DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Baada ya kuhitimu masomo yake ya kidato cha sita mwaka 2013 katika shule ya sekondari ya wasichana Kilakala, Jojina alirudi nyumbani kwao Gairo. Jirani yao Mzee Mkude alikuwa amefungua duka la vifaa vya maofisini na shuleni (stationery) karibu na stendi ya zamani. Hivyo Jojina alimuomba Mzee Mkude awe anamsaidia kwenye duka lake kipindi chote cha yeye akisubiria matokeo yake na aweze kujifunza kutumia kompyuta. Jojina akaanza kazi pale dukani na huku akijifunza kompyuta, mwalimu wake alikuwa dada mmoja ambaye ndiye aliyekuwa ameajiriwa kuisimamia ile steshenari.
Jojina alikuwa na malengo ya kufika chuo kikuu, hivyo katika vitu ambavyo aliweka kama mikakati ni kujifunza kompyuta na kuijua sawasawa. Kwa hiyo alizingatia sana masomo yake, hata yalipotoka matokeo yake na kujiridhisha kwamba alifaulu vizuri alikuwa tayari ameshaweza kuitumia kompyuta vizuri sana hasa micro soft word programu ambayo alikuwa akiitumia sana muda wote akifanya kazi pale steshenari.
Alifanikiwa kuomba nafasi ya kujiunga na chuo kikuu, akapata nafasi chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kusomea masomo ya ualimu. Ingawa ualimu ulikua ni chaguo lake la mwisho lakini akachaguliwa kusoma kozi hiyo. Kwa kuwa kidato cha sita alifaulu kwa daraja la kwanza, Jojina aliamini angeweza kuwa mwalimu mahiri sana. Wazazi wake walimuandaa na kumsafirisha kwenda kuanza masomo yake Dodoma. Kipindi yupo pale steshenari, Jojina alikuwa anapewa fedha kidogo kwa ajili ya kujikimu kwa mahitaji madogo madogo. Na alipomaliza muda wake wa kazi Mzee Mkude akampa kiasi kidogo cha fedha ili kiweze kumsaidia kwenye masomo yake ya chuo. Kwa kuwa alikuwa na malengo ya kufika chuo kikuu Jojina alikuwa anazitunza zile fedha ili akipata kiasi cha kutosha na yeye anunue kompyuta ya wake.
Chuoni Dodoma, alipangiwa kuishi chumba kimoja pamoja na wanadada wawili (Amina na Herieti) na mama mmoja mtu mzima mwalimu wa sekondari shule ya sekondari Katoro huko Kagera Madam Rweyemamu aliyekuwa anajiendeleza. Hawa wote hawakuwa na ujuzi wa matumizi ya kompyuta zaidi ya Jojina. Ingawa mwaka wa kwanza walisoma somo la kompyuta lakini hata hivyo hawakuweza kuwa mahiri. Baada ya miezi miwili ya maisha chuo Jojina alinunua laptop iliyotumika (used) aina ya Dell Latitude D610 kwa kijana mmoja anaitwa Masanja aliyekuwa anaishi Morogoro mjini, yeye alihitimu masomo yake mwaka huo chuo cha kiislamu Morogoro. Hivyo laptop yake akamuuzia Jojina kwa kiasi cha shilingi laki tatu na elfu hamsini tu. Hizi ni fedha ambazo Jojina alizitoa kwenye akiba yake aliyekuwa ameihifadhi muda wote wa yeye kufanya kazi pale Gairo kwenye steshenari ya Mzee Mkude.
Fedha ya mkopo ya kujikimu (Boom) ilivyoingizwa kwa wanafunzi Jojina akawa na fedha ya kutosha kwani alipata mkopo wa asilimia 90, hivyo akatoa kiasi cha shilingi laki mbili na elfu hamsini akanunua printer aina ya HP LaserJet P1102, aliiagizia kutoka Dar-es-Salaam. Laptop na printer vilimsaidia kuchapa kazi zake za darasani hivyo kupunguza gharama za stationeries. Lakini pia akawa anafanya ujasiriamali wa kuchapa kazi za wenzake kwa siri kwa sababu uongozi wa chuo ulikataza wanafunzi kufanya biashara kwenye mabweni yao. Rafiki zake waliokuwa wanajua Jojina ana printa na anatoa huduma ya kuchapa hawakusita kumletea. Kwa kuwa Jojina alikuwa mahiri sana katika uchapaji, alipata umaarufu sana kwa muda mfupi na kwa kazi ile ilimuongezea kipato sana. Hata hivyo hilo halikumzuia yeye kusoma kwa bidii.
Fedha kidogo alizokuwa anazipata kwenye shuguli yake ya uchapaji alikuwa anaihifadhi na sehemu ndogo sana alikuwa anaitumia kwa ajilii ya matumizi yake ya ziada.
Mwaka 2016 Jojina alihitimu masomo yake ya shahada ya kwanza ya ualimu na kutunukiwa cheti. Wakati anamaliza masomo akaunti yake ilikua na kiasi cha kutosha, hivyo aliporudi nyumbani kwao Gairo, akatafuta eneo zuri la yeye kufanya shuguli zake. Akapata fremu moja mkabala na sheli ya Shabibi akafungua duka lake la vifaa vya shuleni na maofisini. Fedha zake hazikuweza kununua vifaa vyote vinavyohitajika dukani, hivyo alianza na vifaa vichache muhimu na baadhi ya bidhaa ndogo ndogo. Baada ya wa miezi sita mbele duka lake lilianza kuongezeka kidogo kidogo, akapata kijana mmoja wa kike aitwae Atwiya akawa anamsaidia pale dukani akawa anamfundisha kompyuta pia.
Mbali na duka lake la steshenari, Jojina alianzisha tusheni (kituo cha masomo ya ziada) nyumbani kwao. Hivyo jioni alikuwa anarudi nyumbani kufundisha wanafunzi na pale dukani anamuacha yule binti. Mwaka 2017 hakupata nafasi ya kazi za Serikali, hata ilipofika mwaka 2018 hali ikawa ni hiyo kwani ajira za Serikali kwa wakati huo zilikuwa chache sana. Hata hivyo Jojina hakuweza kuyumba kwani tayari alikuwa na sehemu iliyokuwa inampatia mia mbili mia mbili.
Mwanzoni mwa mwaka 2019 kwenye kile kituo chake cha tusheni akaanzisha nursery isiyo rasmi, akapata vijana waliohitimu kidato cha sita na kidato cha nne akawaweka wakawa wanafundishwa watoto yeye akiwa kama mfuatiliaji na mkurugenzi wa masomo.
Hivi ninavyosema Jojina ana mpango wa kufungua shule ya nursery rasmi pale pale Gairo, kiwanja ameshapata na sasa yupo kwenye hatua za awali za kuanza kufyetua tofali aanze ujenzi.
Kuhusu kuajiriwa ameshasahau hilo zamani sasa anapambana na hali yake. Mpaka sasa Jojina bado hajaolewa kwa hiyo anayetaka mseleleko fursa hiyo. Nenda Gairo utampata Madam Jojina.

Upvote
3