Last seen ya mpenzi wako WhatsApp!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari wana MMU.

Kwa wale wanaotumia hii App au kama unaifahamu ni kwamba unaweza kujua kwamba mtu kama anatumia simu wakati gani na mara mwisho kuitumia ilikuwa muda gani.

Lengo la kuanzisha huu uzi.

Je kama unawasiliana na mpenzi wako na umehakikisha kwamba yupo Online kwa wakati huo ikimaanisha ukimtumia message basi instantly au wakati huohuo anaipata.

Naombeni ushauri wenu wakuu kuna mpenzi wangu sijui ana matatizo gani, kila unapomtumia message inafika lakini haijibu mpaka anatoka Online na kurudi tena hana habari na message yangu, anakuja kujibu muda umeshaenda sana hata ukimtumia kwa njia ya kawaida Text message anachelewa kujibu, simu yenyewe kupokea mpaka upige mara tatu au nne na pengine hapokei kabisa! Hatujagombana kwa lolote na mpenzi wangu.

Wakuu hili jambo linanikwaza sana naombeni ushauri wenu,..
 
Sasa mkuu kama anaona na hakujibu ni tatizo kwa haraka haraka huyo ashanasa sehemu nyingine.
 
The best practice ni kumtreat kama anavyokutreat kwa sababu, yawezekana hajazoea kuwasiliana mara kwa mara...ama its just too much for her kila saa kupokea sms. Ukiona mkienda sawa kwenye mawasiliano hakukuridhishi na hakuna namna atabadilika then maybe you are just not cut for each other.
Alternatively, unaweza kuongeza mvuto kwenye mazungumzo
 
Mkichat huwa unaongea nini? Inawezekana maongezi yako si mazuri. Kuna mtu mwingine ukianza kuongea nae hutamani kumaliza ila wapo wengine ukiongea dk mbili yanaanza maswali umevaa nini? Mara uulizwe eti umelalaje? Hell....kesho utakuwa na hamu ya kuchat nae au kupokea simu na mazungumzo yake mabovu kiasi hicho?
 

mmmh!!! sa ndo umwambie vya kuongea, asije kuaribu kabisa.... ndo mana gash wang nmembrok watsap lol!!!
 
Huyo bibie ni mwenyeji love connect?juzi tu ulikuwa unasaka mbona huleti mrejesho
watu bado tunakuwaza ujue
 
Hapa tatizo sio last seen. Hapo tatizo ni mpenzi wako, nawe karibu kutomtafuta mpaka akutafute. Akikutumia sms jibu baada ya siku moja akikwambia uwende mwambie umebwana na mishe zako mpangie siku ya kwenda ww. Mwenyewe atasema poo.
 

Kweli mom umenena vyema ajitathimini katika maongezi yake anaweza akawa ndo chanzo cha tatizo.
 
nmemwambia simu mbovu, bora atume normal txt.... wakati mwingine inakela mtu yupo online afu hajibu, japokua anaeza kua na issu zingne

Hahaaa duuuh....hii kali ngoja na mimi nifanye upembuzi yakinifu mahali fulani hivi.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…