Kuna jamaa yangu yuko Ifakara anatafuta laptop mpya. Ana kiasi cha shilingi laki tano na nusu (550,000/=). Naomba tumwelekeze kama anaweza pata kwa bei hii na ni aina gani anaweza kupata. Akiambiwa na sehemu, i mean duka la kwenda si mbaya pia
Nawasilisha
DDDuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh!!Vp naweza pata commision?
Yeye anataka iweje kwani? Iwe na vitu kama nini?
Mkuu nilidhani kazi ya udalali umekwisha achana nayo.maisha ni magumu sana, Mpwa tafuta ajira nyingine.YoYo anataka kuanzisha kanisa amekuambia?Vp naweza pata commision?
Unasikia Fidel80 jamaa actually sio mtaalamu wa kompyuta ila anataka laptop mpya na sasa hivi kanidokeza kuwa iwe either DELL au HP na window 2007. Sasa nami sio mtaalamu kihivyo ndio maana nimeleta ombi lake hapa. Mimi nafikri tumsaidie kupata mpya nzuri, mshikaji mwenyewe ana-deal na mambo ya utafiti kwa hiyo sidhani kama itakuwa kama ya watu wa ujenzi
Mkuu nilidhani kazi ya udalali umekwisha achana nayo.maisha ni magumu sana, Mpwa tafuta ajira nyingine.YoYo anataka kuanzisha kanisa amekuambia?
mkuu laptop mpya (brand new) kwa bongo hapa labda kuanzia $700 kwa hizo hp au dell. zipo aina nyingine kama Acer unaweza kupata hata kwa $600.
bei mara nyingi zinategemeana na ubora na specifications.
mfano kwa $700 unapata kitu safi kinakuwa na hard disk ya zaidi ya 120GB, 1GB ya RAM, Core Dual Processor ya 1.7GHZ na kuendelea, DVD R/W. hivi ni vitu vya uhimu, lakii zingine zinakua na vikorombwezo kama Wireless Connnectivity(WiFi), BlueTooth, camera etc.
laptop mpya akinunua itakua bomba zaidi kuliko used, kizuri gharama mkuu!!