Laptop ni muhimu kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza??

Laptop ni muhimu kwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza??

akhsante mkuu nimejaribuu kujiregister kupata elimu ila vitabu ndo sijui ntavipataje...wanauza bei kubwa afu online ni hadi uwe na VISA card...hili ni tatizo lingine...sijui library za vyuo vyetu hivi vitabuu vitakuwepo
Kama umejiregister kwenye moja ya hizo site, na ukifuatilia ni lini course inaanza online ofcoz ni muhimu na kama utakua unafanya offline downloading ili hizo lectures uweze kuzitazama muda wowote na kurudia ili upate vzr kinachoongelewa ni nini, na mitihani pia wanatoa ukimaliza wanakupa cheti (kwa baadhi ya courses) vitabu kwa kua uko Tanzania ntashauri tu utumie torrents, vitabu vingi hua vinapatikana kwenye torrent sites kama kickass.to au thepiratebay.sx hata uki-google, sema unataka vitabu gani!
 
Computer ni lazima aisee ila kama mshiko haujalakaa vizuri angalia kama library ya chuo unachoenda inakidhi mahitaji unaeza kununua baadae ila tatizo litakuja kwenye kufanya assignment alaf vitabu vinapoteza muda keene kufanya kazi na kusoma japo kusoma vitabu ni muhimu..KWANGU NI LAZMA..
 
Mimi nilimaliza chuo kikuu bila laptop,inawezekana nawe ukafanya hivyo kama hauna uwezo wa kuinunua kwa sasa ila nayo ina umuhimu wake hasa mnapopewa individual assignment
 
mtoa mada nakumbuka mimi nishatupia uzi kama huu uliotupia..so umerudia mada..samahani lakini...
 
Hahaha, muuliza swali umetisha leo!! mwanafunzi yeyote wa chuo ni sio kua na laptop tu, bali access na internet ya kutosha, tatizo la wanafunzi wa Tanzania ndio linakuja hapo, wanachukulia kusoma ka adhabu vile, au kusoma ni ile kwenda shule unamsikiliza mwalimu unafanya mtihani afu imetoka. Kusoma bna ni kuongeza knowledge, lazima upende kujua kitu kwa undani zaidi hata ya mwalimu wako, lazima upende kujua kitu kulingana na dunia inavokwenda na kujaribu ku-make something new ambacho ni bora zaidi ya hapo, ndivyo wanafunzi wa nje wanavyofanya, yani bongo ni wavivuuuuuu ndio maana last year 95% ya form four walienda chaka, unataka uniambie asilimia yote hiyo ni kua hawana access nzuri na elimu? tena katika hiyo 5% asilimia kubwa ni watoto wa maskini na avarage families, kuna softwares mfano iTunes U, sites kama coursera.org na edx.org wanatoa FULL COURSE mbalimbali tena BURE, na hizi lectures ni kutoka vyuo bora duniani eg. Harvard, MIT, Yale etc.. na nikwambie ukweli, hawa jamaa walifikiria Africa hakuna watu safi ndio maana wakaanzisha hii kitu, ila aibu only 3% ya waliyokwenye hii site wanatoka Africa, 97% wanatoka kwingine. Wewe unasoma finance, kichwani unaweka umalize uende uajiriwe ukae uvae tie, unadhani maisha mepec hivo? soma na course nyingine mfano ukichukua CS50 ya Harvard Intro to Comp Science, ukajifunza programming, unaweza ukatengeneza apps zako mwenyewe ndogondogo za finance since utakua umesoma finance, Usikae ukachoka kusoma ati kisa wewe ni finance ukadhani vingine havina maana, kuuliza hivo inaonyesha kabisa hata uwezo wa computer ni mdogo, nani atakuajiri sasa kama computer hujui? Mimi siku wanafunzi wa Tanzania mkubadilisha ideology zenu kuhusu elimu ntawaona watu wa muhimu sana, kwa njia hii.. ndio maana siku hizi graduates wengi wanaishia doro tu mtaani, kubangaizabangaiza tu
Umesema vizuri kaka, hiyo ya edx hata mimi na irecomend, ni nzuri sana na imesheheni vyuo bora zaidi duniana na kila siku kozi nyngi zinaongezeka, ila bado kuna changamoto kwetu sisi tunaotokea Afrika, ni Upatikanaji wa internet ya Kasi zaidi ili kuangalia video za lecture na pia kushiriki katika group discussion, mimi nilijaribu lakini nikaona hiyo pia ni changamoto, kitu kingine pia ingawaje kozi hizi zinatolewa bure kuna vitabua ambavyo utahitajika uvinunue na vingi huwa vipo online-onlineshopping kwa nchi za kiafrika bado ni changamoto, kwa hiyo pengine ndio maana unaweza sema kuna hiyo asilimia chache kutoka Afrika. Ila kama kuna mtu anataka kupanua fikra zake na kujiongezea potential ya kuimiliki vizuri career yake na pengine ana sparetime ya kutosha mi namshauri akasome kozi zinazotolewa na edx.
 
Back
Top Bottom