LAT, Voice of a Reason, Malila, Ameoba na wengine wengi...

malila and VOR

please we need a calculator for costs estimates/proposed budget

tupo mahali pazuri
 

idea granted with pleasure
 
Wakuu count me in kwenye hiyo project!

Wakuu, naomba tumpendekeze kiongozi mkusanya pesa, ili november hii tukutane Dar na kununua pande la ardhi. Mafisadi wanasoma huu uzi na kuufanyia kazi sambamba na sisi kwenye location hizo hizo tunazozitaja hapa.Tujitoe mhanga na tukusanye fedha, na hapo ndio tutajua nani yumo na nani longo longo, watakaokuwa wamekusanya waanze fasta bila kusita.
 
malila and VOR

please we need a calculator for costs estimates/proposed budget

tupo mahali pazuri

Kwa sasa tutahitaji kujitolea sana kwa mambo mengi ili tufanikiwe, kwa pamoja tuseme tunahitaji eka ngapi za kuanzia, malipo yake yakoje (kama tutakodisha au tununue), banda la farm meneja liwe na ukubwa gani na gharama zake, mbuzi wa kuanzisha kijiwe wawe wangapi( mimi nilishauri 20 wa umri mchanganyiko), na farm meneja atapatikanaje? Maoni ya wote ni muhimu sana.

Kama mtaridhia mimi nishushe maoni yangu haina shida.
 
Project : Raising of Meat Goats

Proposed Budget

Project cost summary

1. Capital Investment
1.1 Land ======= proposased 10-20 acres
1.2 Buildings
Staff ===== one bedroom and store simple shade
Livestock (Goat) barn, fence ====== 5x15 meters suspended wood & log shade (mabanzi na nguzo), with corrugated iron sheet roofing

2. Plant , Machinery & Equipments
2.1 Accessories - Spray pump, Baddizo
2.2 Water tank
3. Motor Vehicle
Not now

4. Furniture & Fittings
Not now

5. Pre operational expenses
5.1 feasibility costs
5.2 aquisition of land expenses
5.3 mobilization expenses

6. Working Capital
6.1 costs of livestocks grains and fodders for 6 months
6.2 salary and wages for 6 months @ 2 workers
6.3 veterinary expenses for 6 months

7. Stocks
7.1 Cost of 50 heads goats (bucks, does and wethers)
7.2 medicines and vaccinations

8. Utilities and consumables
8.1 telephone charges
8.2 water & electricity
8.3 transportation charges

Total amount =======================

wakuu , naomba tuchangia kujaza hii budget
 
Nikushukuru kwa kunyambulisha mahitaji ya project yetu. Nitachangia kwa vipengere ninavyoweza.
 

Nitachangia kadiri nijuavyo kwa sasa, ili wakuu wa hesabu wapate pa kuanzia.
 
malila

thanks for that

- kwakuwa hatuna umeme basi tanki tutalijengea kitako juu kidogo kama 2.5 feet ili iwe rahisi kuweka maji yanayochotwa kwa ndoo na pia kuyafungua kwa bomba dogo kwa ajili ya matumizi
- phones ni ya manager na mmoja ya keepers
- the salary is inclusive his own upkeep including meals but we may grant medical care to our workers
-spray pump for washing, sanitation and fumigation is around TSh 80,000 15ltrs capacity, Baddizo (bucks fatening) is also Tsh 70,000 kifaa kwa ajili ya kuhasi mbuzi
- stock ya dawa za minyoo, antibaotics (OTC 20%) na dawa za kuogeshea for six month for 50 heads can cost around Tsh 50,000
- stock ya mbuzi Tsh 35-40,000 per head inclusive transportation x 50 heads
 
-Tumesahau baiskeli ya kijana ni laki moja na nusu, japokuwa in future tutanunua boda boda moja.

