Linapokuja swala la kuwekeza hua sichelewi sana kuingia na kucheza hiyo ngoma.Mawazo yangu ni haya, kuna fursa nyingi ktk kilimo na mitaji yake sio mikubwa sana,tunaweza vamia pori kubwa bila kununua na tukaanzisha kijiji cha mifugo, mipori iko mingi sana haina wenyewe. Wazo la pili, ninalirudia, twende ktk miji midogo inayokuwa ( Kimanzi/Chalinze/segera nk) tupate eneo kubwa na kulifanya service center, silaha yetu kubwa iwe huduma bora kwa wateja. Naamini inaweza kuwa nembo ya mji huo kwa huduma zetu.
Tumejaribu ktk project ya misitu na tumefanikiwa sana, sasa hivi tunaendelea na uwekezaji ktk shamba dogo la kuku, ardhi tunayo tayari na jengo la kuanzia lipo, hatujaanza na jogoo kama alivyoanza NM bali tumeanza na tetea nane kwa kuwatoa huku huku pwani na jogoo wa jirani.