Computer4Sale Laptop toka USA zinauzwa

Computer4Sale Laptop toka USA zinauzwa

Nilitaka kutia neno, nikaona hii biashara, nisije kuharibu biashara ya mtu.

Lakini kwa kuwa umeniuliza, mimi sina tabia ya kukimbia swali na sitaweza kuanza leo.

Hizi computer kwa miaka mingi zilikuwa zinatumia Hard Disk Drive. Hizi zinazunguka, kuzunguka huku kunasababisha ziwe na kelele, ziwe zinakula umeme sana na zinapata joto sana.Pia ziko slow, kwa sababu data inatafutwa katika disc inayozunguka.

Miaka ya karibuni, kukaja letwa teknolojia mpya ya SSD (Solid State Drive). Hizi hazizunguki, ziko faster kuliko HDD, zinatumia umeme vizuri zaidi, hazipati joto sana. Tatizo moja ni capacity, si rahisi kukuta SSD kubwa kwa bei nzuri.

Hizo sizes za GB 300- 500 kwa sasa laptop mpya nyingi ni SSD. Ndiyo maana nikaona niulize, hizo laptop storage uliyoweka hapo ni SSD au HDD?

Watu wengi washazoea "HDD", kwa hiyo mpaka SSD wanaweza kuziita HDD.

Kama unataka laptop fast, isiyotumia betri sana, isiyo na kelele, isiyoshika joto sana, na itakayoacha data zako salama kutoka nguvu za usumaku, kwa sasa hivi ni vizuri kununua yenye SSD, siyo HDD. Au unaweza kununua yenye HDD ukabadili na kuweka SSD kama mautundu hayo unayo au unajua mtu anayeweza kukufanyia hivyo.

Kama unataka kusoma zaidi in detail, kuna mtu kaandika kuchanbua tofauti za SSD na HDD kitaalamu zaidi hapa.

Mkuu kama kawaida haujawahiniangusha linapokuja suala la kuelimisha jambo.
Kwa kuongezea tu HDD iko mechanical wakati SSD ni Digital. HDD ni kama CD za kawaida hizi za nyimbo/ video zimewekwa nyingi na lazima zizunguke inapofanya kazi. Pia ni rahisi kuharibika hasa inapodondoka au inatokea tu baadhi ya sehemu zinagoma. Hapo unapoteza kila kitu. Na data recovery huku kwetu inahitaji uwekezaji mkubwa. SSD zimeleta mapunduzi makubwa sana.
 
Back
Top Bottom