Wakuu, pendekezeni mtu wa kukusanya michango ya awali, wakati haya ya budgeting yanaendelea watu tunaanza kupunguza michango ili kufikia lengo fasta.
 
kwa wale ambao sasa hawapo nchini lakini wanataka kuwemo 100% kwenye mradi, je wao watalipa gharama sawa na waliokuwepo? malila nakutegemea wewe mkuu.
 
kwa wale ambao sasa hawapo nchini lakini wanataka kuwemo 100% kwenye mradi, je wao watalipa gharama sawa na waliokuwepo? malila nakutegemea wewe mkuu.

Mpaka sasa, hatujaanza kukusanya fedha, lakini ndani ya week hii naamini tutaanza, kwa sababu tunajaribu kuweka makisio sahihi,tukikamilisha proposal zetu kama unavyoziona jukwaani, tutaona kila mtu anatakiwa mchango kiasi gani. Sasa kama uko majuu, hakuna ugumu wo wote ule, niko na jamaa watano huko majuu na siwajui na nina fanya nao project vizuri, na mwingine hata hii project ameomba asiachwe, kama itakuwa shida kwako kutuma mchango basi tujulishe ili tuone jinsi ya kufanya sisi sote kama group.
 
tuko pamoja mkuu haina shida.
 
Mchakato wa LAT umekaa vizuri,Malila nashauri uchukue Jukumu la kuwa Interim Finance controller mpaka mradi utakapo simama.

Tutarajie kuanza na kiasi gani per individually?
 
Mchakato wa LAT umekaa vizuri,Malila nashauri uchukue Jukumu la kuwa Interim Finance controller mpaka mradi utakapo simama.

Tutarajie kuanza na kiasi gani per individually?

Naweza kufanya kazi hii ya kukusanya fedha za kununulia shamba, november nitakuwa na muda mzuri wa kuhangaikia shamba letu hili mpaka litiwe mkononi. Shamba likisha patikana, itabidi tutafute mhasibu/mtunza fedha wa project. Mimi nakuwa nje ya Dar mara nyingi.

Naomba tulenge Tsh 330,000/ kama kianzio/kiingilio, fedha hii ikikusanywa toka kwa watu kumi tu,inatosha kukamata eneo la kuanzia. Kama wanabodi wataunga mkono hoja yako hii ya mimi kukusanya fedha, basi naomba tuchague njia ya kukusanya fedha. Je M-Pesa itafaa? Naamini zaidi bank. Ngoja tusubiri maoni ya wenzetu.

Naingi Dar november 8, ningependa kabla ya jumamosi ya tarehe 12/11/2011 tuwe tumelipia advance ya shamba. Niombe pia, sisi ambao tunakuwa nje ya Dar ( Malila,Kasopa, Kishaju,Manundu) tuhakikishe kazi hii ya kulipata shamba tunaifanya november hii, ili tukirudi porini walioko mjini nao waendelee na vikao na plan zingine.
 
wakuu

pamoja na kuendeleza mapambano haya bila ya kusita wala kusuasua, mimi ningeshauri kwamba tupange siku ya kukutana ili tufahamiane vizuri zaidi, kupanga mikakati zaidi na kukubaliana aina ya umojawetu huu katika hii project, kwa urahisi bila kuwa na mlolongo mimi nashauri tusajili business name ambayo itakuwa legal with the partnership deed, hii registration ninaweza kuifanya ndani ya siku moja tukapata business name certificate pamoja na Rigestrar Extract/partneship deed, registration hii haizidi Tsh 10,000 in which personally i can offer for this,

mambo haya yote yaende sambamba bila kutegemeana

twaweza sasa kutoa mawazo ya jina la project kwa usajili, vile vile tunaweza anza kufanya mawasiliano ya group e.mail with our true identities

nawakilisha
 

Naunga mkono,ni vizuri tuwe na jina na group mail ili mawasiliano yaende barabara. Napendekeza yafuatayo

Mzalendo farm
Jamii farm
Pamoja farm
Umoja farm
Nimependekeza majina ambayo hayataleta tafsiri za ajabu. Na wengine changieni ili tupate jina ambalo litatumika ktk usajili wa jina na group mail.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…