LAT, Voice of a Reason, Malila, Ameoba na wengine wengi...

Linapokuja swala la kuwekeza hua sichelewi sana kuingia na kucheza hiyo ngoma.Mawazo yangu ni haya, kuna fursa nyingi ktk kilimo na mitaji yake sio mikubwa sana,tunaweza vamia pori kubwa bila kununua na tukaanzisha kijiji cha mifugo, mipori iko mingi sana haina wenyewe. Wazo la pili, ninalirudia, twende ktk miji midogo inayokuwa ( Kimanzi/Chalinze/segera nk) tupate eneo kubwa na kulifanya service center, silaha yetu kubwa iwe huduma bora kwa wateja. Naamini inaweza kuwa nembo ya mji huo kwa huduma zetu.

Tumejaribu ktk project ya misitu na tumefanikiwa sana, sasa hivi tunaendelea na uwekezaji ktk shamba dogo la kuku, ardhi tunayo tayari na jengo la kuanzia lipo, hatujaanza na jogoo kama alivyoanza NM bali tumeanza na tetea nane kwa kuwatoa huku huku pwani na jogoo wa jirani.
 

Mkuu my point exactly badala ya kuanza na vitu vyenye overheads kubwa ni vizuri kuanza na kitu kama hiki, tena tunaweza tukafanya experimenting ya bidhaa ambazo zina soko sana hata nje ambazo watu wanaogopa kuzifanya au hawajazifanya. Packing nzuri na processing na sababu tupo wengi tutapata soko tu, am with you on this one
 

Tatizo nipo Guantanamo kwa leo, ningeomba tukutane siku yo yote, tunaingiza hii maneno kwa operation kabisa, halafu uone nini kinaendelea baada ya miezi sita tokea siku tumeamua. Hata kiwanda cha kusindika maziwa tushindwe kumiliki, tunao watalaamu wa b/ness plan kibao, kila mmoja akichangia kwa kile alicho nacho lazima tutoke na kitu kizito.
 
@ Malila & VoiceOfReason

mimi nakubaliana na nyinyi 100% , pamoja na kuwa na mawazo mengi ya sustainable investments, naomba tuende kwenye action plan, tuwe na wazo dogo la mwanzo litakaloweza kutukutanisha na pia kuanzisha a pilot project while we are engineering for other investment ideas

mimi nadhani kwa kuanzia tufungue ranchi ndogo ya mbuzi kwa ajili ya nyama (goat meat), tunawanunua mbuzi wa wastani na kuwaboresha kwa kuwaongezea afya, uzito na usafi (showing of goat for meat) , eneo liwe karibu na dar ambapo soko lake lipo wazi na zuri, nadhani hapo hatuhitaji mtaji mkubwa, anayeweza kufanya mahesabu ya haraka haraka atusaidie, kubwa hapa ni upatikanaji wa eneo na kwa kuanzia tunahitaji eneo la wastani wa heka tano hivi, kinachofatia ni a simple barn (banda kubwa la mbuzi), wafanyakazi wawili na mnunuzi ya mbuzi, tunuie kuanza na mbuzi 200 heads
 

Okay kwa haraka haraka mbuzi kumnunua mdogo kabla ya kumlisha ni kiasi gani na akishafikia marketable price ni kiasi gani kumuuza
Na is it cheaper and more profitable kuwa-breed kabisa au..?
Na soko lake vipi hapo Bongo kuna mdau niliona kwenye post fulani anasema hii issue hata Comoro hii nyama inalipa sana.
 

mkuu

uki source mbuzi kutoka maeneo yasiyo ya mbali kama vile maeneo yaKiyegea, Berega, Gairo na mlali morogoro unaweza pata mbuzi wa wastani kwa Tsh 25-30,000 ukiwasafirisha kila kichwa say Tsh 3,000, baada ya kufika ni kuwanunulia grains kidogo kama pumba, seed meals (cotton & sunflower) madawa kama ya kuogeshea, antibiotics and deworming havina garama kubwa, zoezi la kuhasi mbuzi ndilo litakalotupa ubora (ndafu)

baada ya miezi miwili na nusu mpaka mitatu waweza kuuzwa kwa Tsh 70-90,000, hii ni bei ya jumla, kumbuka kwamba kwenye ranch tutaendelea kufanya breeding na pia mbuzi wengine tutakaonunua porini tutakuta tayari wana mimba
 
Semeni wenyewe, ardhi mnataka iwe na sifa zipi ili niwaambie sasa hivi? Mbuzi msihangaike kwa kuwa ninajua walipo na kwa bei nzuri iliyotajwa hapo juu.
 

Mkuu Malila,

Nilikuomba contacts za hao jamaa wa kuandika Business Plan ukapitiwa...huu mji umejaa matapeli...please nipatie namba zao kama ni watu makini...


