Joram kiango
Member
- Aug 25, 2013
- 82
- 16
Kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza anae chukua bcom in finance ni muhimu awe na laptop??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza anae chukua bcom in finance ni muhimu awe na laptop??
Kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza anae chukua bcom in finance ni muhimu awe na laptop??
Computer ni lazima hata ukiwa darasa la 5
Nunua flash uwe unagongea pc kama huna uwezo wa kununua. .
Kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza anae chukua bcom in finance ni muhimu awe na laptop??
akhsante mkuu nimejaribuu kujiregister kupata elimu ila vitabu ndo sijui ntavipataje...wanauza bei kubwa afu online ni hadi uwe na VISA card...hili ni tatizo lingine...sijui library za vyuo vyetu hivi vitabuu vitakuwepoHahaha, muuliza swali umetisha leo!! mwanafunzi yeyote wa chuo ni sio kua na laptop tu, bali access na internet ya kutosha, tatizo la wanafunzi wa Tanzania ndio linakuja hapo, wanachukulia kusoma ka adhabu vile, au kusoma ni ile kwenda shule unamsikiliza mwalimu unafanya mtihani afu imetoka. Kusoma bna ni kuongeza knowledge, lazima upende kujua kitu kwa undani zaidi hata ya mwalimu wako, lazima upende kujua kitu kulingana na dunia inavokwenda na kujaribu ku-make something new ambacho ni bora zaidi ya hapo, ndivyo wanafunzi wa nje wanavyofanya, yani bongo ni wavivuuuuuu ndio maana last year 95% ya form four walienda chaka, unataka uniambie asilimia yote hiyo ni kua hawana access nzuri na elimu? tena katika hiyo 5% asilimia kubwa ni watoto wa maskini na avarage families, kuna softwares mfano iTunes U, sites kama coursera.org na edx.org wanatoa FULL COURSE mbalimbali tena BURE, na hizi lectures ni kutoka vyuo bora duniani eg. Harvard, MIT, Yale etc.. na nikwambie ukweli, hawa jamaa walifikiria Africa hakuna watu safi ndio maana wakaanzisha hii kitu, ila aibu only 3% ya waliyokwenye hii site wanatoka Africa, 97% wanatoka kwingine. Wewe unasoma finance, kichwani unaweka umalize uende uajiriwe ukae uvae tie, unadhani maisha mepec hivo? soma na course nyingine mfano ukichukua CS50 ya Harvard Intro to Comp Science, ukajifunza programming, unaweza ukatengeneza apps zako mwenyewe ndogondogo za finance since utakua umesoma finance, Usikae ukachoka kusoma ati kisa wewe ni finance ukadhani vingine havina maana, kuuliza hivo inaonyesha kabisa hata uwezo wa computer ni mdogo, nani atakuajiri sasa kama computer hujui? Mimi siku wanafunzi wa Tanzania mkubadilisha ideology zenu kuhusu elimu ntawaona watu wa muhimu sana, kwa njia hii.. ndio maana siku hizi graduates wengi wanaishia doro tu mtaani, kubangaizabangaiza tu
kompyuta ni muhmu maana kuna vitabu huwezi nunua zaidi ya softcopy ila kama hujiwezi unakua na flash halafu unaazima za watu..japo unajua madhara ya kutegemea vya watu..binafsi 1st year nlikua na flash tu nkajichanga 2nd year nmenunua yangu
Nunua flash uwe unagongea pc kama huna uwezo wa kununua. .
Kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza anae chukua bcom in finance ni muhimu awe na laptop??
Mnatumalizia muda laptop au chochote kinachoweza kukupa uwezo wa kusoma na full access ya internet, uchape kaz yako, uhifadhi notes, someni watoto baba zenu tunatamani enz hz zingekuwa zetu tungegundua kitu kama akina Plato, Max,nk.
Mawazo ya ki-Afrika Afrika haya! Watu wanatucheka sana! Eti unakuwa na flash tu halafu unagongea kwa wengine! Hiyo nayo imekuwa sigara? Tuache mawazo ya kitindiga haya! Watu mnapewa pesa halafu mnakimbilia Sub hoofer na kunywa pombe, ili laptop mkagongee?! Hapa si ndo mwanzo wa kulaumu watu jamani? TUBADILIKE!