corluka Neven

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Posts
317
Reaction score
358
LANGO LA KUZIMU SALENDA BRIDGE

Udhibiti juu ya utajiri, majini, uhai na kifo

Hii ni uhalisia na sio story na uwe unafanya uchunguzi maana si kila kitu cha kubisha. Ukiwa ujui kitu kuna watu watapewa neema ya kujua ili wakuambie wewe. Lango za kuzimu ni shimo au nyufa isiyoonekana kwa macho ya kawaida.

Daraja lolote kwa asili ni ishara ya mawasiliano na muungano , iwe kati ya mbingu na dunia au maeneo mawili tofauti. Je, unafahamu kuna mlango wa bahari na daraja huko mjini linaloitwa salenda bridge.

Lilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1929 na imepewa jina la John Einar Selander, Mkurugenzi wa Kwanza wa Kazi za Umma Tanganyika.

Wanaoenda mjini au wakazi wengi wa dar es salaam wanapajua vizuri sana hapo. Tunaona madaraja katika nchi yetu yako mengi lakini kila daraja likiwa na sifa yake kama madaraja ya mito mfano wami, lufiji nk.
Lakini leo tunaangalia daraja la mlango bahari Salenda bridge.

DAIMA KUNA ZAIDI YA KILE USICHOONA KWA MACHO YA KAWAIDA
Je, ni matukio gani ya siri pale salenda bridge tazama katika juma siku ya jumanne saa 9 usiku mfalme wa pepo au (samaeli) na asmodeus anashika mlango hayo kutoka daraja la tanzanite hadi salenda upande wa kaskazini. Huu muda wa uharibifu na kifo katika lango hilo, nguvu hiyo usafiri popote kukusanya roho na kuleta katika lango lake kuu kwaiyo si vyema kutembea muda huu hata kama ukukusudiwa.

Pale pale salenda siku za tar 31 october full moon katika sherehe za halloween siku ambayo katika mwaka mzima panzia la lango la kuzimu linakuwa jembamba sana kuliko full moon ya miezi mingine (watu wengi wanaojua siri hizi ufanya ibada za hades na Miungu mingine).

Ibada nyingi huenda na siku mfano Mwaka 2023 tar 31 ilidondokea juma 4 siku ya visasi na vita na hii ndio siku ya samael ila saa tisa usiku asmodeus anakuwa katika malango hayo kwaiyo nguvu hizi hutumwa kwa visasi na vita. Kwaiyo full moon ya mwaka jana 31 October ilikuwa mbaya zaidi lakini wengine wakifurahia kuwakomesha watesi wao.

Ya mwaka huu inadondokea Alhamisi siku ya heshima na utajiri saa 7 usiku jua linapotawala jupita au saa nane usiku venus na jupita zinapoambatana hii ni upendo na utajiri na heshima, kwaiyo siku kama hii saa 7 na 8 usiku watu utumia fursa ya mlango hasa pale salenda bridge kuomba roho na majini.

Madhabahu mengi ya majini yako masaki na kidogo Osterbay lakini ikiwa lango kuu ni salenda sasa tafakari watu wanaoishi masaki na hali yao ya kiwadhifa, lakini hii inatokana na kuwa karibu na nguvu ya bahari kutumia milango iyo vizuri. Ni kuna mengi sana pale salenda yanayofanyika japo sisi tunashindwa kuzingatia na kufanya chunguzi mbali mbali.

Nitakutolea yote yaliyofichwa chini uone asili na Mungu alivyo wa ajabu sana. GIZA au USIKU sio muda wa kulala ni muda wa kujitafuta na kutafakari ulimwengu huu na kujua siri muhimu za maisha. Jaribu kuwa unapita sehemu iyo mida ya usiku kwa saa maalumu utaona utofauti wa hali.

Wale wanaoongozwa na roho husisimka sana. Kwa nini kuna malango mengi lakini salenda ni kuu hapa D.S.M? Lakin kumbukai sio kila lango bahari ni mlango wa kuzimu ila kila bahari ina nguvu kiroho.

Hata sehem nyingi za bahari,mito,mapango kuna njia za kuzimu ila nini kikubwa zaidi pale salenda? Kutoka daraja la tanzanite hadi salenda ni lango pia na pale kuna kina kirefu ila lango lake limetokana na nguvu kubwa ya salenda bridge pamoja kwamba salenda ni daraja dogo kwa tanzanite bridge.

Maajabu ya maji yake, majini, ibada za toka enzi na enzi, mizimu pamoja Mikoko na miti mbali mbali iliyopo pale na chanzo kikuu cha huo mlango. Kubwa kuliko kutawaliwa na mkuu wa pepo pamoja na mfalme wa kuzimu.

Tunaweza kutumia asili kwa mema au ubaya. Kuona malango na visivyoonekana na katika giza kali vaa jicho la paka katika pete ya silver kwa ibada maalumu.
 
Screenshot_20231111-201809.png
 
Salander bridge pana codes number za kufungua mlango wa baharini ukitaka kwenda ulimwengu wa nje au kuonana na malkia wa pwani.
Mlango ufunguka automatic kama wewe ni member.
Kama si member utaishia kuona miti ya mikoko tu.
Dar ina milango mingi ya kuingia outer worlds
 
Salander bridge pana codes number za kufungua mlango wa baharini ukitaka kwenda ulimwengu wa nje au kuonana na malkia wa pwani.
Mlango ufunguka automatic kama wewe ni member.
Kama si member utaishia kuona miti ya mikoko tu.
Dar ina milango mingi ya kuingia outer worlds
BS.
 
Linaitwa daraja la John Sealander aliyekuwa waziri wa ujenzi kwenye serikali ya mkoloni.
Lilijengwa mwaka 1954.
 
Back
Top Bottom