By the way...navuna vitunguu in (2 weeks time)...subiri picha kibao!!!

Soames.
 
Malila, VOR, Mlachake

tukiji mobilize 20 members each with a start up capital investment of 1M we can start a mini goat meat ranch, 200 heads to start with a target of 1,000 heads within a year and a cycle stock in and stock out (sales)
 
Mkuu Malila,

Nilikuomba contacts za hao jamaa wa kuandika Business Plan ukapitiwa...huu mji umejaa matapeli...please nipatie namba zao kama ni watu makini...


By the way...navuna vitunguu in (2 weeks time)...subiri picha kibao!!!

Soames.

Mtwangie huyu jamaa 0784695579, nina mfahamu sio kwa sura tu hata kwa vitendo kwa sababu ninafanya naye mambo fulani, ni kijana mwenzako na office yake iko city center.Ww mwambie mimi ndio nimekupa namba yake.
 
Malila, VOR, Mlachake

tukiji mobilize 20 members each with a start up capital investment of 1M we can start a mini goat meat ranch, 200 heads to start with a target of 1,000 heads within a year and a cycle stock in and stock out (sales)

Tunaweza kabisa kubadilisha upepo, hamjatoa maoni yenu kuhusu ardhi, huku tunajadiliana na mengine yawe yanafanyika taratibu.
 
malila

hii project inawezekana kabisa tena bila kuvuta muda, tena hakuna hata procedures zenye beauracracy mahali popote pale, tutatengeneza MoU ya umoja wetu, this can be achived even within one month with everything set in place

huu mradi utakuwa ni mfano mkubwa sana, mimi ninamatumaini ya mambo mazuri baadae kwani mifugo pia ni rasilimali kubwa iliyopo na hatuiendelezi na kuitumia ipasavyo

tukifikia ishirini tufanye mpango wa kukutana mara moja

kasopa, kiraka, malila, VOR & LAT very encouraging spirit
 

Kuna mahali nilimpeleka Kasopa kuangalia kama pangemfaa, hakupachukua kwa wakati ule, barabara ipo, maji yapo ya kijito mwaka mzima,tambarare fulani hivi, kuna eka 50 ready for disposal, kizuri zaidi tunaweza kupanua taratibu hadi kufikia ukubwa tunaoutaka, japokuwa kuna vifisadi uchwara kadhaa vimechukua mapande karibu na hapo,bei bado ni nzuri sana.

Mimi naendelea na kutafuta ardhi inayoweza kutufaa kwa muda mrefu bila migogoro na majirani zetu.
 
wakuu

ngoja nitoe dokezo la market potential ya product ya hii project yaani commercial goat meat ranch au raising of goat meat

katika jiji la dar kuna tafrija, sherehe za harusi, sherehe za dini mbali mbali, graduations, birtdays na nyingine nyingi za kifamilia na hata kijamii matukio yote haya hitaji lake mojawapo ni nyama ya mbuzi kwa matumizi, mara nyingi mbuzi huchukuliwa akiwa hai na kutayarishiwa sehemu husika ya tukio, hivyo utaona upatikanaji wa mbuzi hai hutegemea sana sana vingunguti na baadhi ya wafugaji wadogo wadogo sana, hivyo basi hawa ndiyo target market ya kwanza

another target market segment will be dar es salaam bars that sells barberque goat meat (mbuzi choma) and soups

ukiangalia hali halisi ya vingunguti haikidhi market segment niliyoitaja, kwanza eneo lake lipo bila pmangilio, utaratibu wa manunuzi ni mbovu, security ya wateja ni ndogo,hali ya usafi katika soko ni mbaya kubwa zaidi ni mbuzi wa vingunguti hwana ubora, mbuzi hawa hutolewa mikoani wakiwa wanunuliwa kwenye minada na magulio, kwa utafiti wa kawaida mbuzi wengi kwenye minada huuzwa na wafugaji kwa kulenga sababu husika, wengi ni wale wasio na afya na hata wenye matatizo kiafya, mbuzi hawa husafirishwa hata kwa umbali mkubwa sana kwa kutembea hivyo huchoka na kupoteza afya, mbaya zaidi wakifika dar hufungiwa muda mrefu bila matunzo mazuri, risk ya magonjwa kwa mbuzi hawa pia haikwepeki

therefore there is a need for a source of good and healthy meat goats

keep in mind in future the project will diversify its market segments to supermarkets, hotels and meat butcheries
 
Kaeneo ka kwanza wanasema bado kapo. Mungu akipenda,siku tunakutana kila kitu kipo mkononi, ni suala la kupanga action plan,kama hivi suala la soko liko vizuri, pande la ardhi liko 80% linaweza kupatikana lenye viwango, bado idadi ya timu tu, kisha tunapanga mkutano wa kwanza.
 

great !

good news
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…