Larry Madowo aja na Documentary ya kuonesha jinsi Urusi inavyoshawishi Waafrika kwenda kufa vitani Ukrein

Larry Madowo aja na Documentary ya kuonesha jinsi Urusi inavyoshawishi Waafrika kwenda kufa vitani Ukrein

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Miezi ya Juzi kati nilikuja na chapisho la jinsi Waafrika waliokuwa wanaimba kwa Kiswahili walivyokuwa wanadhiakiwa kwa lugha ya Kirusi kwamba hawa ni takataka tu (Disposable) na wanaenda kuwekwa Frontline yani mstari wa mbele vitani.

Sasa Larry Madowo kupitia kituo cha CNN kafanya full Documentary ya Waafrika waliojiunga na jeshi la urusi kwa ajili ya kuisaidia nchi ya Urusi kushinda vita. Wengi wakiahidiwa mishahara minono, pesa nyingi, na kupewa uraia na kazi huko nchini Urusi.

Lakini mambo yamekuwa tofauti badala yake wengi wao wamekuwa wakipelekwa mstari wa mbele vitani hili kuwa kama chambo kumfichua adui au kufichua hatari zozote zilizoko mbele huku Wanajeshi wa Urusi wakiwa nyuma.

Tamaa za mafaniko zimekuwa zikiwaponza wengi, huku hata Mtanzania amewahi kuripotiwa kufariki vitani akipigania Urusi.


View: https://www.instagram.com/reel/DUVX-s8CYjs/?igsh=MXEwejduc2pmZ3l3MQ==

Soma zaidi: Wanajeshi wa Urusi wawaita Wanajeshi wa Afrika "Takataka" wakiwa wote vitani Ukrein
 
Kwani hao wana utofauti na wale wa ford foundation na waliojificha kenya?
 
Pamoja na hayo yote Waafrika bado wataendekeza tamaa bila kujali matokeo yake
 
Huyo Shoga Larry Madowo ndo alitaka na vijana wetu waharibu nchi yao ili wakimbilie huko?
 
Back
Top Bottom